KAZI YA GONGO NA FIMBO KATIKA MAISHA YA MKRISTO

Na Mchungaji Dk Peter Mitimingi

Zaburi 23:4
4 Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.
Kazi ya Gongo Katika Maisha ya Mkristo.
1. Gongo ilikuwa ni zana ambayo wafugaji walikuwa wanaishika kwajili ya kuwalinda kondoo pindi adui akijitokeza kutaka kushambulia kondoo alikuwa anabamizwa kwa kutumia gongo.
2. Gongo la Mungu kwaajili ya Kumpondea adui yako anayekutafuta na kutaka kukuangamiza Bwana atatumia gongo lake kusambaratisha wale wote wasiokuwazia au kutakia mema.
"Gongo lako na fimbo yako vyanifariji."
Kumbukumbu la Torati 28:7
Bwana atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba.
Kazi ya Fimbo Katika Maisha ya MNkristo
1. Fimbo ilikuwa ni zana ambayo wafugaji waiitumia kwajili ya kurudisha kondoo kwenye mstari pale ambapo kondoo waliacha njia na kwenda vichakani.
2. Mungu hutumia fimbo yake kumchapia mkristo ambaye ameokolewa kwa damu ya thamani ya Kristo kisha anaiacha imani na kuyaendea mambo yasiyofaa.
3. Hapo Mungu hulazimika kutumia fimbo yake kuchape sehemu mbalimbali ya maisha yako ili uweze kushtuka na kurudi katika mstari.
Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.
Waebrania 12:6-8
6 Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, Naye humpiga kila mwana amkubaliye. 7 Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye?
8 Basi kama mkiwa hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali.



DONDOO KUTOKA KWA MWALIMU
KOFIA 10 ZA BWANA KWETU
2Samweli 22:2-5


2 akasema, Bwana ndiye jabali langu, na ngome yangu, na mwokozi wangu, naam, wangu; 3 Mungu wa mwamba wangu, nitamwamini yeye; Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, mnara wangu, na makimbilio yangu; Mwokozi wangu, waniokoa na jeuri. 4 Nitamwita Bwana astahiliye kusifiwa; Hivyo nitaokoka na adui zangu.
KOFIA 10 ZA BWANA KWETU
1. Bwana ndiye jabali letu
2. Bwana ni ngome yetu
3. Bwana ni mwokozi wetu
4. Bwana ni Mungu wetu
5. Bwana ni mwamba wetu.
6. Bwana ni Ngao yetu
7. Bwana ni pembe ya wokovu wetu,
8. Bwana ni mnara wetu,
9. Bwana ni makimbilio yetu
10. Bwana ni Mwokozi wetu kwa wenye jeuri.


 DONDOO KUTOKA KWA MWALIMU!
MATOKEO 6 YA KUMWITA MUNGU
Yeremia 33:3
3 "Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua."
1. Lazima kuwepo na Nguvu ya Kumwita Bwana.
2. Mungu akiitwa lazima Aitike.
3. Mungu Haitiki Mpaka Ameitwa.
4. Mungu Akiitika Atatuonyesha Mambo Makubwa.
5. Mungu Akiitika Atatuonyesha Mambo Magumu.
6. Mungu Akiitika Atatuonyesha Mambo Tusiyoyajua.

Comments