TUMFILISI SHETANI

Na Mwl Nickson Mabena

Tarehe Kumi mwezi huu, ilikua siku yangu ya kuzaliwa, katika siku hiyo nilizindia kampeni yangu ya Mwaka huu, inayoitwa TUMFILISI SHETANI, 

Sikua na mpango sana wa hili kwenye mitandaomitandaomii, lakini msisitkumsisitizo ulipokua Mkubwa zaidi ndani yangu, nikaona isiwe Shida, ngaja nilete tu huku!!
Ndani ya kampeni hii, kuna Mambo mengi sana ya kufanya, ili kutimiza Kauli Mbiu hiyo,
Lakini, naanza na Kitu kimoja, kilichomo ndani yake, nacho kinaitwa 
"NUNUA BIBLIA NA UISOME", 

Kuna mambo nitakua nayazungumzia, ili kuwahamasisha Watu, Wanunue Biblia, na Kuzisoma, wasisubiri tu Kusomewa na Wahubiri, bali wasome wenyewe!.

Ndani ya Biblia kuna vitu vya thamani, ambavyo huwezi kuvipata kama huna Biblia yako mwenyewe!.
Pengine unasema huna hela ya kununua Biblia, ndio maana huna Biblia, 

Lakini nikwambie hivi, Bei ya Biblia ni ndogo ukilinganisha na Thamani ya Vitu Vilivyomo ndani!.
Una Simu, Kitanda, Viatu, Shati, alafu unasema huna Hela ya Biblia!?, si kweli, ni UZEMBE TU, na Kupuuzia!.

Ngoja nikushuhudie, nilivyoinunua Biblia ninayoitumia,
Biblia yangu niliinunua tarehe 24/2/2012, baada ya Biblia yangu ya Kwanza kupotea, nikiwa kwenye Kambi la Pasaka Mkoani Mtwara,
Nakumbuka, nilikua na Tsh. 18,000/= kwenye M-Pesa, na nilikua naenda kwenye Semina ya Mwlm C.Mwakasege kwenye uwanja wa Biafra kinondoni (Dar),
Nilinunua Biblia Tsh. 15,000/=, iliyobaki nilitumia kwa nauli, chakula, na Sadaka, bila kujali kesho yake ningeendaje Semina.
Hadi leo ninayo Biblia yangu, nimeizoea, na ina masomo ndani yake kiasi kwamba, nikienda sehemu, nikaambiwa nihubiri, hata kama ni ghafla, sipati shida, ninajua nawezaje kupata somo kwa haraka!.

Nisinge nunua Biblia siku hiyo, kwa kisingizio cha kwamba sina hela, sijui ingekuaje!!.
MIMI NINAYO BIBLIA YANGU, WEWE UNASUBIRI NINI KUNUNUA!?,
NUNUA BIBLIA, SOMA BIBLIA 2016, TUMFILISI SHETANI!.
Ukipenda, ungana na mimi kwenye Kampeni hii, ili watumiaji wa Biblia tuongezeke!!
Na Mungu, atakubariki zaidi!.
By Mwalm Nick
0712265856
(WhatsApp#)

Email: mabenanickson@gmail.com

Comments