ILI KUJENGA NA KUPANDA-02

Na Frank P. Seth
"2 Jihadharini na mbwa, jihadharini na watendao mabaya, jihadharini na wajikatao. 3Maana sisi tu tohara, tumwabuduo Mungu kwa Roho, na kuona fahari juu ya Kristo Yesu, wala hatuutumainii mwili. 4Walakini mimi ningeweza kuutumainia mwili. Mtu ye yote akijiona kuwa anayo sababu ya kuutumainia mwili, mimi zaidi. 5Nalitahiriwa siku ya nane, ni mtu wa taifa la Israeli, wa kabila ya Benyamini, Mwebrania wa Waebrania, kwa habari ya kuishika torati, ni Farisayo, 6kwa habari ya juhudi, mwenye kuliudhi Kanisa, kwa habari ya haki ipatikanayo kwa sheria sikuwa na hatia. 7Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo. 8Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo; 9tena nionekane katika yeye, nisiwe na haki yangu mwenyewe ipatikanayo kwa sheria, bali ile ipatikanayo kwa imani iliyo katika Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu, kwa imani; 10ili nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake; 11ili nipate kwa njia yo yote kuifikia kiyama ya wafu" (Wafilipi 3:2-11).
Ukisoma mistari hii utaona ADHIMA (kusudio) ya mtu ALIYEAMUA kufanya mabadiliko katika MAISHA yake, huku akiwa na malengo maalumu.
Mara nyingi, watu wengi sana wanashindwa kubadili hali za MAISHA yao (zozote) kwa sababu: kwanza, hawana MALENGO; pili, hawana mpango wa KUACHA mambo yasiyofaa, na tatu, hawako tayari kuchagua WATU maalumu wa kushirikiana nao au wa kujitenga nao.
Ukimwangalia Paulo, japo anazungumza kwa habari ya UHUSIANO wake na Kristo, chukua kanuni ile ile katika mambo mengine yote, utagundua ni siri ya mafanikio ya kukuvusha KIWANGO kingine cha kimaisha.

Ili KUJENGA na KUPANDA, imekupasa KUBOMOA, KUHARIBU, KUNG'OA, KUANGAMIZA, maana yake, umekubali kupata HASARA ya mambo fulani ili kufikia MALENGO yako ya KIROHO au mambo mengine ya muhimu ya KIMAISHA.
Katika somo la kwanza kuna orodha ya mambo ya muhimu ya kufanya katika safari hii ya mabadiliko, mojawapo ni kuandika MALENGO yako na VIKWAZAO vya kufikilia hayo malengo.
Angalia, VIKWAZO vingi vinasababishwa na WEWE kwanza kabla ya kwenda kwa WATU wengine au IBILISI. Wewe ni ADUI wa maendeleo yako kuliko hata shetani kwa maana unaMAMLAKA na UTASHI wa kuchagua cha kufanya. UnaRUHUSA ya kutumia nguvu za MUNGU (silaha za Mungu) japo, imekupasa KUTII na KUOMBA kwa bidii bila kukata tamaa. Kwanini ushindwe?
Msisisitizo wa somo hili ni KUJIHADHARI na matendo mabaya (vikwazo vya maendeleo yako), kama ni uvivu, uzembe, kulala kupita kiasi, matumizi mabaya ya fedha, kushindwa kujiwekea akiba, ngono, ulevi, nk., bila kusahau "wajikatao" (watu wasio faa kwa maendeleo yako).

Kwenye Wafilipi 3:10 utaona IMANI imetajwa. Usidhani imani inatumika katika kukemea mapepo tu na kuponya wagonjwa; Hata kujikwamua KIMAISHA unahitahi imani (kumwamini Mungu) na kuchukua hatua nzito (calculated risk), hata kama huoni mbele. Mwamini Mungu, utashinda.
Frank P. Seth

Comments