![]() |
Ufufuo na uzima Morogoro. |
Na:
DR. GODSON ISSA ZACHARIA (SNP)
Utangulizi
wa Somo: Imeandikwa katika Isaya 42:22….[Lakini watu hawa ni watu
walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika
magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana
asemaye, Rudisha.]
Imeandikwa katika Efeso 6:12 ..[Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama;
bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya
pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.]
Tunashindana na falme katika ulimwengu
wa roho, kuna wenye mamlaka wanaoshindana, wakuu wa giza, jeshi la mapepo
wabaya. Tunapopiga majeshi tunashindana na majeshi ya kuzimu.
Yapo majeshi ya aina tatu,
·
Majeshi
ya Mungu
·
Majeshi
ya wanadamu.
·
Majeshi
ya kuzimu
Sauti yako ya kusema kwa ukakamavu na
mamlaka inamaanisha kile unachoongea,ipo nguvu katika kukiri. Kila kitu
ufanyacho fanya kwa nguvu zako zote, si kwa ulegevu. Mmarekani akifanya jambo
anafanya kwa nguvu zake zote. Umepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nnge, ina
maana sumu ya nyoka iko kichwani na sumu ya nnge iko mkiani, hiyo mamlaka uliyo
nayo ina uwezo pande zote.
Mtu anaweza kuibiwa na kutekwa na
kufichwa shimoni(yaani wako msukuleni), kuna mashimo yanayoficha watu. Kuna
watu ambao ni wanadamu, lakini wameibiwa wako magerezani,wamefichwa na
aliyewaiba ni mkuu wa giza.
Imeandikwa katika 2Wakorin12:2 [Namjua mtu mmoja katika Kristo,
yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba
alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu
ya tatu.]
Mwanadumu
ni muunganiko kati ya mwili, nafsi na roho. Roho ya mtu ikitoka nafsi inapotea
pia. Mtu akifa maana yake ni ametengana na roho. Mtu anaweza kuibiwa akatolewa
ndani ya mwili wake, na kuwekewa roho nyingine. Mtu anapochukuliwa msukule
anaenda kutumikishwa, na yule mtu halisi anabakia na mateso,magonjwa, taabu
n.k.
Imeandikwa
katika Yohana 5:25…[Amin, amin, nawaambia, Saa
inakuja, na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wale
waisikiao watakuwa hai].
Imeandikwa
katika 1Samweli 30:1-19…[Ikawa, Daudi na watu wake
walipokuwa wamefika Siklagi siku ya tatu, hao Waamaleki walikuwa wameshambulia
Negebu, na Siklagi, nao wameupiga Siklagi, na kuuchoma moto; 2 nao wamewachukua
mateka wanawake waliokuwamo wakubwa kwa wadogo; hawakuwaua wo wote, ila
wakawachukua, wakaenda zao. 3 Basi Daudi na watu wake walipoufikilia mji,
tazama, ulikuwa umechomwa moto; na wake zao, na watoto wao, waume kwa wake,
wamechukuliwa mateka. 4 Ndipo Daudi na watu waliokuwa pamoja naye wakainua
sauti zao na kulia, hata walipokuwa hawana nguvu za kulia tena. 5 Na hao wake
wawili wa Daudi walikuwa wamechukuliwa mateka, Ahinoamu wa Yezreeli, na
Abigaili, aliyekuwa mkewe Nabali, wa Karmeli. 6 Naye Daudi akafadhaika sana;
kwa sababu watu walikuwa wakisema kwamba apigwe kwa mawe, kwa maana nafsi za
hao watu wote walisononeka, kila mtu kwa ajili ya wanawe na binti zake; lakini
Daudi alijitia nguvu katika Bwana, Mungu wake. 7 Kisha Daudi akamwambia
Abiathari, kuhani, mwana wa Ahimeleki, Tafadhali niletee hapa hiyo naivera.
Naye Abiathari akamletea Daudi naivera huko. 8 Daudi akauliza kwa Bwana,
akasema, Je! Nikiwafuata jeshi hili, nitawapata? Naye akamjibu, Fuata; kwa kuwa
hakika utawapata, nawe hukosi utawapokonya wote. 9 Basi Daudi akaenda, yeye na
wale watu mia sita waliokuwa pamoja naye, nao wakakifikilia kijito Besori,
ambapo wale walioachwa nyuma walikaa. 10 Lakini Daudi akakaza kufuata, yeye na
watu mia nne; kwa maana watu mia mbili walikaa nyuma, ambao walitaka kuzimia
hata hawakuweza kukivuka hicho kijito Besori. 11 Nao wakamkuta Mmisri mavueni,
wakamleta kwa Daudi, na kumpa chakula, naye akala; nao wakampa maji ya kunywa; 12
kisha wakampa kipande cha mkate wa tini, na vishada viwili vya zabibu; naye
akiisha kula roho yake ikamrudia; kwa maana alikuwa hakula chakula wala kunywa
maji, siku tatu mchana na usiku. 13 Ndipo Daudi akamwuliza, Wewe u mtu wa nani;
nawe umetoka wapi? Naye akasema, Mimi ni kijana wa Misri, mtumwa wa Mwamaleki
mmoja; bwana wangu aliniacha, kwa sababu tangu siku hizi tatu nalishikwa na
ugonjwa. 14 Sisi tulishambulia Negebu ya Wakerethi, na ya milki ya Yuda, na
Negebu ya Kalebu; na huo mji wa Siklagi tukauchoma moto. 15 Daudi akamwambia,
Je! Wewe utaniongoza chini hata nilifikilie jeshi hilo? Naye akasema, Uniapie
kwa Mungu, ya kwamba hutaniua, wala kunitia mikononi mwa huyo bwana wangu, nami
nitakuongoza chini hata kulifikilia jeshi hilo. 16 Na hapo alipokuwa
amewaongoza chini, tazama, hao walikuwa wametawanyika juu ya nchi yote, wakila
na kunywa, na kufanya karamu, kwa sababu ya hizo nyara kubwa walizochukua katika
nchi ya Wafilisti, na katika nchi ya Yuda. 17 Naye Daudi akawapiga tangu ukungu
wa jioni hata jioni ya siku ya pili; hakuna aliyeokoka, ila vijana mia nne
waliopanda ngamia na kukimbia. 18 Daudi akawapokonya wote waliokuwa
wamechukuliwa na Waamaleki; naye Daudi akawaokoa wakeze wawili. 19 Wala
hawakupotewa na kitu, mdogo wala mkubwa, wana wala binti, nyara wala cho chote
walichojitwalia hao; Daudi akavirudisha vyote.]
UKIRI
Leo tulazimishe kila kilichoibiwa katika maisha
yetu kirudi katika jina la Yesu. Tunageuza karamu zao za kufurahia mateso
yetu kuwa kilio katika jina la Yesu.Wote waliochukuliwa lazima warudishwe kwa
jina la Yesu. Amen
|
Comments