Huu ndio muoenekano wa Hekalu la mfalme Suleman, Jerusalem kama ilivyotajwa kwenye Biblia


Lakini pamoja na Picha hizi pia nimekuwekea na Somo kama lilivyoandikwa na Charles Mwaisemba


MFULULIZO WA MASOMO YA MATUKIO YA MWISHO WA DUNIA

SOMO 3:DHIKI KUBWA (PART 4)

4) NJIA YA KUPATA WOKOVU WAKATI WA DHIKI KUU
Kwa wayahudi kwao Wokovu wao unapatikana kwa njia mbili maana Mungu alikuwa amekwishajifunga kwenye Neno lake Kuwa atawaokoa Biblia inasema katika WARUMI 11:25-31,
I. Ni kutokumsujudia mnyama au sanamu yake, na kutokupokea chapa ya '666' ambayo itawapelekea wakubali kuteswa hata ikibi kufa ndipo wataokolewa

II. Kukimbilia mahali maarufu palipowekwa na Mungu mwenyewe,Biblia ndio inapataja kama milimani lakini ndio hii sehemu inayojulikana kama PETRA katika Mlima ule wa Mizeituni,mahali pale ambapo Yesu alipaa kwenda mbinguni na ndipo atakaporudi mara ya pili,nao wote waliokimbilia milimani ndipo watakapomuombolezea Yeye waliyemchoma na waliomkataa Mwanzo 

ZEKARIA 12: 10-11 “Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; nao watamtazama yeye ambaye walimchoma; nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza.Siku hiyo kutakuwa na maombolezo makuu huko Yerusalemu……………………………”


Wakati kwa wanaisrael kwao Upo uwezekano wa kupata wokovu wakati huu wa Dhiki kubwa kwa njia hizo,Huku kwetu mataifa ambao kama hatukuweza kuutafuta Wokovu wa Kristo YESU leo,majira haya ya mataifa,Basi wakati wa Dhiki kubwa kwetu mataifa NEEMA au MLANGO WA WOKOVU UTAKUWA UMEFUNGWA, hatutaweza kuokolewa Tena kwa namna yoyote

Ndio maana kwako wewe ambaye umefuatilia historia hii na kusoma Ujumbe,Ni muhimu kuelewa saa ya Wokovu ni sasa,Ukisubiri Dhiki hiyo ije ndo uokoke utakuwa umechelewa,utatafuta mahali pa kuyasikia haya utayakosa,Utakuwa kwenye dhiki hiyo kwa muda wote miaka 7 bila kupata wokovu wowote

Ndugu yangu kwanini Mungu akupe kuyajua haya mambo mazito yatakayotokea siku za usoni za hivi karibuni?Hapendi ukutane na dhiki hii Kubwa ambayo haijapata kutokea Tangu ulimwengu upate kuwepo?

Kweli utaishia kuyasoma tu na kuyapuuza na kuendelea na maisha yako ya Dhambi huku ukijifariji kuwa eti nawe ni Mkristo wakati maisha yako ni machafu hayaendani Na Mungu?

Maisha unayoishi ni ya michanganyo,vuguvugu utaukumbuka ujumbe huu utakapoyaona haya niliyoyaeleza yakitokea mbele ya macho yako kama ukiachwa bila kunyakuliwa lakini utakuwa umechelewa!!!

Utaisikia ile taarifa katika Vyombo vya habari kuwa Israel wamefanya mkataba na umoja wa nchi za ulaya ndipo utakapogundua tayari umeshaachwa!!!

Na juhudi zakozote ulizokuwa unazionyesha mbele za watu kuwa wewe ni mtu mwema,unasali kila siku,unaenda kanisani kila siku lakini kumbe kuna mambo ya sirini unayoyafanya!!!Ooooooooooh itatisha kuanguka mikononi mwa MUNGU aliye hai

Kama unajijua bado hujaokoka,hakikisha unaokoka leo Kwa kutubu Dhambi zako kwa kumaanisha kuziacha,Na kama ulikoka ila umerudi Nyuma Ebu anza tena leo,muendee 

Mungu,atakusamehe lakini pia kama umeokoka lakini unaona kama umeanza kujisahau au kulegea katika wokovu,OoooH Ndugu yangu Inuka Tena,Muombe Mungu akupe Nguvu za kumalizia,Usichoke kutenda mema,Zimebaki siku chache Yesu aje kutunyakua tusiingie katika dhiki hiyo.

Kwa Ujumla Mungu amelileta Neno hili kwako Mwanzo huu wa mwaka 2016 maana hataki tundelee na maisha tuliyo nayo yaamkini nani hajuaye labda Mwaka huu unaweza usiishe Yesu akawa amerudi?JE UMEJIANDAAJE

Kwa mawasiliano Zaidi piga namba 0712-054498 au 0759-420202

stmwaisembac@gmail.com/charlesmwaisemba@engineer.com
Shujaa Charles Mwaisemba
Nimefundishwa na Bishop Zachary Kakobe

Comments