![]() |
Askofu Mkuu Kanisa la Anglikana Duniani Justin Welby |
Kanisa la
Kianglikana duniani limesisitiza kwamba ndoa ni kati ya mwanamume na
mwanamke na likasimamisha ushirika wa jimbo la Marekani lililotambua
ndoa za wapenzi wa jinsia moja.
Viongozi wa kanisa la Kianglikana duniani, waliokutana Canterbury, wamesema kanisa hilo lilikiuka Imani inayofuata na waumini wengi wa kanisa la Kianglikana kuhusu ndoa.
Marufuku hiyo ya muda ambayo imepewa jimbo hilo a Marekani inalenga kuzuia kugawanyika kabisa kwa kanisa hilo kutokana na tofauti kuhusu ndoa za wapenzi wa jinsia moja.
Ndoa hizo zimekuwa zikipingwa sana na majimbo ya kanisa hilo barani Afrika.
![]() |
Gene Robinson ndiye aliyekuwa askofu wa kwanza wa Kianglikana kutangaza hadharani kuwa mpenzi wa jinsia moja mwaka 2003 |
Askofu wa sasa wa jimbo hilo la Marekani Michael Curry amesema uamuzi huo "utasababisha uchungu mwingi".
Mzozo kuhusu ndoa za jinsia moja ulianza kutokota baada ya kutawazwa kwa Kasisi Gene Robinson, aliyekuwa ametangaza hadharani kuwa mpenzi wa jinsia moja, kuwa askofu wa dayosisi ya New Hampshire ya jimbo hilo la Marekani mwaka 2003. Hatua hiyo ilizua mgawanyiko mkubwa miongoni mwa viongozi na waumini wa kanisa hilo duniani.
Comments