NENDA NYUMBA YA MFINYANZI, UKASIKIE NENO LA MFINYANZI!

Na Mwl Nickson Mabena

"Neno hili ndilo lililomjia Yeremia, kutoka kwa BWANA, kusema, Ondoka, ukashuke mpaka nyumba ya mfinyanzi, na huko nitakusikizisha maneno yangu." YEREMIA 18:1-2
Bwana Yesu asifiwe, karibu tujifunze somo hili ambalo Roho Mtakatifu ametaka nililete kwako kwa wakati huu,
Nilikua niandike somo lingine, lakini nilipokua kwenye Maombi jioni hii, Roho Mtakatifu akanikumbusha niandike hili kwanza!.
Kwa hiyo namwamini Mungu, kwamba lipo kusudi kwa ajili ya Ujumbe huu!.
Nilikua natafakari, na Kujiuliza swali, kwa nini Mungu amwambie Yeremia, kwamba aondoke aende nyumba ya Mfinyanzi, ndipo akamsikilizishe Neno lake huko!?,
Kwa nini Mungu asiunganishe tu, hapohapo wakati anaongea naye, angempa na ujumbe aliotaka Yeremia ausikie!?.
Nikapata ufunuo, ambao nataka nikushirikishe na wewe,
👉Kuna Mambo mengine, Mungu hawezi kusema na wewe, hadi utakapokua sehemu sahihi, kwa wakati sahihi!.
Kwenye hilo, nataka nikuambie Umuhimu, wa wewe kwenda Kanisani!.
Watu wengi wanaona ni jambo la kawaida sana kwao kutokwenda kwenye nyumba ya mfinyanzi, Wakati huo huo, wanataka kumuona Mungu kwenye Maisha yao,
Sawa upo digitali, una simu, laptop, tv, n.k unaweza unaweza kufatilia ibada ukiwa nyumbani na kupata Mafundisho toka sehemu mbalimbali, lakini bado ipo haja kubwa ya wewe Kwenda Kwenye Nyumba ya Mfinyanzi!.
Kuna hasara ya wewe kutokwenda Kwenye nyumba ya Mfinyanzi, pale unapohitajika!.
Kanisa nimeliita nyumba ya Mfinyanzi kwa sababu,
Mungu ni Mfinyanzi wetu
"Lakini sasa, Ee BWANA, wewe u baba yetu; sisi tu udongo, nawe u mfinyanzi wetu; sisi sote tu kazi ya mikono yako." Isaya 64:8
Kama Mungu ni Mfinyanzi wetu, nyumba yake ni ipi!?,
Yesu anajibu, "Yesu akaingia ndani ya hekalu, akawafukuza wote waliokua wakiuza na kununua hekaluni, akazipindua meza za wabadili fedha, na viti vyao waliokuwa wakiuza njiwa; akawaambia, Imeandikwa, NYUMBA YANGU ITAITWA NYUMBA YA SALA; bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi." MATHAYO 21:12-13
Kutokana na Maandiko hayo, utakubaliana na mimi, kwamba Hekalu, ni Nyumba ya Mungu, na Mungu ni Mfinyanzi, kwa maana hiyo hekalu ni Nyumba ya Mfinyanzi!.
Ingawa lipo Hekalu la Roho, lisilojengwa kwa mikono ya binadamu, ambalo ni mwili wako,
"Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?" 1KORINTHO 3:16
Lakini kwenye somo langu, sizungumzii hekalu hilo!.
Nazungumzia, Sehemu tunayokusanyika kwa ajili ya Kumwabudu Mungu!.
Lipo, Neno kwa Ajili yako kwenye Nyumba ya Bwana, kupitia Watumishi wake!.
Kama Yeremia angesema ana wageni, hawezi kwenda Nyumba ya Mfinyanzi, Mungu asingeweza kusema naye tena,
Kama Yeremia angesema, amechoka, au hajafua nguo, inabidi afue jumapili ile, kwa sababu jumatatu, anaingia kazini, Pengine Mungu asingeweza kusema naye tena!.
Ipo Sauti ya Mungu kwa ajili yako kwenye nyumba ya Bwana, Usiache kwenda, tafuta sababu ya kwenda, sio Sababu ya kutokwenda,
Karibia Kwenye Nyumba ya Bwana ili usikie sauti ya Bwana!.
"Jitunze mguu wako uendapo nyumbani kwa Mungu; Maana ni heri kukaribia ili usikie, Kuliko kutoa kafara ya wapumbavu; Ambao hawajui kuwa wafanya mabaya." MHUBIRI 5:1

Yeremia alipoondoka, alipofika Kwenye Nyumba ya Mfinyanzi, Mungu alisema naye!.
"3 Ndipo nikashuka mpaka nyumba ya mfinyanzi, na , alikua akifanakifanyayake kwa magurumagurudumuama
4 Na chombo kile, alichokukuwa akikifinyanga, kilipoharibika mkononi mwake yule mfinyanzi, alikifinyanga tena kuwa chombo kingine, kama alivyoona vyema yile mfinyanzi kukifanya.

5 Ndipo neno la BWANA likanijia, kusema,". YEREMIA 18
Na wewe nenda kwenye nyimba ya mfinyanzi wiki hii, Bwana atasema na wewe kama alivyosema na Yeremia!.
Nikupe kazi Moja unayesoma Ujumbe huu, Kabla hujaenda kwenye nyumba ya Mfinyanzi jumapili hii, Mwambie Mungu, akaseme na Wewe, ukamsikie Mungu kwenye Mahubiri, na nyimbo!.
Usiende kama ulivyozoea, Utamshangaa sana Mungu jumapili hii, na nyingine!!.
ONDOKA, NENDA NYUMBA YA MFINYANZI, USIKAE NYUMBANI, TUMFILISI SHETANI 2016!
Mungu akubariki, nakutakia Ibada njema
MUHIMU: USISAHAU KWENDA NA BIBLIA YAKO

Ubarikiwe!.
By Mwalm Nick
0712265856
(WhatsApp#)

Comments