WEWE NI WEWE?


 
Na Mchungaji MAXMILLIAN MACHUMU, UFUFUO NA UZIMA

Malaki 10:1 Imeandikwa:- 1 "Angalieni, namtuma mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia mbele yangu; naye Bwana mnayemtafuta atalijilia hekalu lake ghafula; naam, yule mjumbe wa agano mnayemfurahia, angalieni, anakuja, asema Bwana wa majeshi."
Malaki 4: 5 "Angalieni, nitawapelekea Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya Bwana, iliyo kuu na kuogofya. Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana."
Malaki anaelezea juu ya mjumbe wa pili Eliya. Unaweza kujiuliza Eliya alishaletwa na akafanya kazi yake na kupaa kwenda mbunguni."

Luka1: 11 "Akatokewa na malaika wa Bwana, amesimama upande wa kuume wa madhabahu ya kufukizia. Zakaria alipomwona alifadhaika, hofu ikamwingia. Lakini yule malaika akamwambia, Usiogope, Zakaria, maana dua yako imesikiwa, na mkeo Elisabeti atakuzalia mtoto mwanamume, na jina lake utamwita Yohana. Nawe utakuwa na furaha na shangwe, na watu wengi watakufurahia kuzaliwa kwake. Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za Bwana; hatakunywa divai wala kileo; naye atajazwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye. Na wengi katika Waisraeli atawarejeza kwa Bwana Mungu wao. Naye atatangulia mbele zake katika roho ya Eliya, na nguvu zake, ili kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto, na kuwatilia waasi akili za wenye haki, na kumwekea Bwana tayari watu waliotengenezwa."
Zakaria ameambiwa atamzaa mtoto na jina lake atamwita Yohana ambaye atakuwa na nguvu zile zile za Eliya na kazi yake itakuwa ni kugeuza mioyo ya watu imrudie Baba.
Hapa tunaona mtu mwingine aliye ndani ya mtu. Duniani kulikuwa na kazi ya kugeuza mioyo ya watu, watu walimtambua kwa kumwangalia tu mwilini kama Yohana lakini mbinguni walimtambua kama Eliya.

Mtu huyu alikwenda jangwani akawa anakula asali na nzige, vilevile kama Eliya alivyokuwa anaishi jangwani. Mtu huyu alikuwa ni mtu mzuri japo alikuwa anaishi ndani ya mwili wa mtu mwingine. Hii na kwamba hata mtu mbaya pia anaweza akaishi ndani ya mwili wa mtu na kufanya mambo mabaya.
Mathayo 17: 9 "Na walipokuwa wakishuka mlimani, Yesu aliwaagiza, akasema, Msimwambie mtu ye yote habari ya maono hayo, hata Mwana wa Adamu atakapofufuka katika wafu. Wanafunzi wake wakamwuliza, wakisema, Basi kwa nini waandishi hunena ya kwamba imempasa Eliya kuja kwanza? Naye akajibu, akawaambia, Kweli Eliya yuaja kwanza, naye atatengeneza yote, ila nawaambia, ya kwamba Eliya amekwisha kuja, wasimtambue, lakini wakamtenda yote waliyotaka. Vivyo hivyo Mwana wa Adamu naye yuaenda kuteswa kwao."
Wanafunzi wa Yesu walikuwa wameshasoma maandiko na wakatambua kuwa kabla yeye hajaja ilibidi aje Eliya kwanza halafu yeye ndio aje lakini Bwana Yesu aliwajibu vizuri kuwa Eliya alishakuja lakini wao hawakumtambua.
Kwa ufahamu huu kwenye maisha yetu ya kawaida mchawi anaweza kuja kwenye familia bila kumtambua. Unaweza kumwona mtu anafanya mambo ya ajabu anaongea maneno machafu na anatabia mbaya kumbe ndani yake sio yeye kuna mtu mwingine ndiye anayeyafanya hayo yote.

Tumeona Eliya alikuja akawa anafanya mambo makubwa kwa ujasiri kama alivyokuwa anafanya kwenye agano la kale. Tumeona alikuwa anafanya kazi yake ya kuigeuza mioyo ya watu imwendee Baba na baadaye akauwawa.
Mathayo 1: 23 Imeandikwa: "Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi."
Mathayo 2: 1 Imeandikwa: "Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema, Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia."
Tumeona amezaliwa mtu asilimia mia moja na Mungu asilimia mia moja, alikuwa anakula kama wanadamu na anatenda kama Mungu. Waliofahamu Yesu mtu ambaye ndani yake ni Mungu walikuwa ni mamajusi. Kibinadamu walifahamu huyu mtoto ni mtu lakini ndani kuna Roho ambayo ndiyo ya muhimu sana kuliko mwili wake ndio maana mamajusi walienda kumsujudia kama Mfalme.
Kwenye maisha yetu ya kawaida kuna watu ambao ndani yao kuna roho ambazo ni za kuzimu zimeingia ndani ya familia za watu na kuharibu maisha yao. Elimu hii ndiyo tunayoishughulikia sababu watu wengi wanaishi lakini ndani yao kuna roho ambazo zinawatesa na kupindisha kusudi la maisha yao lisitimie.
Tumeona Bwana Yesu alizaliwa duniani kwenye holi la Ng'ombe na akaishi na watu mpaka alipofika miaka 30 ndipo alipoanza kufanya kazi yake iliyomleta hapa duniani lakini watu alioishi nao hawakumtambua japo mamajusi ambao walikuwa ni wachawi walimtambua yeye ni nani na kumwelezea kama mfalme.
Hii inatufundisha kwamba wachawi wanatambua sana kwamba mtu anaweza akawa anaishi kumbe sio yeye, wanaweza kumchomoa mtu ndani na wakaingia ndani yake au kuweka roho ya kuzimu ndani yake na mtu huyo akawa anafanya mambo mabaya ya ajabu.

Mfano: kwenye ndoa unaweza ukawa unaishi na mke/mume akawa anafanya vitu ambavyo sio vya kindoa na wewe ukaamua kwenda kwa washauri nao wakakuambia unatakiwa uishi naye kwa akili, ukaamua kuishi naye kwa akili laki ni mambo yakawa bado magumu mkeo/mmeo haeleweki. Kwenye ulimwengu wa rohoni unatakiwa utambue kwanza mtu huyo ni yeye au sio yeye ili umshungulikie mkeo/mumeo ambaye anafanya mambo ya ajabu uondoe roho zote zilizoingia ndani yake na mtu aliyeingia ndani yake ili akukomeshe na umpate yeye wa asili.
Mungu anaishi kwenye ulimwengu wa Rohoni ambao ni halisi na sisi tunatakiwa tutambue sisi ni Roho ambazo zinakaa ndani ya nyumba ambazo zinaitwa mwili. kwenye hii dunia shetani ameamua kuhamia ndani ya mwili wa mwanadamu ili atende kazi zake sababu watu wengi wanayafukuza mapepo kwenye miili ya wanadamu, na kusahau kwamba sio mapepo tu yanayoweza kukaa ndani ya miili ya watu,bali hata wachawi pia wanaweza kukaa ndani ya wanadamu.
Kwenye mambo ya Rohoni, zipo ngazi za nguvu, na Roho wa Mungu nguvu ni namba moja, roho ya mwanadamu ni namba mbili na wa tatu ni Makerubi na maserafi. Ngazi ya mwisho kwa nguvu ni malaika akiwemo shetani na malaika zake.
Mungu akitaka kazi fulani ifanyike anatumia Binadamu na malaika, vilevile shetani naye akitaka kufanya kazi anatumia mapepo na wanadamu. shetani sasa hivi ametambua kwamba mapepo anayoyatuma kuharibu wanadamu yanapigwa kwa damu ya Yesu sasa hivi ameamua kutumia wanadamu wa kawaida ambao wanatembea.
Watu wengi hawafahamu Elimu hii na maombi yao yanakuwa ya kawaida sana wakidhani Mungu atatenda bila wao kupigana rohoni.
Dalili ya mtu ambaye sio wa kawaida.
1. Kusikia sauti isiyo ya kawaida ambayo inakuelekeza kufanya mambo fulani. sauti hiyo inakuwa inakuongoza kutenda matendo ambayo hata wewe mwenyewe hupendi kuyafanya lakini unajishangaa kwanini unayafanya. maana yake kuna mtu ndani ambaye anakulazimisha ufanye kama vile anavyotaka yeye. akili yako inakuambia jambo hili ni baya sio zuri lakini unashindwa kujizuia.
2. Mawazo ya kujiua au kufanya hatari mbalimbali. kama ulishawahi kuona mtu anataka kujiua fahamu kuwa kuna mtu ndani yake ambaye anataka kumuua ili aupoteze mwili wake na yeye aliyechukuliwa asirudi ndani ya mwili wake. unaweza kuona mtu anafuata hatari bila kuogopa kumbe mtu huyo anaongozwa na mtu mwingine aishiye ndani yake ili auwe mwili wake.
Watu wanaofanya mambo haya ya kuingia ndani ya watu wanamahesabu yao jinsi ya kuwateka watu wenye nyota nzuri. watu hawa huwa wanaanza urafiki na wazazi au ndugu ili waweze kuingia ndani ya watu ambao nyota zao zinang'aa sana, watumie akili zao, wafanye mambo ya kishetani bila watu kufahamu na kudhani ya kuwa ni mtu amebadilika kumbe ni wale waishio ndani wanosababisha. Ashukuriwe Mungu muumba mbingu na nchi ambaye ametufunulia Elimu hii na kutupa uwezo wa kutoka kwenye vifungo hivi kwa jina la Yesu.
3. Magonjwa yasiyoeleweka/ ya ajabu ajabu/ yasiyotibika. Unaweza kujiuliza kwanini mtoto amekua tumboni ametoka nje ya uzazi na wanasayansi wanakuwa na maelezo yao kumbe ni mtu ambaye ameingia kwenye ulimwengu wa rohoni na kufanya hayo yote.
Unaweza kukutana na mtu kwenye mahusiano ambaye ukimwelezea mambo ya kuoana anakuwa hakuelewi lakini kwenye mambo ya beach, kutoka out, anakuelewa vizuri sana, ukimweleza kuhusu mambo ya mahubiri, au Biblia inasemaje mtu huyo anakuwa hakuelewi na mara nyingi kwenye maombi anakuwa haombi hata kama unakwenda naye kanisani anakuwa haombi yeye anasubiria kusema amen. Mtu kama huyu ni mtu ambaye hana malengo na wewe bali anakutafuta ili aharibu maisha yako.
Watu wengi wameingia kwenye mahusiano na watu ambao wameharibu maisha yao bila wao kufahamu kumbe ni mfumo wa kishetani ambao umejengeka duniani ili kuharibu maisha yao na kusudi lao.
Namna ya kumkomesha mtu akiwa ndani ya mtu.
Usiamini kila Roho bali kila roho mzijaribu. Fanya maombi ukijua mtu ndani ya mtu ndiye anayekusumbua. Unatakiwa ufikie mahali usiamini kila roho unayokutana nayo bila kufanya maombi. Kama mtu hayumo ndani yake unamwita njoo na anakuja.
Uchawi umefika mahali ambapo unapambana na akili za kibinadamu unapambana na mazingira, hospitali, maombi unajua kabisa mtu anaweza kwenda kuomba. kinachowachanganya wachawi ni kutokujua maombi yanayokwenda kufanyika pale mtu anapokwenda kanisani

Comments