USIRUDI MISRI



HESABU 14:1-4
1 Mkutano wote wakapaza sauti zao wakalia; watu wakatoka machozi usiku ule.
2 Kisha wana wa Israeli wote wakamnung?unikia Musa na Haruni; mkutano wote wakawaambia, Ingekuwa heri kama tungalikufa katika nchi ya Misri, au, ingekuwa heri kama tungalikufa katika jangwa hili.
3 Mbona BWANA anatuleta mpaka nchi hii ili tuanguke kwa upanga? Wake zetu na watoto wetu watakuwa mateka; je! Si afadhali turudi Misri?
4 Wakaambiana, Na tumweke mtu mmoja awe akida, TUKARUDI MISRI (Capital letter msisitizo wangu ).

Hakuna kitu kigumu kama pale ambapo mtu unaamua kuokoka ukiamini YESU atakusaidia na kukutetea katika masuala flani lakini ukajikuta kumbe baada ya kuokoka umekuwa na changamoto mara mbili ya ulivyokuwa duniani/ kabla hujaokoka .

Kuna vitu vingi vinatokea katika maisha yetu kiasi kwamba unaweza kujiuliza ni kweli MUNGU yupo, ni kweli anasikia maombi ya watu wake, ni kweli anatamani tuwe na furaha?, mara nyingi tunapofika katika hatua kama hii ni dalili kwamba mioyo yetu inakuwa imechoka

Kuna wakati umeomba sana ukiamini kuwa maombi humshusha MUNGU ajibu kile utakacho lakini badala yake umeomba na kuomba, ukafunga na mifungo yote lakini still changamoto iko palepale

Wapo wanaokwambia endelea kumngoja BWANA, lakini pia hawakosekani wanaokwambia ni afadhari kabla hujaokoka mambo yako yalikuwa vizuri, sasa umekoka hakuna badiliko chanya kwako, YESU wako yu wapi.

Inawezekana moyoni mwako pia kuna sauti inapiga kelele kila wakati, kila mara, kila siku ikikwambia mbona hujibiwi, mbona hufanikiwi, mbona kuna giza tupu katika maisha yako, kadri unavyomtafuta MUNGU ndivyo mambo yako yanavyozidi kuwa magumu 

Naomba niseme nawe tuu kuwa “Usinyamazishwe kumwendea YESU kwani ndiye mwenye majibu yako”, Usifikilie kurudi Misri kwasababu ukijaribu tuu utatumikishwa mara nyingi zaidi ya mwanzo

Changamoto, shida na mahitaji uliyonayo yasikupigie kelele na kukufanya ukaona ni kama Wokovu hauna maana
Pamoja na kwamba hujajibiwa mahitaji yako, still MUNGU ni MUNGU tuu, still Wokovu ni wa muhimu na wa thamani
Usimwache YESU, Usichoke, Usikate tamaa, BWANA wa nyakati na majira atatokea na kukushangaza.

Usiitamani Misri kwasababu ya changamoto za jangwani, Kaanani yako I karibu na Bwana yupo pamoja nawe katikati ya hilo jangwa akihakikisha anakufikisha salama Kaanani

Cha muhimu ni lazima ufuate sheria na kanuni, ukimtii MUNGU kwa kila jambo hata katikati ya hiyo changamoto
Usirudi Misri

Ni maombi yangu kwamba BWANA akusaidie kusimama, kusonga mbele name kuvuka salama jangwa hilo
Barikiwa

★Cecy Charles ★

Comments