JE, UNAIJUA NJIA YA KWENDA KWENU?

Na mtumishi Peter Mabula.
BWANA YESU YESU atukzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno hai la MUNGU aliye hai.
Je, unaijua njia ya kwenda kwenu?
Ni kama Swali rahisi kwa sababu kila mwanadamu anajua nyumbani kwako hivyo haitamsumbua kukuambia kwamba anaijua  hiyo njia. Kwa sababu kila mwanadamu anajua njia ya kwao.
Hakuna Mtu Asiyejua Njia Ya Kwenda Kwao, leo mimi nazungumzia njia ya kwao kila mwanadamu baada ya kuondoka duniani.
Kuna njia ya mbinguni ambayo inaitwa njia nyembamba kwa sababu wanaoiona ni wachache.
 na kuna njia pana sana ila ya kwenda jehanamu na hiyo wanaoiona ni wengi sana.
Biblia inasema hivi;

''Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache-Mathayo 7:13-14'' 

Njia ya  kwenda mbinguni au jehanamu hutengenezwa na mwanadamu kipindi angali anaishi duniani.
Matendo ya kila mtu ndio yanayotengeneza njia yake ya kule atakakokwenda baada ya kuondoka duniani.

Je, unaijua njia ya kwenda kwenu?
Watu wengi wanajua Njia Ya Kwao Lakini Njia Ya Mbinguni Wengi Hawajui. 
Njia Ya Mbinguni Ni YESU KRISTO Pekee.
BWANA YESU mwenyewe anasema kwa kinywa chake kwamba;

''Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini MUNGU, niaminini na mimi. Nyumbani mwa BABA yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo. Nami niendako mwaijua njia. Tomaso akamwambia, BWANA, sisi hatujui uendako; nasi twaijuaje njia? YESU akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa BABA, ila kwa njia ya mimi. Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na BABA; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona.-Yohana 14:1-7''

Njia ya uzima ni YESU KRISTO.
Hatuipokei njia ya uzima kwa kuiangalia tu bali tunaipokea njia ya uzima wa milele kwa kuifuata njia hiyo.
Biblia inatufundisha namna ya kuifuata njia ya uzima ikisema kwamba;

''Kwa sababu, ukimkiri YESU kwa kinywa chako ya kuwa ni BWANA, na kuamini moyoni mwako ya kuwa MUNGU alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.-Warumi 10:9-10'' 

Baada ya kuifuata njia ya uzima, hutakiwi kuishia kuifuata tu bali unatakiwa uishi maisha matakatifu kama njia ya uzima inayotaka.
Biblia inakushauri hivi wewe uliyeamua kuifuata njia ya uzima wa milele na umeipokea haki ya uzima wa milele kwamba;

''Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu; bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu. Na ikiwa mnamwita BABA, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni. Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu; bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya KRISTO. Naye amejulikana kweli tangu zamani, kabla haijawekwa misingi ya dunia; lakini alifunuliwa mwisho wa zamani kwa ajili yenu; ambao kwa yeye mmekuwa wenye kumwamini MUNGU, aliyemfufua katika wafu akampa utukufu; hata imani yenu na tumaini lenu liwe kwa MUNGU. Mkiisha kujitakasa roho zenu kwa kuitii kweli, hata kuufikilia upendano wa ndugu usio na unafiki, basi jitahidini kupendana kwa moyo. Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la MUNGU lenye uzima, lidumulo hata milele. Maana, Mwili wote ni kama majani, Na fahari yake yote ni kama ua la majani. Majani hukauka na ua lake huanguka; Bali Neno la BWANA hudumu hata milele. Na neno hilo ni neno lile jema lililohubiriwa kwenu. ''1 Petro 1:14-25 '' 
 
Hayo ndio maisha ya waenda uzima wa milele.
Hayo ndio maisha ya watu walioiona njia ya uzima na kuipokea.
Ni Vizuri Kuijua Njia Ya Mbinguni Ili Usipotee Wakati Wa Kuondoka Kwako Duniani. 
Hakuna njia nyingine ya uzima wa milele ila hiyo moja ambayo ni YESU KRISTO.
BWANA YESU anatuthibitishia akisema; 

''Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani. Amin, amin, nawaambia, Saa inakuja, na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa MUNGU, na wale waisikiao watakuwa hai. Yohana 5:24-25 '' 

Je, unaijua njia ya kwenda kwenu?
Watu Wengi Wanajua Dini Ila Hawamjui MUNGU
Watu Wengi Wanajua Madhehebu Ila Hawamjui MUNGU.
MUNGU wa kweli yuko katika KRISTO YESU pekee maana KRISTO ndiye aliyemfunua MUNGU wa kweli kwetu.

''Hakuna mtu aliyemwona MUNGU wakati wo wote; MUNGU Mwana pekee aliye katika kifua cha BABA, huyu ndiye aliyemfunua-Yohana 1:18 

-Biblia inasema KRISTO ndiye aliyemfunua MUNGU kwetu.
-Tumemjua MUNGU wa kweli kupitia YESU KRISTO.
-Nje ya YESU hakuna MUNGU ila kuna miungu tu ambayo na yenyewe inasubiri jehanamu kama wanadamu wanaoitumainia.

Je, unaijua njia ya kwenda kwenu?
 Kama ukimpokea YESU KRISTO na kuanza kuishi maisha mataktifu katika yeye kama Biblia inavyoagiza, hakika wewe kwenu ni uzima wa milele.
Lakini kama utaendelea kukataa kuokoka huku ukiendelea na dhambi hakika njia ya kwenda kwenu baada ya wewe kufa itakuwa njia ya jehanamu.

 ''Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya MUNGU ni uzima wa milele katika KRISTO YESU BWANA  wetu.-Warumi 6:23'' 

MUNGU BABA hataki mwanadamu hata mmoja aende jehanamu ndio maana ameleta ukombozi kupitia Mwanaye wa pekee YESU KRISTO.
Na BWANA YESU katika kuhakikisha hakuna mwanadamu anaenda jehanamu ameleta Neno lake kupitia watumishi wake kama hivi leo hapa ili tu wanadamu waende uzima wa milele.
BWANA YESU ni njia pekee ya uzima wa milele.
BWANA YESU hatupeleki asikokujua bali anatupeleka anakokujua na yeye mwenyewe ametangulia huko kutuandalia makao ya uzima wa milele.
Naamini sana najua umeifahamu njia unayotakiwa wewe upite baada ya kuondoka kwako duniani.

'' Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.-1 Yohana 1:9''

Hakuna haja ya kuhangaika bali ni muhimu kumpokea BWANA YESU ili jina lako liandikwe kwenye kitabu cha uzima.
 Ukombozi upo  na Mkombozi yupo.
Na siku zote Ukombozi hutoka kwa Mkombozi.
Bila Mkombozi basi hakuna ukombozi.
Hakuna mkombozi mwingine ila YESU KRISTO.

Ukimkosa YESU maishani mwako hesabu ni hasara namba moja kwako.
Ukijitenga na BWANA YESU tambua kwamba huko ni kujitenga na uzima wa milele.
Kwanini njia yako isiwe njia ya uzima wa milele?
Ndugu, nakushauri kwamba hakikisha njia yako inakuwa ni YESU KRISTO huku ukitimiza utakatifu wote kama Biblia inavyofundisha.
 Ukifanya hivyo Utapata kibali mbele za MUNGU ni itakuwa  rahisi sana kupata pia kibali mbele za wanadamu.

Mathayo 7:13 '' Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo.''

 Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichako chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili

Comments