Kanisa la EAGT Lamsimika Dr.Brown Mwakipesile,kuwa Askofu mkuu wa pili wa kanisa hilo,

Waziri Mkuu Majaliwa Kassimu Majaliwa akiteta jambo na Askofu Mkuu wa Kanisa la EAGT Brown Mwakapesile, wakati wa sherehe ya kumsimika Rasmi Askofu huyo.

Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania EAGT limemsimika Askofu mkuu wa pili tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo Dr.Brown Mwakipesile baada ya kuchaguliwa na mkutano mkuu wa Halmashauri kuu ya kanisa hilo,Askofu Mwakipesile anakua ni wa pili baada ya aliyekua muanzilishi wa kanisa hilo na askofu mkuu wa kwanza Dr.Moses Kulola kufariki dunia mwaka 2013.

Usimikwaji huo wa Askofu Mkuu Mwakipesile umefanyika February 7 mwaka huu 2016 na kuhudhuriwa na waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania,Mh.Kasim Majaliwa Majaliwa pamoja na Mmishenari wa muda mrefu zaidi ya miaka 50 hapa nchini Dr.Hegmire ambaye ndiye aliyeongoza shughuli ya kumsimika Askofu Dr.Brown Mwakipesile



Waziri mkuu Majaliwa Kassimu Majaliwa akifafanua jambo wakati alipokuwa akiwahutubia waumini wa kanisa la EAGT, alipokuwa mgeni Rasmi wakati wa kuapishwa kwa Askofu Mkuu wa Kanisa Hilo Brown Mwakipesile aliyeteuliwa mwishoni mwa mwakajana.

Mwenyekiti wa umoja wa makanisa ya Kipentekoste Nchini Askofu David Batenzi ambae pia alikuwa msimamizi wakati wa kuteuliwa kwa Askofu Mkuu wa Kanisa la EAGT, Brown Mwakaipesile mwishini mwa mwaka jana, akizungumza jambo wakati wa kusimikwa rasmi kwa Askofu huyo.

Waziri mkuu Majaliwa Kassimu Majaliwa akipokea Risala ya kanisa la EAGT toka kwa Katibu Mkuu wa kanisa hilo Dkt, Leonard Mwizarubi katika sherehe ya kumuapisha rasmi Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Brown Mwakipesile.

Kwaya mbalimbali zikitumbuza kwa nyimbo






















Comments