MAARIFA YANAYOPATIKANA KWENYE BIBLIA, HAYAPATIKANI KWENYE VITABU VINGINE!.

Na Mwl Nickson Mabena

"Na roho ya BWANA atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha BWANA;" ISAYA 11:2
Bwana Yesu asifiwe Mtu wa Mungu popote ulipo, unayeendelea kufatilia Mfululizo wa masomo haya maalumu kwa ajili ya Kampeni ya Kumfilisi Shetani, huku tukiwa na jambo muhimu la NUNUA BIBLIA NA UISOME!,
Naamini tangu uanze kuyafatilia masomo haya, kuna kitu umejifunza, kama mimi ninavyoendelea kujifunza..
Tuje sasa kwenye Somo hili, ambalo litakuonyesha tofauti iliyopo, kati ya Biblia, na vitabu vingine,
Tofauti kati maarifa yapatikanayo ndani ya Biblia na vitu vingine,
Pengine umekua ukisoma sana Magazeti, Vitabu vya Hadithi, au vijalida mbalimbali, lakini huwezi kabisa kusoma Biblia,
Au inawezekana unaweza kuangalia Movies, siries, na tamthilia mbalimbali, lakini hata Biblia huna, au unayo lakini hauisomi kwa kudai kwamba huna Mda!.
Yawezekana unasoma/tazama hivyo kwa lengo la kujifunza, yaani kuna elimu flani unaipata kupitia hizo Bongo Movies,
Lakini nikwambie hivi, huko inawezekana unayatafuta maarifa flani, lakini, HUWEZI KUYAPATA MAARIFA KAMA MAARIFA YAPATIKANAYO NDANI YA BIBLIA,
Katika Isaya 11:2 (andiko la somo hili), huo ulikua unabii wa Yesu Kristo, ukianza kusoma mstari wa kwanza, utakubaliana na mimi nachokisema!
Biblia inasema, Ndani yake kuna roho kadhaa,
Ambazo ni
👉Roho ya hekima na ufahamu. 👉Roho ya shauri na uweza 👉Roho ya maarifa na ya kumcha BWANA.
Sasa nisikilize,
Yesu ni Neno (Yoh 1:1), kwa maana hiyo, Ukiwa unasoma Biblia, maana yake unamsoma Yesu Mwenyewe!.
Kwa hiyo, Kama hizo Roho zipo ndani ya Yesu, maana yake pia zipo ndani Neno, ambaye ndiye Yesu!.
Kwa hiyo, nina ujasiri wa Kusema kwamba, Kuna Hekima huwezi kuwa nayo isipokua Umeokoka, pia Unasoma Biblia!
Naweza nikasema, Kuna Ufahamu huwezi kuwa nao kama Hujampokea Yesu Kristo ndani yako!
Katika kuthibitisha hili, naweza nikakwambia, kuna Watu, Ukiwaona Unaweza kudhani Wasomi wa Chuo kikuu, Lakini kumbe hata Shule hawajaenda, ila wapo hivyo walivyo kwa sababu ya Yesu Kristo na Maarifa wanayoyapata kwa kusoma Biblia!
Pamoja na Usomi wako, inakubidi umtafute, akupe Hekima, na Ufahamu, kwa sababu Yesu amempa, lakini wewe na Usomi wako Umekosa!.
Naamini umekutana na watu kama hao,
👉 Roho ya Maarifa,
Somo langu, lipo hapo, kwenye Maarifa!.
Maarifa, ni Elimu au Ujuzi juu ya jambo flani!
Kuna Mtu akasema, Maarifa ni Elimu ya Ufalme wa Mungu, iliyowekwa kwenye Matendo,
na mimi nakubaliana na tafsiri hiyo.
Unaposoma Biblia, kuna Elimu ya Ufalme wa Mungu, inayoingia ndani yako, ambayo huwezi kuipata Popote, isipokuwa kwenye Biblia, na ukiiweka kwenye matendo Elimu hiyo hugeuka kuwa MAARIFA!
Maarifa hayo, huwezi kuyapata kwa kuangalia Movies za Wakina Lulu, na Wema,
Maarifa hayo, huwezi kuyapata kwa kusoma hadithi za Erick Shigongo, na wengineo,

Bongo fleva na Bongo Movies hazikufundishi kama unavyodhani, Bali zinakupotosha tu, ndio maana unawaiga jinsi wanavyovaa, na Kunyoa!.
Kwa sababu umewaona kwenye Video wakiwa wamevaa Vimini na Visuruali (kwa wadada), na wewe umewaiga, unavaa nguo za kulalia Mchana kweupe!,
Nunua Bilia na Uisome, upate Maarifa ya KiMungu!.
"Kila apendaye mafundisho hupenda maarifa;..." MITHALI 12:1
Ukipenda Mafundisho ya Neno la Mungu, unapenda Maarifa ya KiMungu, kwa Sababu, ndani ya Neno la Mungu kuna ROHO YA MAARIFA!.
Unanielewa!?,
Ninachokisisitiza hapa, ni wewe kuchukua hatua ya Kununua Biblia, na Kuisoma Biblia, kwa kufanya hivyo, Kuna Maarifa ambayo huwezi kuyapata Darasani, ila utayapata ndani ya Biblia!.
Kuna Madaktari na Maprofesa, pamoja na Usomi wao, bado ni Wazinzi, bado ni Walevi, bado ni wala rushwa tu,
Hii ni kwa sababu, Hawana Maarifa, yanayopatikana na Neno la Mungu!.
👉Ukiyataka Maarifa haya, ruhusu Biblia ikufundishe, sio wewe Uifundishe Biblia!.
Mwalimu Mkuu wa Biblia ni Roho Mtakatifu,
Nunua Biblia, soma Biblia, Tumfilisi Shetani 2016!.
Usiridhike na Maarifa uliyoyapata shuleni,
KUNA MAARIFA NDANI YA BIBLIA, AMBAYO HUWEZI KUYAPATA KWENYE VITABU VINGINE, NUNUA BIBLIA, SOMA BIBLIA UPATE MAARIFA TUMFILISI SHETANI 2016!.
MIMI NINAYO BIBLIA YANGU, NA NINAISOMA, WEWE JE!?
Naamini kuna kitu umejifunza ndani ya somo hili,
Ahsante kwa kunisikiliza!.
Bwana Akubariki sana!
By Mwalm Nick
0712265856
(WhatsApp#)

Comments