NI HERI KUIEPUKA HUKUMU LEO.

Na Mtumishi Peter Mabula.

BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Napenda tu kumwaambia mtu mmoja kwamba MUNGU atahukumu na hakuna mbingu ya watu wanaomtukuza shetani.
 Kuokoka leo ndio kitu muhimu zaidi.
Kuacha dhambi ni jambo muhimu sana na ni jambo ambalo kila mtu mwenye akili timanu  anatakiwa alitekeleze.

Hizi ni Si siku za mwisho na Biblia inasema kwamba;


'' Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa.Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.-Ufunuo 22:11-12''

Hizi ni nyakati za kila mwanadamu kuamua hatima ya maisha yake.
Sio wakati wa kulidhika na maisha ya dhambi bali ni wakati wa kuishi maisha matakatifu.
Huu ni wakati wa kuufuata uzima wa milele ambao ni kumpokea BWANA YESU na kuanza kuishi maisha matakatifu. 
Mwisho u karibu sana na hukumu iko mbele ya mwanadamu ndio maana nasema wakati huu ni9 wakati wa kuamua kuchagua njia ya uzima ambayo ni BWANA YESU. 
Tena liko onyo kubwa sana kutoka kwa MUNGU kuja kwa wanadamu likisema;

'' Kwa maana hiyo siku ya BWANA i karibu juu ya mataifa yote; kama ulivyotenda, ndivyo utakavyotendwa; malipo yako yatakurudia juu ya kichwa chako mwenyewe.-Obadia 1:15 ''


 Siku ya BWANA i karibu, ni siku ya kuwahukumu wanadamu.
Kila mwanadamu atalipwa sawasawa na matendo yake aliyoishi duniani.
Wanadamu walio wengi maisha yao hayampendezi MUNGU.
Ulimwengu kwa sehemu kubwa umeathiliwa na mambo mabaya ambayo yamejaa kila maeneo.
Siku hizi watu kujitangaza kwamba wao ni mashoga imekuwa jambo la kawaida.
Siku hizi watu kujitangaza kwamba ni waabudu shetani imekuwa jambo la kawaida sana.
Ni siku za mwisho lakini wanadamu wengi ingawa wanalijua hilo lakini hawaendani na Neno la MUNGU linavyotaka.
Wanadamu walio wengi wala hawaitii tena Biblia.
Mfano Hapa Dar es salaam maduka ya nguo za watu wazima ni machache kwa sababu watu wazima wengi siku hizi wanavaa nguo za watoto, hivyo wauza nguo sasa wanauza tu nguo za watoto maana hizo ndizo na watu wazima wanavaa.
Unakuta mama wa miaka 55 amevaa ki gauni kimevuka magoti, na wakati mwingine unakuta mama wa miaka 48 amevaa kigauni kinachoishia mapajani na kwa hesabu za kawaida kabisa kigauni kama hicho angevaa mtoto wa miaka 11 au 12 angependeza sana na sio watu wazima wanaong'ang'ania nguo hizo.
Ukitembea madukani siku hizi ni rahisi sana kuona wamama wa miaka 30 na kuendelea wanajaribishia nguo ambazo mwenye miaka 9 ndio alitakiwa ajaribishie nguo hizo.




2 Timotheo3:1-5 ''Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema, wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda MUNGU; wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao. ''

Dunia ni kama inaenda mbele lakini kimaadili naona dunia inarudi nyuma kwa spidi kubwa kuliko inavyokwenda mbele.
Watu wengi sana wamenyeshewa na mvua ya shetani kiasi kwamba hata wakishauriwa hawaelewi.
Yezebeli yuko kwenye ubora wake wa kuwakamata wanadamu.

Kuna waimbaji wa nyimbo za injili wanaimba nyimbo zenye ujumbe unaogusa sana na mzuri sana lakini ukiwaona live unaweza ukawakata maksi 98% kwa sababu ya mavazi ya kikahaba wanayovaa.
BWANA YESU alisema haki yetu wateule lazima iizidi haki ya Mafalisayo(walio nje) na kama haki yetu haitaizidi haki ya mafalisayo basi uzimani hatuingii.


Mathayo 5:20 ''Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.''

=Haki ya mafalisayo inawaruhusu kuvaa nusu uchu na kufanya kila aina ya ukahaba lakini haki yetu inatutaka kumcha MUNGU hata kupitia mavazi yetu.
=Kuwa mteule ni kujikana na sio blaablaa za mitaani.
=Kuiga dunia ni kumuiga shetani.


 Samaki mmoja akioza mtoe na mtupe mbali ili wengine waendelee kuwa safi.
Kwa kanisa; Muumini mmoja akikengeuka hatutakiwi kulihukumu kanisa zima bali atengwe au asaidiwe au aondolewe.

mambo ya kidunia mengine mpaka yanaingia kanisani na kunajisi kanisa zima.

 Matendo  3:19 ''Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake BWANA;''


Kuna maisha ya wana kanisa ambayo yanasababisha baadhi ya watu washindwe kuokoka kwa sababu hawaioni tofauti ya huyo anayedai ameokoka na yeye ambaye hajaokoka.
Ndio maana mafundisho ya utakatifu kwa kanisa ni muhimu sana wakati huu kuliko aina nyingine ya mafundisho.
Kanisa halitakiwi kuifuata dunia bali dunia ndio ilifuate kanisa.


1 Timotheo 3:14-15 '' Nakuandikia hayo nikitaraji kuja kwako hivi karibu. Lakini nikikawia, upate kujua jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya MUNGU, iliyo kanisa la MUNGU aliye hai, nguzo na msingi wa kweli. '' 
 Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichaka chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili.

 

Comments