LAANA YA FAMILIA

Na; MCH. KIONGOZI JOHN KILIMA,UFUFUO NA UZIMA
DUGA MWEMBENI - TANGA
Utangulizi.
Mungu huwa anatembea katikati ya watu, na anapotembelea kusanyiko huwa anaangalia aliyejiweka tayari ili ampatie kile alichomuandalia. Kanisa ni kusanyiko (eklezia), maana yake Mungu anataka kusikioa kutoka kwetu nasi tusikie kutoka kwake.
Leo tutajifunza kwa habari ya laana ya familia.
[1wafalme 18:41 Naye Eliya akamwambia Ahabu haya inuka ule unjwe kwni pana sauti ya mvua tele.]
Laana ni roho zinazotumwa kwa mtu ili aje aharibu kwa mikono yake mwenyewe. Maneno husemwa ili mtu huyu atakapofanya jambo akosee mwenyewe. Huwezi kuwa na matokeo chanya.
[1wafalme17:1 basi Elia mtishbi wa wageni wa Gileadi,akamwambia Ahabu kama Bwana MUNGU,wa Israeli aishivyo,ambae ninasimama mbele zake ,hakutakua na umande wala mvua miaka hii, ila kwa neon langu]
Ahabu alifanya mambo kijeuri hivyo Mungu naye akamtuma nabii jeuri Eliya ili atakaposema neno itakuwa sawasawa na vilevile alivyosema. Ahabu aliua watu wengi wa Mungu, ndipo Mungu alipomtuma Eliya nabii akajionyeshe kwa Ahabu baada ya njaa nzito.


[1wafalme18:1-Ikawa baada ya siku nyingi ,neno la Bwana likamjia Eliya,katika mwaka wa tatu kusema Enenda ukajioneshe kwa Ahabu nami nitaleta mvua juu ya nchi ]
Unaweza ukasema jambo na likatokea, Eliya alisema hakutakuwa na mvua kwa muda wa miaka mitatu na nusu. Mengi alitenda Ahabu kwa sababu ya mwanamke aliyekuwa naye aitwaye Yezebeli.
Ukiona mwanaume yupo vizuri ujue nyuma yake yupo mwanamke imara nyuma yake na ukiona mwanaume haeleweki yupo kama amechanganyikiwa ujue mwanamke hayupo vizuri. Yezebeli mkewe Ahabu alikuwa akimshauri mumewe kuwauwa watu wa Mungu.
Obadia aliishi kwenye nyumba ya Ahabu lakini yeye alimuabudu Mungu kwa kumaanisha kabisa ingawa alifanya kazi na waabudu sanamu. Alikuwa akificha manabii kwenye mapango ili wasiuliwe na Ahabu.
Eliya alitamka hakutakuwa na mvua na ikawa, hiyo ni laana. Ahabu na Yezebeli waliuwa makuhani wa Bwana walikuiwa wakizuiwa kazi ya Mungu isiendelee. Mungu akachukizwa nao akamtuma Eliya ndipo Eliya akafunga mvua. Ahabu alilaaniwa na Eliya ili kusiwe na mvua na ikawa kwa sababu ya mabaya aliyoyafanya mbele ya Mungu kwani alimjengea Baali madhabahu na kumuabudu badala ya kumuabudu MUNGU Jehova.
Unapoinuka ili kuwatesa watu wa Mungu, Mungu husimama na kupigana mwenyewe 2 samuel 1:1- Mungu alikuwa na vita na Amaleki kizazi hata kizazi. Waamaleki walikuwa wanawazui wana wa Israeli kwenda wnakotakiwa kwenda.
Kutoka 17:10-16
Unapoomba vita huwa inapiganwa, kadri unavyopigana ndivyo unavyotengeneza uwezekano wa kushinda. Unapoinua mikono kumuabudu Bwana vita huwa ikipiganwa ukichoka ukashusha mikono malaika waliotumwa kwenye vita hushindwa. Musa alipokuwa akiinua mikono walishinda vita aliposhusha walipigwa. Unapomzuzia mtu kwenda mahali anapotakiwa kwenda, kufa imempasa yule azuiae.Inakubidi kutamka jambo juu ya wale wanaokuzuia kusonga mbele, yeye ameapa kuwa na vita kizazi hata kizazi na adui hivyo yeyote atakayeinuka juu yako unapoomba Mungu ataendeleza kuwa na vita juu ya Amalaki wa maisha yako. Amaleki ni roho humpata yeyote ili kuzuiwa watu wasisonge mbele. Hivyo lazima ashughulikiwe. Mungu alimuinua Sauli awe Mfalme ili awaangamize Waamaleki wote, alichokosea ni kubakiza baadhi ya mali ya watu wa Amaleki kwenye ufalme wake ndio ufalme wake uliporaruliwa.
Ukitaka Mungu ashuke kama alivyo au awe mtu wa vita ni pale anapoona yule aliyemtuma anazuiwa njiani. Unapokuwa mzuiaji Mungu hutengeneza jambo ambalo ukilifanya utaangukia hapo, huandaa mazingira. Ahabu ailtangaza kuwa Ramoth-giliadi kuwa ni yake hivyo akaandaa namna ya kuitwaa iwe yake Mungu naye akaruhusu mashetani wa uongo waingie vinywani wa manabii wake ili wamtabirie uongo ili atakapoenda kupiigana vita akapigwe huko. Mungu ameapa kuwa na vita na wale wanaomzuia yule aliyemtuma kwa kazi yake.
Kuzuiwa si lazima uone kwa macho ila ni vile hali ngumu ya maisha inakubana kiasi kwamba huwezi kufanya lolote ili uendelee.
Kuna laana zinatumwa kwenye maisha ya mtu lakini unapaswa kujua uzima na mauti vipo kwenye uweza wa ulimi wako.
Mithali18:21….mauti na uzima vipo katika uweza wa ulimi nao waupendao watakula matunda yake.
Wewe ndio wa kuamua ufanye nini kwani mauti au uzima viko kwenye uweza wa ulimi wake
Mithali14:1 ….mwanmke mwenye hekima huijenga nyumba yake na mwanamke mpumbavu hubomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe.


Laana inakufanya uharibu mambo kwa mikono yako mwenyewe. Laana ni roho mtu anawekewa ili aharibu mwenyewe. Mashetani husimamia laana hizo zitimie kwenye maisha ya mtu kizazi hata kizazi kama asipopatikana wakuzivunja.
Utamkuta mtu anasema “nitakufa mimi”, ni kwasababu zipo roho zinakusema kutamka kinyume na maisha yako.
Ni vema kuwa makini na maneno ya mtu, namna anavyosema nawe. Angalia Yesu alivyozungumza na shetani jangwani hata akamshinda. Luka4:1-11
Laana huweza kuvunjika. Ipo mamlaka ya kuvunja laana hizo, unapokuwa una laana ni rahisi kupigwa na laana. Utapigwa na magonjwa, mikosi balaa, umasikini. Zipo madhabahu ambazo huwa zinatuma roho za kulaani
Hesabu22:10-12
Mtu anaweza kubariki au kulaani kupitia madhabahu. Zipo Baraka zilizotokea kwenye madhabahu za kichawi. Baalam alikuwa na madhabahu ya kichawi ya kulaani na kubariki akataka awalaani Waisraeli.
Kimsingi kitu kilichobarikiwa na mungu mtu hawezi kukilaani Baalam alipotaka kuwalaan wanaisrael MUNGU akamwabia niliowabariki mimi hakuna anaeweza kuwalaan(HES 22:12)
MAOMBI:
Unaweza kuomba hivi ili kuvunja laana yoyote kwenye maisha yako.


Katika Jina la Yesu ninavunja laana zote zilizotumwa kwenye maisha yangu, kila mashetanani kutoka madhabahu za kichawi waliotumwa kusimamia laana ninawateketeza wote kwa damu ya Yesu, imeandikwa huwezi kulaani kiolichobarikiwa ninawaangamiza mashetani wote waliogeuka kuwa laana ya umasikiniu, magonjwa, laana mikosi, balaa, kutokuoa, kutokuolewa, ……………(endelea kutaja). Mauti na uzima vipo katika uweza wa ulimi leo ninakataa laana za aina yoyote iliyonitesa kwenye maisha yangu, nazirudisha laana zote kutoka kwa aliyezituma, kwa Jina la YESU mimi nimebarikiwa tangu sasa na hata milele. Amen.
AMEN
INFORMATION AND MEDIA MINISTRY
UFUFUO NA UZIMA
DUGA MWEMBENI - TANGA

Comments