MAOMBI YA KUHARIBU MITEGO YA MWINDAJI.

Na Mtumishi Peter Mabula.


BWANA YESU atukuzwe.
Jana jumapili nikiwa kanisani nilipata ufunuo ulioniamsha na kuanza kuombea ombi ambalo sikuwahi kuliwaza wala kulifikiria.
Sauti ilinijia ikisema ''Haribu mitego ya Mwindaji''
Ilikuwa ni kipindi muhubiri amemaliza kuhubiri na amelitaka kanisa zima tuombe maombi ya kumshukuru MUNGU, lakini wakati huo huo ndipo niliposikia sauti ikiniambia juu ya kuharibu mitego ya mwindaji.
Niliomba kwa juhudi hata kama maombi ya
Ufunuo kama huo, ROHO wa MUNGU hunipa kwa sababu ya kunisaidia jinsi ya kuomba, jinsi ya kuwaeleza wenzangu katika maombi ya mkesha  na jinsi nitakavyowaandikia rafiki zangu ili wafunguliwe pia na wao katika eneo hilo  la ufunuo.


Nilianza kuomba nikiharibu kila mtego ya mwindaji.
Baadae nilikutana na maandiko yanayoelezea mitego ya mwindaji ambayo inaweza ikategwa na kunasa watu.
Mitego ya mwindaji ni mitego ya shetani na mawakala zake ambayo inaweza kutegwa ili kunasa watu wa MUNGU.
Mitego hutegwa na kazi ya mitego ni kuwanasa waliotegwa.
Leo jiondoe katika kila mtego wa mwindaji, jiondoe kwa jina la YESU KRISTO.

Leo nataka tukaombe juu ya kuharibu mitego yote ya mwindaji.
Mimi sijui unawindwa na maadui zako katika eneo gani.
Mimi sijui shetani ametega mtego kwenye eneo gani la maisha yako.

Zaburi 91:3 '' Maana Yeye(BWANA) atakuokoa na mtego wa mwindaji, Na katika tauni iharibuyo.''

MUNGU atakuokoa na mitego yote ya wanaowinda maisha yako, ndoa yako, mwili wako, afya yako, masomo yako, biashara yako na kila kitu chako.
MUNGU atakuokoa na mitego yote ya mwindaji kwa maombi yako utakayoomba.

Damu ya YESU KRISTO ipo na jina la YESU KRISTO lipo ndio maana ushindi mkuu leo upo kwa maombi yako.

Hakikisha unaharibu kwa jina la YESU KRISTO kila mtego ambao adui ameuweka katika ndoa yako.
Kuna watu wamewekewa mitego katika uchumba wao, mtego huo ukiwanasa uchumba wao unaweza kuvunjika.
Kuna watu adui ameweka mitego katika ndoa yao, upendo wa kwanza unaondoka na kunaanza vita kila siku.
Ndugu usikubali mitego ya mwindaji ambaye ni shetani na malaika zake, usikubali ikakunasa ndio maana leo ROHO wa MUNGU ameleta ufunuo huu ili kuhakikisha unaharibu kila mtego wa mwindaji katika eneo lako.
Kama adui wameweka mtego katika masomo yako ili ufeli, hakikisha unaharibu mitego yote ya mwindaji na mwindaji mwenyewe.
Ita jina la YESU katika kila eneo lako.
Popote mwindaji anakufuatilia ili kukuharibia hakikisha unamharibu huyo mwindaji pamoja na mitego yake.
Pambana ndugu kwa jina la YESU KRISTO.
Omba maombi yako na MUNGU atakushindia.
Omba maombi ya vita.
Dumu katika utakatifu na maombi.
Omba maombi ya kufunga kama utasikia msukumo huo ndani yako, ila katika maombi yako hakikisha unaharibu kila mtego wa mwindaji katika maisha yako.
Hakikisha anayekuwinda aanze kuwindwa yeye kwa moto wa jina la YESU KRISTO.

Kataa kuwekewa mtego na adui. Vunja, haribu, angamiza na teketeza kwa jina la YESU KRISTO.

Maombi haya ni ya kuanzia tu kwa yule mtu ambaye ni muombaji mchanga ili yamsaidie katika kuombea hitaji lake katika eneo la maisha yake. maombi haya yawe chanzo cha kumsaidia mtu kuomba maombi ya muda mrefu.

Maombi ya kuharibu  mitego ya adui.

Ninakushukuru MUNGU BABA wa mbinguni kwa ulinzi na uzima wako kwangu.
BWANA niko mbele zako nikiomba unisamehe dhambi zangu zote.
Natubu kila uovu nilioutenda na kuanzia sasa BWANA nipe nguvu za kushinda kila vishawishi na kila dhambi.
Nisamehe MUNGU wangu na takasa kinywa changu.
Nakataa dhambi zote zinazosababishwa na kinywa changu na nisamehe kila dhambi inayosababishwa na mawazo yangu.
naomba unisamehe MUNGU wangu.
Neno lako linasema katika Matendo 3:19 kwamba '' Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake BWANA''
BABA wa mbinguni ninatubu na kurejea, nisamehe MUNGU wangu na kwa neema yako naomba Roho wako aingie ndani yangu kwa upya ili anisaidie kushinda ulimwengu.
Nakushukuru MUNGU wangu maana umenisamehe.
BABA wa mbinguni nakushukuru tena kwa ajili ya siku ya leo ya kuharibu kila mtego wa mwindaji maishani mwangu.
Kwa jina la YESU KRISTO ninaharibu kila mtego wa mwindaji katika maisha yangu.
Naharibu kila mtego wa mwindaji katika ndoa yangu, Naharibu kwa jina la YESU KRISTO.
popote pale mitego ya mwindaji imetegwa katika uchumba wangu, ninaiharibu mitego hiyo ya mwindaji, naiharibu kwa damu ya YESU KTISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mtego wa mwindaji katika masomo yangu nauharibu kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mtego wa mwindaji katika uchumi wangu nauharibu kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mtego wa mwindaji katika familia yangu nauharibu kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mtego wa mwindaji katika ukoo wangu nauharibu kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO nauharibu kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mtego wa mwindaji katika miradi yangu nauharibu kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mtedo wa mwindaji katika mali zangu nauharibu kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mtego wa mwindaji katika kazi yangu nauharibu kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mitego ya mwindaji na mwindaji mwenyewe naiharibu kwa damu ya YESU na kwa jina la YESU KRISTO.
kila mtego wa mwindaji kokote ulikowekwa katika maisha yangu nauchoma moto kwa damu ya YESU na kwa jina la YESU KRISTO.
Niko kinyume na kila mwindaji na mitego yake, ninaiharibu  mitego hiyo kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Asante sana BWANA maana kwako nimeshinda. Kuanzia leo mitego yote niliyotegewa imeharika na kuangamia kwa jina la YESU KRISTO.
Ushindi wangu ni leo na ushindi huo umepatikana kwa jina la YESU KRISTO.
Nakushukuru JEHOVAH MUNGU wa milele maana fadhili zako ni za milele. Asante BWANA kwa ushindi ulionipa leo dhidi ya mitego ya mwingaji.
Katika jina la YESU KRISTO nimeomba na kupokea.
Amena Amen.

Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichako chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili

Comments