Bibi wa Mambo ya Uchawi atupwe nje


Snp Dr. Godson Issa Zacharia. UFUFUO NA UZIMA - MOROGORO
Utangulizi
Je Wachawi wapo? - kweli wapo na wanayatesa maisha yako!
Ukiyachunguza maandiko matakatifu kwenye kitabu Biblia , utaona neno;
Wachawi limeandikwa kwenye biblia mara 20
Mchawi limeandikwa ktk Biblia mara 8
Uchawi mara 14
Uganga mara 18,
Waganga 21
Hirizi mara 3
Pepo Mara 141

Tuangalie tafsiri kadha wa kadha za neno hili Uchawi yamkini utapata maarifa kisha tumpe kichapo mchawi na kuufyeka uchawi wake
Uchawi ni nguvu za giza zinazotumiwa na jamii nyingi duniani, kwa ajili ya mtu kuumiza wengine kimazingara, au kwa ajili ya kujilinda au kujifurahisha kwa kuwatesa watu wengine kwa kuwachukua msukule au kuwafanya waugue au wafe (Kamusi ya Wikipidia)
Lakini twende mbele kidogo kuhusu mambo ya uchawi, kumbuka somo letu linaitwa "Bibi wa mambo ya Uchawi"
Kwa mujibu wa - Al Azhari (mtunzi wa kamusi maarafu ya kiarabu iitwayo“LisanulArab”)
1. Uchawi ni kitendo cha kujikurubisha/kuhusiana/kushirikiana (closeness) na shetani na kwa msaada wake (shetani)”
2. Uchawi kulibadilisha jambo mbali na uhakika wake, nako nikuwadhihirishia watu jambo lisilo la kweli wakaliona kuwa ni la kweli.”

Kwa mujibu wa - Sheikh WahiydAbdulsalaam Bali - mtaalamu maarufu katika elimu ya majini na mashetani na uchawi
3. Uchawi ni makubaliano baina ya mchawi na Jinni, mchawi akishurutishwa kufanya mambo ya haramu au ya shirki (ushirikina), na baada yakufanya hayo, Jinni anashurutishwa kumsaidiana kumtii mchawi huyo kwa kila anachotaka."

Tupige hatua kidogo tuyasongeshe majeshi ya Bwana na leo lazima kieleweke kwa jina la Yesu
Na mchawi
ni mtu kabisa lakini mtu muovu anayetumika kufanya kazi za uovu za kuwatesa watu wengine (Yeremia 5:26-8):
Ni waovu, wanaotega mitego, watu wenye hira, hawatetei maslahi ya wengine (yatima, wajane)
Mara nyingi, wachawi wanaweza kuwasiliana na kushirikiana na roho kama mashetani, majini, vibwengo, vinyamkera n.k. Ezekiel 13:18-19

Mchawi : Witch (Exford Dictionary)
a person, now especially a woman, who confesses or is supposed to practice magic, especially black magic or the black art; sorceress.

Tafsiri
Mchawi ni mtu , sasa hasa mwanamke , ambaye anakiri au anakufanya mambo ya kichawi, hasa uchawi mweusi au sanaa nyeusi, ufundi wa kichawi.

Ndo maana imeandikwa KUTOKA 22:18 Usimwache mwanamke mchawi kuishi.
JEREMIAH 5:26-28
26 Maana katika watu wangu wameonekana watu waovu; huotea kama vile watu wategao mitego; hutega mtego, na kunasa watu.
27 Kama tundu lijaavyo ndege, kadhalika nyumba zao zimejaa hila; kwa hiyo wamekuwa wakuu, wamepata mali.
28 Wamewanda sana, wang'aa; naam, wamepita kiasi kwa matendo maovu; hawatetei madai ya yatima, ili wapate kufanikiwa; wala hawaamui haki ya mhitaji.

EZEKIEL 13:18-19
18 useme, Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao wanawake wale, washonao hirizi katika viungo vyote vya mikono, wawekao leso juu ya vichwa vya kila kimo, ili wawinde roho za watu; je! Mtaziwinda roho za watu wangu, na kuzihifadhi hai roho zenu wenyewe?
19 Nanyi mmeninajisi kati ya watu wangu, kwa ajili ya makonzi ya shayiri na vipande vya mkate, ili kuziua roho za watu ambao haiwapasi kufa, na kuzihifadhi hai roho za watu ambao haikuwapasa kuwa hai, kwa kuwaambia uongo watu wangu wasikilizao uongo

Mchawi na mganganga wa kienyeji ni jamii moja - kazi zao ni za aina moja
Bibi wa mambo ya uchawi
NAHUMU 3:4~6
4 Kwa sababu ya wingi wa ukahaba wa yule kahaba mzuri, yule bibi wa mambo ya uchawi, auzaye mataifa kwa ukahaba wake, na jamaa za watu kwa uchawi wake.
Agano la Mungu Nahumu 3:5-6
5 Tazama, mimi ni juu yako, asema Bwana wa majeshi; nami nitafunua marinda yako mbele ya uso wako; nami nitawaonyesha mataifa uchi wako, na falme aibu yako.
6 Nami nitatupa uchafu uchukizao juu yako, kukufanya uwe mchafu, nami nitakufanya kuwa kitu cha kutazamwa kwa dharau.

Kumbe Mchawi anaweza kukuuza
Mchawi anaweza kuliuza taifa au nchi au mataifa na jamaa za watu

Ufunuo 18:11-13
11 Nao wafanya biashara wa nchi walia na kumwombolezea, kwa sababu hapana mtu anunuaye bidhaa yao tena;
12 bidhaa ya dhahabu, na fedha, na kito chenye thamani, na lulu, na kitani nzuri, na nguo ya rangi ya zambarau, na hariri, na nguo nyekundu; na kila mti wa uudi, na kila chombo cha pembe, na kila chombo cha mti wa thamani nyingi, na cha shaba, na cha chuma, na cha marimari;
13 na mdalasini, na iliki, na uvumba, na marhamu, na ubani, na mvinyo, na mafuta ya mzeituni, na unga mzuri, na ngano, na ng'ombe, na kondoo, na farasi, na magari, na miili na roho za wanadamu.

Madhara ya Wachawi na nini agizo la Mungu kuhusu wachawi
Mungu hawapendi wachawi na uganga wao anaagiza waangamizwe kwakuwa kusudi kubwa la mchawi
Ni kuiba, kuchinja, kuangamiza, kuua
kuchukua mtu msukule, kupindisha maisha ya mtu,
Vifo vya dharula na kutatanisha
Kuzaa wanadamu (roho za watu na miili ya watu) - Ufunuo 18:11-13,
Adui wa haki ya mwanadamu
Kutia roho ya kuacha

MATENDO YA MITUME 13:6~11
6 Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa uongo, Myahudi jina lake BarYesu;
7 mtu huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio Paulo, mtu mwenye akili. Yeye liwali akawaita Barnaba na Sauli waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu.
8 Lakini Elima, yule mchawi (maana ndiyo tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka kumtia yule liwali moyo wa kuiacha ile imani.
9 Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia macho,
10 akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka?
11 Basi, angalia, mkono wa Bwana u juu yako, nawe utakuwa kipofu, usilione jua kwa muda. Mara kiwi kikamwangukia na giza, akazungukazunguka na kumtafuta mtu wa kumshika mkono na kumwongoza.

Agizo ya Mungu dhidi ya wachawi, waganga, wasihili, wasoma nyota na uchawi
KUTOKA 22:18
Usimwache mwanamke mchawi kuishi.

ISAYA 47:9
9 lakini mambo haya mawili yatakupata katika dakika moja siku moja, kufiwa na watoto, na ujane; yatakupata kiasi kitimilifu, uchawi wako ujapokuwa mwingi, na uganga wako mwingi mno.

MAMBO YA WALAWI 20:27
Tena mtu mume au mtu mke aliye na pepo, au aliye mchawi, hakika atauawa; watawapiga kwa mawe; damu yao itakuwa juu yao.

KUMBUKUMBU LA TORATI 18:11
wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.

KUMBUKUMBU LA TORATI 18:10~11
10 Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,
11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.

Jinsi ya Kuwashughulikia wachawi na shughuli zote za kichawi na KUPATA USHINDI KAMILI
1. Mpokee Yesu - Okoka
2. Pokea mamlaka ya wapiga wachawi na uwe huru maana Bwana wetu Yesu amewapa amri
3. Tunaposema tuwapige wachawi na waganga tuwaangamize - hivi vita si ya mwilini : “Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)”
2 Korinto 10:3-4

Comments