MUNGU ANAWEZA KUKUTUMIA TENA(1)


WAAMUZI 16:28
"Samsoni akamwita BWANA, akasema, Ee Bwana MUNGU, unikumbukuke, nakuomba, ukanitie nguvu, nakuomba, mara hii tu, Ee Mungu, ili nipate kujilipiza kisasi juu ya Wafilisti kwa ajili ya macho yangu mawili". WAAMUZI 16:28
Bwana Yesu asifiwe, habari ya Uzima,
Karibu tujifunze, Somo hili ambalo nimesukumwa nikushirikishe siku ya Leo!.
Ujumbe huu ni Ujumbe wa Neema,
Na MwlNickson Mabena.
Ujumbe huu unamuhusu mtu ambaye,
1. Alikua anamtumikia Mungu, akaanguka kwenye dhambi, na hajarudi tena kwenye utumishi wake (ameacha wokovu)
2.Alikua anamtumikia Mungu, akaanguka kwenye Dhambi, akatubu, lakini hajarudi kwenye kiwango kile cha mwanzo cha huduma yake.
3.Mtu ambaye hajaokoka, lakini kutokana na Maovu anayoyatenda anadhani haiwezekani kuwa Mtumishi wa Mungu (, kwa jinskwalivyo halivyokani kua Mtakatifu).
anadhani
Kama wewe upo miongoni mwa watu hao watatu, basi ujumbe huu wa neema, unakuhusu, pia hata kama unaona haukuhusu moja kwa moja, basi unaweza kumsaidia Mwingine.

Kwa utangulizi wa Somo, nataka tuangalie Huduma ya Samsoni, ikiwa kama mfano wetu, kwenye somo hili.
Somsoni, alikua mnadhiri wa Bwana, alitengwa kwa Ajili ya kusudi la Bwana, la kuwaokoa Israeli na Mkono wa Wafilisti,
Kabla Samsoni hajazaliwa,
Mama yake aliambiwa hivi;

"Kwani tazama, utachukua mimba, nawe utazaa mtoto mwanamume; na wembe usipite juu ya kichwa chake; maana mtoto huyo atakuwa mnadhiri wa Mungu tangu tumboni; naye ataanza kuwaokoa Israeli na mikono ya Wafilisti". WAAMUZI 13:5
Samsoni, alikua na huduma kubwa sana, Mungu alikua anamtumia kwa viwango vya juu,
alikua ana upako wa Roho Mtakatifu usio wa Kawaida,
Kama angekua Muhubiri, ningesema alikua akisimama Madhabahuni, Miujiza isiyo ya kawaida ilikua inafanyika,
Kama angekua Muimbaji, ningesema kwamba, Akipanda Madhabahuni kuimba, hata kama hajui kucheza, alikua akiimba, watu wanajazwa Roho Mtakatifu, Mapepo yanakimbia yenyewe!.
Ningesema, ndani yake kulikua na furaha ya Wokovu, inayoletwa na Roho Mtakatifu, alikua ana ujasiri wa Kuwashuhudia Wengine habari za Yesu,
Au alikua anavaa Mavazi yenye utukufu Mbele za Mungu na wanadamu.

Pengine ningesema alikua anawahimiza wengine kuomba, au kuhudhuria Ibada kanisani.
Samsoni kwa uweza wa Nguvu za Roho Mtakatifu, alifanya Mambo ya Ajabu sana,
moja ya muujiza alioufanya Samsoni ni Huu..

👇👇👇👇
"Samsoni akaenda akakamata mbweha mia tatu; kisha akatwaa vienge vya moto akawafunga mbweha mkia kwa mkia, akatia kienge kati ya kila mikia miwili" Amuzi 15:4

Kukamata Mbweha 300, kwa akili ya kawaida haiwezekani, tena kuwafunga mikia wote 300 ni ngumu zaidi,
Kama wangekua kuku tena kuku wa kisasa, nijaribu kuelewa, lakini kwa Mbweha, ni ngumu, lakini Samsoni, kwa Upako wa Roho Mtakatifu aliweza!.

Pamoja, na Upako wote huo, Lakini Samsoni akaanguka Mikononi mwa Delila, akatenda Dhambi, Upako ukaondoka, Huduma ikafa, Maombi hamna tena, Kushuhudia hawezi tena, Mavazi yamebadilika, kunena kwa Lugha kumebaki kwa Mazoea tu, hamna Nguvu za Mungu ndani yake!.
Samsoni, akatobolewa Macho,
"Wafilisti wakamkamata, wakamng'oa macho; wakatelemka naye mpaka Gaza, wakamfunga kwa vifungo vya shaba; naye alikua akisaga ngano katika gereza." Amuzi 16:21
Hana tena maono ya kumtumikia Mungu, na Shetani anamchezea anavyotaka!.
Yawezekana unayesoma Ujumbe huu, yamekupata ya Samsoni, Huduma yako imekufa kwa Sababu ya Dhambi, Sasa hivi huwezi kuomba kama Zamani, Huna Hofu ya Mungu kama kwanza, Hata Ukitenda Dhambi unaona kawaida, huhukumiwi tena,
Furaha ya Wokovu imeondoka, kiwango cha Imani kimepungua,
Ukihubiri unaona sauti inakurudia ndani,
Umebaki na Shuhuda za Zamani tu, kwamba, zamani nilikua nahubiri sana, au nilikua naomba sana, lakini tangu, nilivyozini na yule Binti/Kijana, siwezi tena, hata faida ya Kwenda kanisani siioni!.
Nmeomba Msamaha kwa Mungu, lakini mbona hasemi na mimi kama zamani!?.
Nisikilize nikwambie, Mungu anaweza kukutumia Tena, na Anataka Akutumie tena,
Shetani anakudanganya, kwamba huwezi Kusimama tena, Lakini Mungu anataka akusimamishe tena!.
Yesu anataka akutumie tena, lakini kuna Hatua za Kuchukua,
Narudia kusema, Mungu anaweza kukusimamisha tena!.
Ni Maombi yangu kwa Mungu, Mungu akupe neema tena, wewe ambaye Mungu amesema nawe kupitia somo hili,
Na ninamwamini Mungu, kwamba atakupaka Mafuta tena!.
Mungu akubariki sana kwa Kuusoma Ujumbe huu!.
Ahsanteni kwa kinisikiliza.
.....Somo litaendelea......
By Mwalim Nick
0712265856
(WhatsApp#)

Comments