KUUTAZAMA MWILI WA MTU WA UKOO WENU ALIYEKUFA WAKATI WA MAZISHI

Na Mtumishi Geofry Mwanza.

Bwana Yesu asifiwe sana?
Mwaka jana nilipokuwa nikimwombea dada mmoja aliyekuwa amepagawa mapepo na ambayo yalijitambulisha kuwa yalikuwa ya makaburini na tayari yalikuwa yamewaua watu watano katika ukoo wa dada huyu nilitambua siri moja.
Nimekutana na dada mmoja leo mtandaoni ambaye amenifanya niyakumbuke hayo ya mwaka jana.
Mapepo ndani ya dada huyo wa mwaka jana nilipoyaamrisha kwa Jina la Yesu kufichua jinsi yalivyokuwa yakiwashika watu wa ukoo huu na kuwaua yalisema:
(Sauti ya pepo)
".....tayari tumewaua watu wazima watatu na watoto wawili katika boma hili.Tunawatumia hii roho ya mauti wakati wa mazishi ya mmoja akifa huku wakati wanatazama mwili wa marehemu tunachipuka na kukamata mwingine wa ukoo.Hatuwezi kumwua mwingine papo kwa hapo au karibuni kwani tutatambulika kwa haraka tukifanya hivyo.Hata ndio unaona tukiwaletea ndoto za huyu tuliyemwua ili ajipange kumfwata.

inaendelea (Tukishika mwingine tunajificha ndani yake hata miaka miwili au mitatu kisha huanza kumla polepole huku tukimtia magonjwa au ajali....." (imeishia hapo)
Ndugu kunayo makabila ambayo ni lazima yafanye tambiko fulani wakati wa mazishi.
Makabila mengine hupenda kufanya makumbusho ya mwanadamu wa ukoo huu aliyekufa.

Hii in hatari sana na inaweza pelekea mauti ya ukoo mzima.
Wengine utaona wakitumia bakora/upanga/kisu/mikuki/mishale nk na kuzunguka boma nzima wakikimbia huku wanakimbiza kitu kisichoonekana na ukiuliza wanakwambia kuwa walikuwa wakiondoa kifo kwa familia ile!
Kunao wengine ni lazima wafanye mapenzi ya kimwili na maiti.Hapa ujue utakuwa umejiunganisha na kaburi na mapepo ya makaburini.

Kama ni wakati wa kuutazama mwili kama umeifadhiwa vizuri mortuary ni vizuri kutuma mtu wa mbali kidogo na ukoo kwani mauti zingine huwa ni za kikafara ya ukoo na utapata boma zima limefungwa maana wenyeji wamekufa wote kwa kutokujua siri za rohoni.

Omba sana uyapate mafunuo mengi ya kiroho kwani hata watumishi wengi huduma zao zimekufa/kupungukiwa na nguvu za rohoni kwa ajili ya kupendapenda kuiendea miili mifu ya kiukoo na mtu hajakomaa sana kiroho.
Kama hujaokoka okoka sasa Bwana Yesu yu njiani.

MUNGU wa mbinguni akubariki sana.
Ni mimi ndugu yako Mtumishi Geofrey Mwanza.
Huduma ya "The Global Evangelism Ministries".
(Kenya).
0724 656 653
Geoffreymwanza@yahoo.com

Comments