MWENYE KUMPENDA BWANA MUNGU NI YUPI?

Na Mtumishi Geofrey Mwanza.

Bwana Yesu ainuliwe?
Mithali 8:17 "Nawapenda wale wanipendao na wenye kunitafuta kwa bidii wataniona"
Mtu ampendaye Bwana Mungu ni yule azishikaye sheria zake Bwana Mungu.

Bwana anasema kuwa anawapenda wale wazishikao sheria zake.
Kuzishika sheria za Bwana Mungu sio kuzitii amri kumi peke yake maana sheria za Mungu sio kumi pekee ni nyingi sana.
Kuzishika amri za Mungu sio kwenda Kanisani pekee.
Kuzishika sheria za Mungu sio kuhubiri injili pekee.
Kuzishika sheria za Mungu ni kumkubali mwanawe wa pekee Yesu Kristo maana yeye ndiye sheria zote za Bwana Mungu.
Kuna watu hudhani kuwa wanazishika sheria za Bwana maana wao ni wahuduma Kanisani.

Kuna watu hudhani wanazishika sheria za Bwana Mungu maana wanatoa fungu la kumi kwa uaminifu na huku hawajaokoka.
Kuwa na wokovu wa Bwana Yesu Kristo ndio kuzishika sheria za Bwana Mungu.

Mungu anamaanisha anawapenda wale wampendao na kuzishika sheria zake maana wakimtafuta yeye watamuona.
Ni lazima uokoke ndio umuone Mungu.Huwezi kuona Mungu kama hujaokoka na kujitenga na dhambi.
Kuona Mungu sio kununua na kuendesha gari.Kumuona Mungu ni kuupokea uzima wa milele upatikanao kwa wokovu wa Bwana Yesu pekee.

Mpendwa okoka ndio umuone Mungu kwani mwanzo wa kumuona Mungu ni kuokoka.
Usimtafute Mungu tu ila mtafute Mungu kwa bidii maana huku ndiko anakosema Bwana.

Mungu wangu Yehova akubariki na kama haujaokoka na unasema unamtafuta Bwana Mungu ujue wajidanganya mwenyewe huwezi kumuona kwanza okoka ndio mambo yakwendee salama.
Tubu leo,acha dhambi leo na Bwana Yesu atakuifadhi na utaishi milele.
Pokea ujumbe huu katika Jina kuu la Yesu Kristo.

MUNGU wa mbinguni akubariki sana.
Ni mimi ndugu yako Mtumishi Geofrey Mwanza.
Huduma ya "The Global Evangelism Ministries".
(Kenya).
0724 656 653
Geoffreymwanza@yahoo.com

Comments