MUNGU ANAWEZA KUKUTUMIA TENA!(3)

Na Mwl Nickson Mabena
"Samsoni akamwita BWANA, akasema, Ee Bwana MUNGU, unikumbuke, nakuomba, ukanitie nguvu, nakuomba, mara hii tu, Mungu, ili nipate kujilipizia kisasi juu ya Wafilisti kwa ajili ya macho yangu mawili." WAAMUZI 16:28
Karibu tuendee na Somo letu, ujumbe huu ni ujumbe wa neema, ambao unamtaka Mtu arejee kwenye nafasi yake ya kwanza ya Utumishi,
Namshukuru Mungu kwa ajili ya Shuhuda za watu, ambao wananieleza kiu waliyonayo ya kutaka kurejea kwenye Utumishi,
Hii ni sehemu ya tatu ya somo, nikushauri uitafute, sehemu ya kwanza na pili kama hukuzisoma!.
Nikukumbushe tu, tulianza na kumuangalia Samsoni na Huduma yake, Samsoni alikua na Nguvu za Mungu, alikua ana Upako wa Roho Mtakatifu,
Lakini akaja akaanguka kwenye Dhambi, Upako ukaondoka, Ujasiri ukapotea,
Neema ikaondoka.
Tunamuangalia mtu ambaye yupo kwenye mazingira kama hayo, yaani alikua Ameokoka, na anamtumikia Mungu, lakini akaanguka dhambini!
Pengine anahisi hawezi kutumiwa tena na Mungu!
Leo, nataka tuangalie, nini cha kufanya, baada ya kuanguka dhambini, na Kupoteza Huduma, au Furaha ya Wokovu!.
Kuna vitu nilikueleza kwenye sehemu iliyopita, ni muhimu sana kujua!.
Juu ya aina tofauti tofauti za toba, kutokana na madhara yanayotokea baada ya dhambi!
Ukisoma vizuri, hilo andiko letu la somo (Waamuzi 16:28),
Utaona Samsoni alikua Muomba Mungu, na Maombi hayo, aliyaomba Baada ya Kupoteza nguvu zake za Kwanza,
Alisema 'Ee Bwana MUNGU, unimumbuke, nakuomba, ukanitie nguvu,....'
Maneno hayo, unaweza ukasema alikua anataka arudishiwe nguvu za awali, kutoka na somo hili naweza nikasema, ALITAKA MUNGU AMTUMIE TENA!.
Nilikupa, Mifano miwili, ya Dhambi ambazo zinaweza kuharibu Nafsi yako, na Gharama yake ikawa kubwa sana kwako,
Nataka nikuonyeshe gharama walizoingia watumishi mbalimbali baada ya huduma zao kuanguka!.
GHARAMA ZA KURUDISHA HUDUMA/WOKOVU TENA BAADA YA KUANGUKA!
Kuna gharama za kuingia ili huduma au wokovu wako urudi kwenye kiwango kile cha Mwanzo.
Nataka tuanze kumwangalia Musa, kwenye Huduma yao alifanyaje!?.
KUMBUKUMBU LA TORATI 9:
16 Nikaangalia, na tazama, mlikua mmefanya dhambi juu ya BWANA, Mungu wenu; mmefanya ndama ya ng'ombe ya kusubu; mmekengeuka upesi katika njia aliyowaamuru BWANA.
17 Nikazishika zile mbao mbili, nikazitupa kutoka katika mikono yangu miwili, nikazivunja mbele ya macho ya yenu.
18 Nikaanguka nchi mbele za BWANA siku arobaini usiku na mchana, kama pale kwanza; sikula chakula wala kunywa maji; kwa sababu ya makosa yenu yote mliokosa, kwa kufanya yaliyo maovu machoni pa BWANA, kwa kumkasirisha.
Musa alienda mbele za Bwana, kwa maombi ya Siku arobaini, anarudi, anawakuta watu anaofanya nao huduma, wamejiharibu nafsi zao,
Huduma ilibidi iishie hapo, maana Mungu aliamua kusitisha huduma kwa kuwaangamiza,
Baada ya Dhambi, Mungu anajitoa kwenye Huduma yako, anakuacha peke yako,
Musa, ilibidi aingie gharama, ili kurejesha huduma yao kwenye hali yao ya kwanza,
Kama kuhubiri, kushuhudia, kusoma neno, kuimba waweze kufanya kama walivyokua wanaganya kabla ya Dhambi,
Musa, aliingia kufanya Maombi ya Toba, tena kwa kufunga, siku 40 zingine,
Angalia, Huduma badala ya kusonga mbele, inasimama siku 40, hadi Musa ashuke mlimani,
Angalia, badala ya kuombea familia, masomo, au huduma zingine, ikabidi aombe Toba, tu!.
Angalia, kuna watu walikufa baada ya dhambi ile!.
Angalia, Mungu aliwasamehe na kusahau tangu siku ya kwanza, siku 39 zilikua kwa ajili ya kurudisha uhusiano uliokuwepo kwanza, ili aendelee na upako uleule!.
Sasa nisikilize Mtu wa Mungu, unayetaka Huduma/Wokovu virudi kama zamani!
Mungu anaweza kukutumia tena, lakini inabidi uingie gharama,
Sasa sijui 'siku 40' zako ni ngapi,
Kama umeomba toba, Mungu amekusamehe, lakini kwa suala la kurudisha Upako wako, kuna cha ziada...
Mungu akusaidie, kuona, ujue gharama yako ipoje!
Nehemia aliposikia Ukuta wa Yerusalemu umebomolewa, aliingia gharama ya maombi ya toba (Nehemia 1:1-7),
Ndio akaenda kujenga tena, (Nehemia 2:17)
Mungu anaweza kukutumia tena, kubali kuingia gharama!.
Neema, ya Mungu bado ipo, Usikubali Kufia Jangwani, rejea kwa Bwana Yesu!.
Amenifurahisha sana Samsoni, hakukubali kufa jangwani, ikabidi aingie gharama, Pamoja na upako kuondoka kwa sababu ya Dhambi, akaomba Mungu amtumie tena!.
Biblia inasema, aliowaua siku ile ya Mwisho, walikua wengi kuliko aliowaua wakati wa Uhai wake!
Naweza nikasema, Mungu alimpa Upako Mkubwa, kuliko aliowahi kumpa kwanza,
Alimpa Ujasiri mwingi, kuliko aliokua nao hapo kabla!.
Ndugu yangu unayesoma Ujumbe huu, Mungu anaweza kukutumia tena, kabisa anaweza!.
Ungana nami, mwaka 2016 tumfirisi Shetani, usikubali kuendelea kua Mikononi mwake, eti kisa ulimkosea Mungu!.
MUNGU ANAWEZA KUKUTUMIA TENA, ANATAKA AKUTUMIA TENA, LIPIA GHARAMA!!!.
Mungu akubariki sana, kwa kua nami kwenye somo hili, tukutane kwenye Masomo Mengine tena!.
...MWISHO....
By Mwalm Nick
0712265856
(WhatsApp#)

Email: mabenanickson@gmail.com

Comments