KWA IMANI YOTE YANAWEZEKANA.

Na Mtumishi Peter Mabula.
BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Kwa furaha sana nakukaribisha tujifunze neno la MUNGU.


2 Kor 5:7 ''Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona ''



Imani ni uhakika wa rohoni ambao hutimia katika KRISTO YESU.
Imani ina kazi nyingi sana. -Yote Yanawezekana Kwa Imani. 
-Kwa Imani Tutamuona BWANA YESU Akitenda Makuu.
 -Kwa Imani Injili Ya BWANA Itamfikia Kila Mtu. 
Kwa imani tulipokea ushindi na kwa imani tutapokea tena ushindi mkuu.

Waefeso 6:16 ''zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.''


 Ni Vizuri Kuamini Ahadi Za MUNGU, Tunaziamini Ahadi Hizo Kwa Imani.
Imani Ina Nguvu Sana.
-Imani Huvumilia Hadi Jambo Hilo Litakapotimia Kwa Kuonekana. 
Waebrania 11:1 ''Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.''

  Kuna vikwazo vingi ambayo vinaweza kusababisha imani ya mkristo isikue.
=Kutokusamehe kunaweza kuzuia imani ya Mkristo isikue.
=Kukosa maombi kunaweza kusababisha imani ya mkristo isikue.
=Dhambi inaweza kufuta kabisa kukua kwa imani.

Wapo ambao imani yao ilikuwa kwa sababu ya uaminifu wao kwa MUNGU pamoja na kumwamini MUNGU.
Ibrahimu Baada Ya Kuamini Ahadi Ya MUNGU, MUNGU Alimwambia Asiendelee Kuitwa Au Kujiita Abramu Bali Ibrahimu.

 Mwanzo 17:5 '' wala jina lako hutaitwa tena Abramu, lakini jina lako litakuwa Ibrahimu, kwani nimekuweka uwe baba wa mataifa mengi. ''

 Jina Ibrahimu Maana Yake Baba Wa Mataifa Mengi.
 Changamoto Kwa Ibrahimu Ilikuwa Kujiita au kuitwa Baba Wa Mataifa Wakati Hali Halisi Inaonyesha alianza kuitwa baba wa mataifa mengi  kipindi ambacho Hana Mtoto Kwenye Ndoa Yake. Hebu Jaribu Kupiga Picha Kwa Watu Waliomzoea, Ghafla Mtu Angemuita Abramu Naye Angempinga Na Kusema "mimi Sio Abramu Bali Ni Ibrahimu Yaani Baba Wa Mataifa Mengi". 
Hii Ni Imani Kubwa Sana Yaani Unajiita Baba Wa Mataifa Mengi Wakati huo Huna Mtoto Hata Mmoja. 
Huyu alikuwa na imani ya ajabu sana.

Ndugu Zangu Tuongeze Imani Na Tuenende Kwa Imani. 
Tusisitesite Wala Kuhofu Kuhusu Kupokea Ahadi Za MUNGU. Ukiamini Yote Yanawezekana kwa imani.

Marko 9:23 ''YESU akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye.''

Wewe Kama Unaumwa Omba Kwa Imani Na Kusema "Mimi Ni Mzima" Hata Kama Unaumwa Sana.
Wewe Mwanamke ambaye watu wanasema hutaolewa wewe sema ''Nitaolewa kwa jina la YESU KRISTO.''
 Wewe unayesoma sema ''Nitafaulu kwa jina la YESU KRISTO''
Hata kama uko katika magumu kiasi gani nakuomba kwa imani katika jina la YESU KRISTO sema'' Naenda kufanikiwa na kupona kwa jina la YESU KRISTO.''

 Mtu mmoja anayekutia Moyo katika wakati Mgumu ni muhimu zaidi kuliko kundi la Watu likushangilialo wakati wa mafanikio
Naomba pia ujue kwamba;  Huwa Kuna Mapito Na Majaribu wakati mwingine  Katika Safari Ya Wana Wa MUNGU Kuelekea Uzima Wa Milele.
 Duniani Hapa Hakuna Mtu Aliye Kisiwa Kiasi Kwamba Hahitaji Msaada Wa Mtu Mwingine. 
Hata Kama Wewe Ni Tajiri Kiasi Gani Lakini Siku Ukipata Malaria Utamhitaji Tu Daktari. 
Kila Mtu Ni Muhimu. 
Ni Muhimu Kusaidiana Na Kuombeana Sana Kama Kanisa La MUNGU. 
Usipokuwa Msaada Wewe Kwa Huyo Ndugu Anayepitia Kwenye Magumu Ipo Siku Na Wewe Utapatwa Na Hayo Hayo Na Msaada Utakosa. 
Kusaidia Wengine Ni Kupanda Mbegu Njema Ambapo Kwa Kumsaidia Mtu Mmoja Utakuwa Unafungua Mlango Wa Watu 7 Kukusaidia Wewe.
Hayo yote yatawezekana kwa imani tu.

1 Thesalonike 5:8 '' Lakini sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, hali tukijivika kifuani imani na upendo, na chapeo yetu iwe tumaini la wokovu.''

 Rahabu Alikuwa Kahaba Lakini Kutenda Mema Kwake Kwa Israeli Kulimfanya Apate Faida Kubwa Na Hata Mbinguni Utamkuta Maana Alifanyika Mteule. 
Kwa imani Rahabu alimwamini MUNGU aliye hai akaokoka.
Rahabau aliamini katika MUNGU wa Israeli na kufanikiwa kupona.
Imani ni muhimu sana.
Kwa imani yote yanawezekana.

Kwa namna yeyote usikate tamaa wakati mwingine ushindi unapatikana katika ukurasa wa mwisho

=Sara alipata mtoto wakati akiwa na miaka 90 na alikua amekoma kwa desturi za wanawake.
=Daniel mtu aliyekua anapendwa na BWANA maombi yake ya kufunga na kuomba hayakujibiwa mpaka siku ya mwisho.
=Lazaro aliyekufa hata siku ya nne baada ya kifo chake MUNGU alifanya muujiza.
Usikate tamaa hata katika lile jambo unaloona limekufa, MUNGU aliyemfufua Lazaro anaweza kulifufua tena siku ya leo,kama ni kuomba tunatakiwa tuombe mpaka mwisho.
Kwa imani utashinda kupitia maombi yako.

Mithali 3:5-6 ''Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.'' 

 Mwambie MUNGU bila wewe siwezi,nishike mkono BWANA maana peke yangu siwezi!
katika ndoa yangu siwezi peke yangu,usiniache BWANA uniongoze.Mshike mke/mme wangu,watoto wangu!Biashara,mashamba,ajira na masomo,niwezeshe BWANA;Nakutegemea wewe tu.


 Yakobo 2:26 ''Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa''

 Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichako chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili

Comments