YUKO MUNGU MMOJA TU WA KWELI.

Na mtumishi Peter Mabula.

BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze jambo muhimu sana.
Yuko MUNGU Mmoja Tu Wa Kweli Na Wa Pekee.
Naomba ufuatane nami mwanzo hadi mwisho huku tukiyapitia maandiko ambayo ndiyo pekee yaliyo kweli ya daima. 

1 Wafalme 8:60 ''Watu wote wa ulimwengu wajue ya kuwa BWANA ndiye MUNGU; hakuna mwingine.''

- Biblia imeweka wazi kabisa kwamba dunia kama inataka kumjua MUNGU wa kweli basi BWANA ndie MUNGU wa kweli. Ukiangalia maana ya jina BWANA katika kamsi ya kiswahili sanifu utaona kwamba BWANA maana yake Mwenyezi MUNGU, Mola au Muumba. Muumba ndiye pekee mwenye sifa ya kuitwa MUNGU maana ndivyo alivyo.  Kwenye Biblia limeandikwa kwa herufi kubwa likiwa na maana YAHWEH au JEHOVAH.
watu wengi wanachanganyikiwa kwa sababu hawajui kwamba Mungu sio jina ila ni sifa  lakini BWANA ni jina  tena ni sifa. 

sifa ya MUNGU wa kweli ni 
=Ni Muumbaji.

Mwanzo 1:1, '' Hapo mwanzo MUNGU aliziumba mbingu na nchi. '' 
 Na ndio maana hiyo hiyo inasema  

'' Njoni, tuabudu, tusujudu, Tupige magoti mbele za BWANA aliyetuumba.-Zaburi 95:9 ''.

Hata ningeishia hapo tu ungekuwa sasa umemjua MUNGU wa kweli ambaye aliumba mbingu na dunia na peke yake huyo ndie anayestahili kuabudiwa.
=Sifa nyingine ya MUNGU ni Anatawala pote
 
 Isaya 45:18 '' Maana BWANA, aliyeziumba mbingu, asema hivi; Yeye ni MUNGU; ndiye aliyeiumba dunia na kuifanya; ndiye aliyeifanya imara; hakuiumba ukiwa, aliiumba ili ikaliwe na watu; Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine.''

MUNGU Amejifunua kwetu wanadamu Katika Utatu Mtakatifu.

Mathayo 28:19 '' Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la BABA, na MWANA, na ROHO MTAKATIFU.;''

BABA na MWANA na ROHO MTAKATIFU, huo ndio ukamilifu wa MUNGU ndio maana Biblia inaendelea kusema 
'' Neema ya BWANA YESU KRISTO, na pendo la MUNGU, na ushirika wa ROHO MTAKATIFU. ukae nanyi nyote.-2 Kor 13:14''

Utatu Wa MUNGU Ni MUNGU BABA, YESU KRISTO Na ROHO MTAKATIFU. Wengi Inawachanganya Hii Wakitaka Kila Kitu Lazima Kiwe Kama Ufahamu Wa Mwanadamu Ulivyo.
 Unaweza Kujiuliza Haya ili uelewe.

     1.  YESU Ni MUNGU mkuu.

Tito 2:13 '' tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa KRISTO YESU, MUNGU mkuu na Mwokozi wetu;''

=YESU KRISTO aliitwa MUNGU maana ndivyo alivyo.

 Yohana 20:28 '' Tomaso akajibu, akamwambia, BWANA wangu na MUNGU wangu! ''.

=YESU KRISTO kabla hajaja duniani kuwaokoa wanadamu alikuwa ni MUNGU mbinguni.

Wafilipi 2:6-8 '' ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya MUNGU, naye hakuona kule kuwa sawa na MUNGU kuwa ni kitu cha kushikamana nacho;  bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.''

=YESU KRISTO ni MUNGU aliyedhihilika katika mwili kama mwanadamu.
 
1 Timotheo 3:16 '' Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. MUNGU alidhihirishwa katika mwili, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.''  

=YESU KRISTO ni MUNGU katika mwili.

 Wakolosai 2:9 ''Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa MUNGU, kwa jinsi ya kimwili.''.

=Akiwa duniani YESU alikuwa ni mfano wa MUNGU asiyeonekana.

Wakolosai 1:14-15 ''ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi; naye ni mfano wa MUNGU asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.'' 

Nimetaka Biblia iongee zaidi kuliko mimi Peter Mabula ninayekuletea somo hili. ok ngoja tuendelee zaidi.

Nafsi tatu za MUNGU hufanya kazi moja na kusudi moja lenye maana moja.
Akisema ROHO MTAKATIFU hapo ni MUNGU BABA amesema.
Akisema MUNGU BABA hapo ni BWANA YESU amesema.
Akisema BWANA YESU hapo ni MUNGU BABA amesema.
Kwa sababu kazi yangu leo ni kufafanua kwanini kuna MUNGU mmoja tu wa kweli na kwanini MUNGU huyo mmoja tu wa kweli anaabudiwa na WAKRISTO waliookoka?
Linganisha ufafanuzi huu ili umujue BWANA MUNGU wako ambaye ndiye pekee mwenye uzima wako wa milele.

    2.  MUNGU Kama BABA.

Mathayo 13:43 ''Ndipo wenye haki watakapong'aa kama jua katika ufalme wa BABA yao. Mwenye masikio, na asikie.''

=Biblia haiishii hapo tu kuthibitisha kwamba MUNGU ni BABA.

 1 Petro 1:17''Na ikiwa mnamwita BABA, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni.''

=Hakika MUNGU ni BABA mzazi wa roho zetu, kwa amri yake tulizaliwa na kwa amri yake tunaishi na kwa amri yake tutakufa na kwa kuliishi Neno lake tutaenda uzima wa milele kwa walio haki tu. 

 1 Kor 1:3 ''Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwa MUNGU BABA yetu, na kwa BWANA YESU KRISTO. ''

 3.  BABA Alimtuma MWANA 

Yohana 20:21'' Basi YESU akawaambia tena, Amani iwe kwenu; kama BABA alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi  ''

 Na Biblia inaendelea kusema;

 1 Yohana 4:9 '' Katika hili pendo la MUNGU lilionekana kwetu, kwamba MUNGU amemtuma Mwanawe pekee ulimwenguni, ili tupate uzima kwa yeye. ''


4. ROHO MTAKATIFU Alimzaa YESU KRISTO.

Luka 1:34-35 ''Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijui mume?  Malaika akajibu akamwambia, ROHO MTAKATIFU atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa MUNGU.''


 5.  YESU KRISTO Alimtuma ROHO MTAKATIFU.
 
Yohana 15:26 ''Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa BABA, huyo ROHO wa kweli atokaye kwa BABA, yeye atanishuhudia.''

  6. KRISTO Hubatiza Kwa ROHO MTAKATIFU.

Mathayo 3:11 '' Kweli mimi(Yohana mbatizaji) nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa ROHO MTAKATIFU na kwa moto. ''

 7. BABA Na MWANA Ni Mmoja.

Ufunuo 21:22 '' Nami sikuona hekalu ndani yake; kwa maana BWANA Mwenyezi na Mwana-Kondoo, ndio hekalu lake.''

Biblia inaendelea kusema 

Yohana 14:7-9 ''Kama mngalinijua mimi(YESU), mngalimjua na BABA; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona. Filipo akamwambia, BWANA, utuonyeshe BABA, yatutosha. YESU akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona MIMI amemwona BABA; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe BABA? ''

Kumjua MUNGU Kuna Hitaji Ufunuo Kutoka Kwake. Ndio Maana Wahubiri Wanatakiwa Waombe Roho Ya Hekima Na Ufunuo Katika Kumjua MUNGU Ndipo Watahubiri Vizuri.

Waefeso 1:17 '' MUNGU wa BWANA wetu YESU KRISTO, BABA wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye;''

Kwa maelezo hayo na maandiko hayo unaweza ukajiuliza kwa japokuwa ROHO MTAKATIFU alimleta BWANA YESU duniani lakini Biblia kwenye maandiko mengine inasema MUNGU BABA ndio aliyemleta YESU KRISTO, Maana yake hapo ni kwamba MUNGU BABA ndio ROHO MTAKATIFU vile vile.
Japokea Biblia inasema BWANA YESU atamleta ROHO MTAKATIFU lakini maandiko mengine Biblia inasema MUNGU BABA ndio atamleta ROHO wake Mtakatifu, maana yake hapo BABA ndio MWANA.
Unaweza ukajiuliza katika maandiko mengi sana katika agano la kale yanasema MUNGU atakuja kuhukumu wanadamu wote lakini ukisoma katika agano jipya YESU KRISTO atakuja na ndio atahukumu watu wote, maana yake hapo ni MUNGU yle yule aliyesema zamani na ndiye huyo huyo atatimiza hukumu hiyo.
Kumjua MUNGU ni lazima tupate ufunuo kutoka kwake ndipo tutamfahamu vizuri.
Kinachowachanganya wanadamu wengi ni kutokumjua BWANA YESU.
Kuna tofauti kubwa kwa BWANA YESU alipokuwa duniani na sasa akiwa mbinguni.
YESU akiwa duniani ungeweza kusema ni mtoto wa Mariamu lakini sasa BWANA YESU akiwa mbinguni utaona kwamba ndiye aliyeumba watu wote akiwemo na Mariamu maana ndivyo Biblia inavyozungumza , soma Yohana 1:1-3 na Ufunuo 19:13.  
na

Wakolosai 1:13-17 ''Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake; ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi; naye(YESU) ni mfano wa MUNGU asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote. Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake. Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye.   ''

Kumjua MUNGU hakika kunahitaji ufunuo kutoka kwake.
Kwa leo naishia hapo na natambua nimekupa mwanga kidogo ili ujue MUNGU wa kweli aliyeumba mbingu na dunia. Siku nyingine nitafafanua zaidi ili kukuongezea maarifa muhimu zaidi kwako yaani kumjua MUNGU pekee wa kweli ambaye amejifunu kwetu kupitia Neno lake Biblia takatifu.
 Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichako chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili.

Comments