KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU~02

Na Mchungaji Gasper Madumla.


Bwana Yesu asifiwe…
Karibu tuendelee;
(B) Kipaji (Talent)
~Ni uwezo wa kiasili (wa kuzaliwa nao) wa kimwili wa kutenda jambo au kitu fulani pasipo kujifunza. (Natural ability or skill)
Mungu ametoa vipaji mbali mbali kwa watu wake. Mfano,wengine wamepewa wawe waimbaji,wengine mafundi,wengine wachoraji,wengine wacheza sarakasi N.K Mara nyingi vipaji hivi hutumika kama sehemu ya kujiingizia kipato kwa mwenye nacho.
Maana wapo watu ambao ni mafundi wazuri wa mambo mbali mbali mfano fundi radio,ambaye kwa kweli hajasomea ufundi radio bali amezaliwa na uwezo wa kukorokochoa radio yoyote na kisha kugundua tatizo pamoja na kupata uvumbuzi wake,kisha na kujipatia kipato chake kwa ufundi huo. Wengine utakuta ni wachoraji wazuri sana,uwezo wa kuchora pasipo kujifunza mahali popote pale ni kipaji,ambapo kipaji hiki kinatoa kipato.
 Ujuzi unatofautiana na kipaji,kwa maana ujuzi unaupata kwa sababu ya elimu fulani uliyoipata darasani wakati kipaji ni uwezo wa kuzaliwa nao wa kutenda jambo pasipo kujifunza darasani. ( Ingawa mtu anaweza akawa ni fundi radio kwa kusomea,ufundi huu ni ujuzi.)
Lakini kumbuka hili; Mwenye kipaji anaweza akaenda shule kwa madhumuni ya kukikuza kipaji chake. Na hapo,ndiposa kipaji kinakuwa kina mapana makubwa ya utendaji kazi.
Je kipaji kinahitajika katika kanisa la leo?
JIBU;
Kipaji kinahitajika sana katika kanisa la leo sababu watu hawa wenye vipaji wanaweza kutumika kama chachu ya kuwakusanya watu wengi sehemu moja,kisha baada ya hapo wakahubiriwa na muhubiri na hatimaye kuvuna roho za watu hao.
Mfano;Wenye vipaji vya uchezaji,wanaweza wakacheza mahali pa mkutano wa injili kabla ya muhubiri kupanda,gafla waweza kuona kundi kubwa la watu wakitekewa na machezo ya nyimbo za sifa kwa Bwana kupitia wale wenye vipaji vya kucheza,kisha katika hali hiyo hiyo ndiposa muhubiri aja kuzikomboa roho za watu wale waliokusanyika. Mfano huu mimi ninaufananisha na mvuvi aliyezitega nyavu zake baharini  kisha samaki kunaswa na zile nyavu zake.
Kumbuka;kipaji ni zawadi ya bure itolewayo na Bwana Mungu kwa watu bila kuzingatia itikadi za imani zao. Maana mtu anaweza akawa hata aamini kabisa!yaani mpagani lakini akawa bado ana kipaji kizuri tu cha kufanya jambo fulani,Tofauti na karama,maana karama  inamtaka mtu  aokoke kwanza.
C)Karama(Spiritual gift)
Ni utendaji kazi wa Roho mtakatifu ndani ya mwamini aliyeokoka.
Zifuatazo ni baadhi ya tofauti chache kati ya ujuzi,kipaji na karama;
(i)Ujuzi ni uwezo upatikanao darasani,kipaji ni uwezo wa kuzaliwa,karama ni uwezo wa Roho mtakatifu wa utendaji kazi baada ya kuokoka.
(ii)Ujuzi ni kwa kila atakayesomea,kipaji ni kwa kila mtu sawa sawa na alichopewa,karama ni watu wachache waliokoka kwanza na kudumu katika wokovu.
(iii) Ujuzi una gharama ya pesa katika upatikanaji wake,kipaji hakina gharama ya pesa maana mtu hawezi kununua kipaji kwa pesa,karama ina gharama ya kuyauza maisha yako kwa Bwana Yesu ili Yeye Bwana awe Bwana na mwokozi wa maisha yako.
(iv)Ujuzi ni jitiada za mtu mwenyewe,kipaji hutoka kwa Mungu,Karama utolewa na Roho mtakatifu kama apendavyo Yeye.
Kila  aliyeokoka ana karama yake,kwa sababu sote tu viungo vya Kristo “Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana.” 1 Wakorintho 12:7. Hivyo basi karama ;hutolewa na Roho mtakatifu kama apendavyo Yeye kwa wale watu wake wanaomcha.
Kumbuka;mtu wa mataifa asiyeamini hana karama,mpaka anapokuja kwa Bwana,akiokoka ndipo upewa karama moja wapo kwa kadri ya Roho mtakatifu apendavyo. Hata wewe mpendwa ipo karama yako ikiwa utakuwa ndani ya Yesu na Yesu awe ndani yako.
~Je mtu anaweza kuipata karama yake kwa kusomea darasani?
JIBU;
Karama haipatikani kwa kusomea darasani,kwa maana Yeye atoaye kila karama ni Roho mtakatifu.( 1 Wakorintho 12:8). Bali mwenye karama anaweza kwenda darasani kwa lengo la kuikuza karama yake kimaarifa ili atakapokua akiitumia aweze kuwa na wigo mkubwa wa matumizi ya karama hiyo.
Jambo hili leo limekuwa ni shida kubwa inayoisumbua kanisa la leo,maana wapo watu wanaohudumu kiroho huko makanisani kwa sababu walienda kusomea karama zao kisha baada ya mafunzo wengine wakajiita au kuitwa ni wachungaji,mashemasi,mitume,manabii N.K
pasipo Roho mtakatifu kuhusika kuwapa nyadhifa hizo. Mfano; Uchungaji hausomewi bali utolewa na Roho mtakatifu,kisha baada ya kupewa huduma hiyo mtu aweza kwenda shule kupata mwanga zaidi juu ya uchungaji alikadhalika na karama nyingine zozote zile.
 Hatuwezi kuwa wachungaji,mitume,walimu kwa vyeti tu kwa sababu kinachohudumu kanisani sio cheti bali kile kinachohudumu ni roho ikiongozwa na Roho mtakatifu. Kama ndio hivyo,basi ni dhahili kabisa Roho mtakatifu ndie agawaye karama tofauti tofauti kama apendavyo Yeye.
~ Je mtu mmoja anaweza akawa na karama zote?
JIBU;
Mtu mmoja hawezi kuwa na karama zote,bali hupewa karama fulani kwa kufaidiana na mwingine ( 1 Wakorintho 12:14-20).
~Je mtu mmoja aweza kuwa na ujuzi wa jambo fulani,kisha akawa na kipaji na papo hapo akawa na karama?
JIBU; Ndio,mtu aweza akawa na ujuzi wa jambo fulani,akawa na kipaji kisha akawa na karama. Mfano mtu kabla ya kuokoka alikuwa na kipaji cha uimbaji wa nyimbo za kidunia,
then alipookoka ule uimbaji wake wa awali ukabadilishwa kwa Roho mtakatifu~ kile kipaji cha uimbaji kikavuviwa na Roho mtakatifu akawa na karama ya uimbaji,kisha mtu huyo akaonelea si vyema kubakia na karama hiyo pasipo kuijua kiundani hapo akaenda chuo cha mziki kwa ajili aikuze zaidi karama yake kwa ujuzi huku Roho mtakatifu naye akahusika kuikuza karama hiyo. Kwa hiyo umeona,mtu huyo amekuwa na ujuzi,kipaji pia karama.
~Je karama inahitajika kwa kiwango gani katika kanisa la leo?
JIBU;Karama inahitajika sana kwa kiwango cha juu katika kanisa la leo. Maana karama ndio utendaji kazi wa Roho mtakatifu,hivyo inahitajika. Kumbuka;mambo ya kanisa ni mambo ya kiroho na mambo ya rohoni huongozwa na Roho.
Hivyo basi ujuzi,kipaji na karama kila kimoja kinatofautiana na mwenzake haswa katika utendaji wa kazi. Tofauti hizi ndizo haswa zinazohitajika katika kanisa la leo ili makusudi mwili wa Kristo ujengwe.
02.TOFAUTI KATI YA WITO NA KARAMA.
Ipo tofauti iliyopo kati ya wito na karama,ingawa mara nyingine wito wa mtu inawezekana ndio ikawa ni karama yake.
A) Wito.(calling)
(i)Wito ni sauti kamili ya Roho mtakatifu juu ya kazi maalumu iliyotengwa kwa ajili ya yule aitwae. Mfano tunaona akina Barnaba na Sauli; “Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia.”Matendo 13:2
(ii) Wito ni kazi maalumu ya kiroho,au ofisi maalumu ya kiroho itolewayo na Roho mtakatifu kwa Yeye apendaye kumpa. Mfano katika zile huduma tano (Waefeso 4:11) ni wito uliotolewa na Roho mtakatifu,biblia inasema “Naye alitoa…” maana yake “ aliwafanya kuwa~ kwa wito.”
Tofauti iliyopo ni hii; mtu anaweza akaitwa awe mchungaji lakini katika uchungaji akapewa karama ya miujiza. Ndio maana waweza kuona wapo watu walioitwa kuwa wachungaji lakini wamejawa na matendo ya miujiza.
Kumbuk;wito huu ni uchungaji,bali karama katika uchungaji wake ni matendo ya miujiza. Mfano mwingine;mtu aweza kuitwa katika ofisi ya ualimu,lakini akapewa karama ya matendo ya huruma.
Ndio maana unaona walimu wengine makanisani wamejawa na matendo ya huruma sana. Mfano tena,mtu anaweza akitwa katika ofisi ya unabii lakini katika unabii wake akapewa karama ya kunena kwa lugha mbali na wito wa unabii.
Na mtu mwingine akawa na wito wa uinjilisti lakini akapewa ziada ya karama ya neno la maharifa,hivyo katika wito wake wa uinjilisti akawa amejawa na neno la maharifa. N.K
ITAENDELEA…
~Kwa huduma ya maombezi,nipigie sasa +255 655 11 11 49.
Mchungaji Gasper Madumla.
Beroya bible fellowship church(Kimara,Dar,TZ)
UBARIKIWE.

Share this:

Comments