JIFUNDISHE NA KUJUA "JINA" NI NINI?

Na Mtumishi Geoffrey Mwanza

Bwana Yesu apewe sifa?
Karibu tujifundishe Neno la Mungu.Leo nataka tujifundishe kuhusu Neno"Jina".
Neno Jina limetokana na Neno la Kigiriki "Sum" ambalo lamaanisha ukumbusho.Biblia yasema:

KUTOKA17:14 "Kisha Mungu akamwambia Musa, andika habari hii katika kitabu iwe ukumbusho kisha uihubiri masikioni mwa Yoshua kuwa nitafuta ukumbusho wa Amaleki kabisa husiwe tena chini ya mbingu"

Sababu za kumpa mtu jina hutofautiana kulingana na mambo fulani.Majina yawezakupeanwa kwa misingi fulani kama vile majira ya kuzaliwa, desturi,dini nk.

Mungu ndiye asili ya kukabidhi wanadamu majina alipomuumba Adamu na Hawa.Ni vizuri tuzingatie kusudi la Mungu tunapowapa watoto wetu majina maana tutakuwa twamtii Mungu.Nyakati zingine watoto walipewa majina hata kabla ya kuzaliwa kwao :mfano Yesu.

Hebu tuyaone baadhi ya majina ya kiyahudi na maana
yake kwani majina yanayo maana:

Amosi- Mwenye nguvu.
Adrea-Mwanamume
Ayubu-Mwenye kutubu

-Danieli-Mungu ni hakimu wangu
-Daudi-Apendwaye
-Delila-Anayejipendekeza

-Elisha -Mungu ni wokovu
-Eliya-Yehova ni Mungu
-Ezekieli-Mungu anatia nguvu

-Gabrieli-Mtu wa Mungu
-Hawa-Uhai
-Ibrahimu-Baba ya wengi
-Israeli-Mungu anapigana
-Nuhu-Likizo/mapumziko

-Martha-Malkia
-Musa-Anayevutwa juu.

Ubarikiwe tutaendelea siku nyingine na ukae kwa maombi.Kama hujaokoka okoka sasa kwani hapana muda mwingine wakati ni sasa hivi.
By Pastor Geoffrey Mwanza. 

Tupigie simu kwa ushauri zaidi:
THE GLOBAL EVANGELISM MINISTRIES
Geoffreymwanza@yahoo.com
+254724 656 653

Comments