ANGAMIZA ROHO YA MAUTI KUPITIA KUJITIA KITANZI,KULA SUMU NA KUJITUPA NDANI YA KISIMA.

Na Mtumishi Geofrey Mwanza.

Bwana Yesu asifiwe?
Kila ninapotaka kufundisha ujumbe huu mtandaoni huwa najiwa na jambo kama mtu kunipigia simu ili nichanganyikiwe/kompyuta yangu inazima moto ili nisiweze kufichua siri hii.
Je, kwa ukoo wenu kushaatokea mauti ya aina hii?
Hii ni mojawapo ya njia angamivu sana kwa kuweza kuukabili na kuumaliza ukoo mzima.

Basi kama kwenu/ kwa jirani yenu kushatoke mauti ya aina hii na hiyo roho haikung'olewa kwa damu ya Yesu,ujue bado hiyo roho ya mauti bado iko hapo na kwaweza tokea mauti nyingine na nyingine hata nyingine mpaka Jina la Yesu litakapopandwa pale.
Roho hii haivunjwi/kung'olewa kwa kumwita mganga hapo kwenu kama mlivyofanya, ni lazima litumike Neno la Yehova Mungu kwani ule ni ufalme uliojengwa pale na ni lazima ubomolewe katika Jina la Yesu Kristo.

Yeremia 1:10 " Leo nimekupa mamlaka juu ya mamlaka na falme, uwe na mamlaka ya kung'oa na kubomoa,mamlaka ya kuharibu na kuangamiza, mamlaka ya kujenga na kupanda"
Roho kama hii haiendi mahali inabakia pale kwa lile boma mpaka iue mwingine maana kusudi lake pale ni kuumaliza ukoo mzima.
Damu ya Yesu ndiyo njia pekee ya kumaliza mambo haya kisha familia ile iokoke na kukaa katika maombi kwani roho ile ikiondolewa pale itaenda kuzimu/jangwani na baada ya muda fulani itarudi kuangalia kama bado wana familia ile wamesimama na Yesu au la.

Ikikupata hujasimama na Yesu ujue itakukamata mara una hasira ya mumeo hakulala nyumbani,mara watu wote wanakuchukia ,mara unaambiwa shamba lako sio lako huku unajawa na hasira na kutwaa kamba unajinyonga pia.Unampa shetani points tatu za away game.
Dada/ndugu hakikisha umeiangamiza roho hii kwa ukoo wenu kwani ni kama moto katika kichaka chenye nyasi kavu.
Mzee/mama ninasema wazi kabisa sijatumia tasfida ili uelewe na umjue Yesu Kristo kwani yeye ndiye njia ya uzima wa milele.
Tubu dhambi zako leo na umwendee Yesu maana kwake pekee kuna uzima.

Usidanganywe na mtu yeyote kuwa wokovu hauna maana,wokovu wa Yesu ni cheti chako cha kukuingiza mbinguni.
Hakikisha umeomba kwa njia iliyo sahihi kuing'oa roho hii kwa ukoo wenu.

Pia kuna waombaji wengine huenda kung'oa roho kama hizi kwa familia za watu na wengine zinawamaliza au kuwakausha nguvu za rohoni kwani ndani mioyoni mwao hawana Yesu ila midomoni wanaye Yesu.
Mweke Yesu moyoni sio mdomoni mpendwa nawe utashinda yote.
Kama hujaokoka kimbia uokoke sasa.

Comments