MUNGU ANAWEZA KUKUTUMIA TENA(2)

Na Mwl Nickson Mabena

"Samsoni akamwita BWANA, akasema, Ee Bwana MUNGU, unikumbuke, nakuomba, mara hii tu, Ee Mungu, ili nipate kujilipiza kisasi juu ya Wafilisti kwa ajili ya macho yangu mawili". WAAMUZI 16:28
Bwana Yesu asifiwe Mtu wa Mungu, karibu tena tuendelee kujifunza, ujumbe huu ni ujumbe wa Neema, Roho Mtakatifu amenipa kwa ajili ya Mtu aliyemkusudia,
Nimemwomba Mungu kwa ajili yako, utakaposoma ujumbe huu, ufahamu uingie ndani yako, na Roho Mtakatifu akusaidie kuchukua hatu!.

Kwenye Sehemu ya Kwanza ya Somo hili, nilieleza watu watatu waliokusudiwa kwenye ujumbe huu wa neema,
(Lipitie tena somo la kwanza, uwaone hao watu wa tatu)
Kwenye Mfano,
tuliangalia Huduma ya Samsoni, ambaye alikua ana upako wa Roho Mtakatifu, na nguvu za Mungu za Ajabu zilikua juu yake,
Lakini Baadaye alianguka dhambini, na huduma yake ikafa, Upako ukaondoka!.


Nikasema kuna watu walikua wanafanya huduma kubwa au ndogo, lakini Wakaanguka kwenye Dhambi, baada ya hayo Upako ukaondoka, hawawezi kufanya Huduma tena kama Mwanzo, hawana Ujasiri tena kama mwanzo, hawawezi kuhubidi kama mwanzo hawawezi kuomba kama Mwanzo..
Kama ni wewe, yamekukuta hayo, nikwambie Tu, Mungu anaweza kukutumia Tena.

Wengi wanapofanya Dhambi, Wanaomba rehema kwa Mungu, Mungu ni mwaminifu, anasamehe na Kusahau,
Lakini, wengi hawajui, kwa nini wanashindwa kuirudia hali ya kwanza!?. 

Nimewahi kusikia, Watu wanasema hakuna dhambi kubwa wala Ndogo, Dhambi ni Dhambi, hiyo ni Kweli, na mimi naikubali,
Lakini, kwa Upande mwingine kuna Dhambi kubwa na Ndogo,
Kuna Dhambi kubwa na ndogo kivipi!?,
Dhambi kubwa au ndogo inakuja kwenye GHARAMA YA TOBA INAYOIHITAJIKA, ILI KUREJESHA HALI YA KWANZA ILIYOHARIBIWA KUTOKANA NA DHAMBI HIYO!.
Najiskia leo kuzungumza sana kwenye hili,
Utakubaliana na mimi kwamba, huduma nyingi sana zimeanguka kwa sababu ya Dhambi ya Uzinzi/Uasherati.
Je! Kwa nini Mtu akisema uongo, au akitukana au akimchukia ndugu yake Anaweza akaendelea vizuri tu!?,
Uzinzi, na dhambi hizo zingine, zote Adhabu yake ni kwenye ziwa la Moto,
Lakini, hapa duniani gharama ya toba zipo tofauti, inategemea madhara gani yametokea baada ya dhambi hiyo!.
Ngoja nikupe mifano miwili hapa, ili unielewe zaidi.
Mfano wa Kwanza.
"Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake". MITHALI 6:32
Unapozini, nafsi yako inaharibika, sasa kama umeokoka, ukazini, cha kwanza Nguvu za Mungu zinaondoka, cha Pili nafsi yako inaharibika vibaya!.
Ndio maana utajiona Mtupu, pia Ujasiri wa kusimama mbele za Mungu unapotea. 

Kwa hiyo, Toba yake, ni Kubwa sana, maana unatakiwa utubu ili usamehewe na Mungu, pili Utubu ili Nguvu za Roho Mtakatifu zirejee, tatu Mazoezi ya kuijenga nafsi kurudi kwenye hali yake!.
Wengi huishia kwenye toba ya kwanza, ya kusamehewa dhambi, anashangaa haoni mabadiliko, anaamua kuacha Wokovu/huduma.
Ngoja nikupe mfano wa pili, alafu nimalizie sehemu hii ya pili,
Mfano wa Pili
"BWANA akamwambia Musa, Haya! Shuka; kwa maana watu wako uliowatoa katika nchi ya Misri wamejiharibu nafsi zao, wamepotoka upesi kuiacha ile njia niliyowaamuru, wamejifanyizia ndama ya kuyeyusha wakaiabudu na kuitolea dhabihu, wakasema, Hiyo ndio miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya Misri". KUTOKA 32:7-8

Wana wa Israeli walipotengeneza ndama na kuiabudu, WALIJIHARIBU NAFSI ZAO,
Kilichotokea, Nguvu za Mungu zikatoweka, Huduma Ikafa, Mungu akaghairi kwenda nao kwenye huduma,
Ingekua leo, ningesema wangeenda kuhubiri, wangehubiri kimazoea, lakini ukweli ni kwamba Roho Mtakatifu hayupo katika huduma yao!.

Mungu ni mwingi wa rehema, ulipotubu, alikusamehe,
Neno lake linasema,
"Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali aziungamaye na kuziacha atapata rehema." MITHALI 28:13

Kama umeziungama na kuziacha, Mungu amesamehe, lakini swali linakuja, Mbona hujarudi tena kwenye Huduma yako!??.
Mwingine, umeacha kabisaa na Kwenda kanisani, ukidhani Mungu hawezi kukutumia tena!.

Shida hapo, nafsi yako imeharibika, ulipoomba msamaha, ulisamehewa, lakini bado ulikua una kidonda kwenye nafsi,
Lakini, usiogope, Somo hili ni lako, Mungu anaweza kukutumia Tena!.
Sehemu ya tatu, nitakwambia cha kufanya, kama unatamani kurudi kwenye Wokovu, au kurudi kwenye huduma yako, au kuja kuokoka kwa mara ya kwanza.
MUNGU ANAWEZA KUKUTUMIA TENA!.
Mungu akubariki kwa kunisikiliza!.
....Somo litaendelea...
By Mwalm Nick
0712265856
(WhatsApp#)

Email: mabenanickson@gmail.com

Comments