MUNGU ANATAKA UTAKATIFU KWETU WANADAMU.

Na Mtumishi Peter Mabula.
BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU la uzima.
MUNGU Ni Mtakatifu Na Siku Zote Anatutaka Sisi Waaminio Tuwe Watakatifu.

1 Petro 1:15-16 '' bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.''

Kumbe Ni Muhimu Kuishi Maisha Ya Utakatifu. 
Kama Hujaupata Utakaso Hakikisha Unautafuta Kwa BWANA YESU Kwa Kutubu.
Utakaso ni ni hali ya kupata baraka za MUNGU ili kusafishwa dhambi.
Utakaso ni kutakaswa.
Maisha ya utakaso katika KRISTO ndio maisha matakatifu.
Maisha ya utakatifu ni maisha endelevu katika maisha ya mtu mwenye nia ya uzima wa milele.
Maisha ya utakatifu ni kama ngozi ya mwili  ambayo siku zote iko katika mwili.
MUNGU anataka tuwe watakatifu.
Hatutakiwi kujitenga na utakatifu bali utakatifu unatakiwa kuwa maisha yetu ya kudumu.

 Ili Tuende Uzimani Lazima Tuwe Watakatifu.

Waebrania 12:14 ''Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona BWANA asipokuwa nao;''

MUNGU siku zote yuko ndani ya Neno lake takatifu.
Na neno la MUNGU ni chakula cha uzima.
Neno la MUNGU  ni chakula cha kutupa afya ya kiroho.
Neno la MUNGU huagiza tuwe watakatifu.
Kama mtu analitii neno la MUNGU hakika mtu huyo atakuwa anaishi maisha mataktifu.

 Wateule wa MUNGU ni watakatifu daima.
 Wateule Ni Wale Waliowekwa Wakfu Kwa MUNGU Kupitia YESU KRISTO 

1 Thesalonike 4:3 '' Maana haya ndiyo mapenzi ya MUNGU, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati; ''

Kutakaswa kwetu ni lazima tuepukane na uasherati.
uasherati ni maagano na shetani, ni mapatano na shetani na MUNGU hataki tufanye mapatano au maagano yoyote na shetani.
Tumetakaswa na BWANA YESU na hivyo tunatakiwa kuishi siku zote katika utakatifu wa MUNGU.
Kama kweli tunampenda MUNGU kama vinywa vetu ambavyo hukiri kila mara kwamba tunampenda MUNGU basi hatutakiwi kujitenga na utakatifu wa MUNGU.
Kama mtu anadai anampenda MUNGU harafu haishi maisha matakatifu huyo hampendi MUNGU.
MUNGU anataka waaminio halisi wajitenge na dhambi na wajitenge na mabaya yote na wajitenge na shetani.

 2 Kor 6:17 '' Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema BWANA, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. ''

 Utakaso Ni Muhimu Na Huo Utakaso Unapatikana Kwa Njia Zifuatazo.

 1. Utakaso Hupatikana Kwa Imani Katika Neno La MUNGU

Yohana 17:17 ''Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli. ''

2. Utakaso Hupatikana Katika Damu Ya YESU KRISTO.

Waebrania 10:10 '' Katika mapenzi hayo mmepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa YESU KRISTO mara moja tu. ''

 3. Utakaso Hupatikana Katika Kazi Ya ROHO MTAKATIFU Maishani Mwetu

1 Petro 1:2 '' kama vile MUNGU BABA alivyotangulia kuwajua katika kutakaswa na ROHO, hata mkapata kutii na kununyiziwa damu ya YESU KRISTO. Neema na amani na ziongezwe kwenu. ''

4. Utakaso Hupatikana Mara Baada Ya Kumpokea YESU Kwa Sala Ya Toba

1 kor 6:10-11 '' wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi. Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana YESU KRISTO, na katika ROHO wa MUNGU wetu. ''

 5. Utakaso Ni Tukio Endelevu Katika Mkristo Mcha MUNGU

2 Kor 7:1 ''Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha MUNGU.''

Ni Muhimu Sana Kuishi Maisha Matakatifu Ndani Ya KRISTO. Usiishi Kwa Sababu Tu Unaishi, Bali Ishi Kwa Sababu YESU KRISTO Aliye BWANA Na MWOKOZI Anaishi Ndani Yako.

  1 Yohana 1:7 '' bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake YESU, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.''


 Utakatifu ni muhimu sana kuendelea katika maisha ya wateule wa KRISTO.
Utakatifu huanza na mtu kutubu kisha baada ya kutubu ndugu huyo anaanza kuishi maisha mataktifu.
Kuna watu huwa hawapendi sana kufundisha kutubu na utakatifu, mimi watu hawa huwaita vichwa ngumu.
Vichwangumu Huwa Hawapendi Kuelezwa Ukweli.
Vichwangumu Hawataki Kusikia Habari Za Kuwaelekeza Kutubu. Vichwangumu Hawauhitaji Wokovu. Mimi Nawaitwa Vichwangumu Maana Licha Ya Kuhubiriwa Kila Siku Lakini Kuchukua Hatua Kwao Limekuwa Jambo Ambalo Halipo, Wanaweza Wakaahidi Kwamba Mwakani Nitaokoka Lakini Hawajui Hata Huo Mwakani Kama Watakuwa Hai. 
 Kama una mawazo ya ukichwa ngumu nakuomba badilika na tubu maana kuna wengine hufa kabla majina yao hayajaandikwa katika kitabu cha uzima.
Kuna wakati  Vifo Hutokea Kwa Wengine Kama Taarifa Kwetu Tulio Hai Kwamba Tujiandae Maana Zamu Yetu I Karibu. 
Kuna Rafiki Yangu Mmoja Nilipishana Nae Nikiwa Nina Haraka Lakini Baada Tu Ya Kumpita Akaniita Na Kunisalimia Nikarudi Tukasalimiana Na Mimi Nikaondoka Kwenda Nyumbani Kumbe Ile Ndio Ilikuwa Mara Ya Mwisho Kuonana Nae Maana Baadae Usiku Akiwa Kwake Alisikia Kelele Nje, Alipotoka Akakuta Majambazi Yanaiba Kwenye Duka La Mpesa, Hakujua Kama Majambazi Yana Bunduki, Akapigwa Risasi Na Huo Ndio Ukawa Mwisho. Niliumia Sana Na Jambo Hilo Lilinitesa Sana Kwa Miezi Mingi. Ndugu Zangu, Wokovu Ni Sasa Tena Sasahivi. Kuokoka Ni Lazima Kama Unautaka Kweli Uzima Wa Milele.
Ni muhimu kuokoka na kuanza kuishi maisha matakatifu.
MUNGU siku zote humsamehe yule anayeamua kutubu toba ya kweli.

Zaburi 86:5 ''Kwa maana Wewe, BWANA, U mwema, Umekuwa tayari kusamehe, Na mwingi wa fadhili, Kwa watu wote wakuitao. ''
 Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichako chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili

Comments