MAOMBI YA KUANGUSHA MIPANGO MIBAYA DHIDI YETU.

Na Mtumishi Peter Mabula

BWANA YESU asifiwe.
Kuna wakati mwingine wasiokutakia mema hujikusanya na kupanga mipango mibaya juu yako.
Mara nyingine wale unaowapa siri zako wanaweza kukugeuka na kuanza kusambaza siri zako kwa lengo la kukuharibia.
Maombi ya leo ni kuwaangusha wanaokusanyika kinyume chetu.
Kuharibu mipango yao mibaya juu yetu.

Kwa sababu damu ya YESU KRISTO ipo na jina la YESU KRISTO lipo basi leo ushindi mkuu upo kupitia maombi yetu ya kuangusha mipango mibaya juu yetu.


Isaya 54:15 '' Tazama, yamkini watakusanyana; lakini si kwa shauri langu. Watu wo wote watakaokusanyana juu yako wataanguka kwa ajili yako.''

-Leo kupitia maombi utakayoomba hakikisha unaangusha na kufuta mipango yote mibaya ya adui zako, Kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
-Pinga makusanyiko yote ya siri yaliyokusanyika dhidi yako, Kwa jina la YESU KRISTO aliye hai..
-Vunja vioo vyote vya kipepo, Kwa jina la YESU KRISTO aliye hai..
-Tumia zima moto ya kiroho ili kuzima kila moto wa shetani ulioinuka dhidi yako, Kwa jina la YESU KRISTO aliye hai..

-Hakikisha unafuta maneno yote mabaya yaliyotamkwa na vikundi vya watu juu yako, Kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
-Hakikisha uko kinyume na kila kusanyiko la kipepo dhidi yako, Kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
-Hakikisha kila wanaokusanyika kinyume chako ili wakuharibie kazini au kwenye ndoa kaa kinyume nao kwa jina la YESU KRISTO.
-Pambana kiroho kupitia maombi maana leo uko ushindi ndani ya jina la YESU KRISTO.
-Tiisha kila kusanyiko, wachafulie usemi ili wakosane wao kwa wao, Kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
-Kila jambo waliloadhimia na kukusudia ili likupate hakikisha kwa jina la YESU KRISTO unakaa na kupinga na kuharibu na kufuta kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.

Pambana mpendwa na hakikisha unashinda kupitia maombi ya imani kupitia jina kuu sana la YESU KRISTO.
Anza na kutubu dhambi zote na ukiziacha zote  maana maombi ya mtu asiye haki ni machukizo kwa MUNGU.

Mithali 15:29 ''BWANA yu mbali na wasio haki; Bali huisikia sala ya mwenye haki.''

 Maadui watakuogopa na kukimbia kama tu utakuwa muombaji na mtakatifu.
Leo omba kwa imani huku ukijitenga na uovu wote.
Jina la BWANA YESU lipo ili kuharibu kila kusanyiko lililo kinyume na wewe.
BWANA ameahidi kuangusha kila kusanyiko la waovu na maadui zao kama tu ukiomba kwa imani.

Maombi haya hapa chini ni ya kukuelekeza tu baadhi ya sehemu za kugusia katika maombi yako lakini wewe omba kulingana na hitaji lako na utapokea.
Maombi ya kuangusha mipango mibaya dhidi yako.

''ROHO wa MUNGU pokea sifa milele.
Ninakushukuru MUNGU BABA kwa ulinzi wako na uzima kwangu.
Siishi kwa akili zangu bali kwa neema yako.
Nakushukuru sana BWANA maana neno lako ni ndio na neno lako ni uzima wetu.
Biblia Katika Yeremia 1:12 inasema wewe MUNGU unaliangalia Neno lako ili upate kulitimiza.
Neno lako leo linasema;
''Tazama, yamkini watakusanyana; lakini si kwa shauri langu. Watu wo wote watakaokusanyana juu yako wataanguka kwa ajili yako.-Isaya 54:15''
 BWANA naomba Neno hilo litimie kwangu leo ili kila wanaopanga vikao kwa ajili yangu waaibike na kusambaratika kwa jina la YESU KRISTO.
Kila maadui zangu wanakusanyika usiku wa leo kupanga mipango na mikakati mibaya juu yangu, ninaharibu mipango yao kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila wafanya kazi wenzangu wasionitakia mema wanaopanga mabaya kwa ajili yangu, ninafuta mipango yao kwa jina la YESU KRISTO.
Kila kikundi kinachowaza mabaya juu ya ndoa yangu ninafuta mipango yao na maneno yao kwa jina la YESU KRISTO.
Maadui wote wa siri ninafunga vinywa vyao kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Vikao vya maadui dhidi ya mke/muwe/Mchumba ninafuta mipango hiyo ya kishetani kwa jina la YESU KRISTO.
Vikao vyote vyenye nia mbaya dhidi ya watoto wangu au uzao wangu, ninaharibu hila hizo kwa jina la YESU KRISTO.
Kila kusanyiko la kipepo leo linaanguka kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Asante BABA wa mbinguni maana umetenda na kunishindia.
Vikao vyote vya wabaya wangu vinmeanguka kwa jina la YESU KRISTO.
Asante BWANA maana malaika wako wameshambulia ngome zote za makusanyiko ya wabaya wangu.
Nina katika jina la YESU KRISTO nimeomba na kupokea.
 Amen Amen.

Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichako chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili.

Comments