PETE YA BIBI ARUSI YAPOTELEA KANISANI SIKU YA ARUSI MASAA MACHACHE BAADA YA KUKATA KEKI

Na Mtumishi Geofrey Mwanza.

Bwana Yesu ainuliwe?
Mapema mwaka jana nikiwa katika maombi ya kuona mtu mmoja mmoja almaarufu (one on one)Kanisani nilikutana na dada mmoja liyekuja nimwombee na alinipa kisa kimoja cha kuongofya na kustaajabisha.
Katika siku ya arusi yake alipotiwa pete kidoleni na mume wake, wakakata keki na kulishana masaa mawili baadaye alipata kuwa pete yake haikuwa kidoleni tena!
Huu ulikuwa mshituko na hofu kuu sana kwani pete kaenda wapi na ilikuwa yatoshana na kidole vizuri?
Je, imekuwaje pete bado yapotelea katika mazigira ya Kanisani!
Kutoka hapo walipofika nyumbani kwa lango la kuingia bomani alipatikana joka mkubwa sana na kisha akauawa.
Ilikuwa hofu kuu kwa dada yule anapoukaribisha umama ndani yake kwani baada ya miezi miwili mumewe akabadilika na kuwa mlevi chakari na hata akawa hajielewi kabisa.
Kwa muda huo huo majoka yalikuwa yakiuliwa ndani ya boma lile huku kila mmoja akijionea kioja kama Musa.
Dada alipata mimba kisha ikawa inamsumbua sana kwani akiwa wiki mbili kujifungua daktari alimlazimu alazwe spitalini aongezwe damu kwani kiasi kile kilikuwa kidogo sana kwa mwanadada yule kujifungua.....
Ni vizuri sana wadada /wandugu mnaoingia kwa ndoa mkawa waombaji sana ili kuziepuka balaa kama hizi.
Shetani anaweza kutumia pete yako kukufunga hata wakati wa arusi yako.
Shetani anaweza kutumia anayekufungisha ndoa akakufunga.
Shetani anaweza kutumia anayekusimamia harusi yako kukufunga.
Shetani anaweza kutumia zawadi unazoletewa na marafiki kukufunga.

Shetani anaweza kutumia mahali unapofungishiwa ndoa kukufunga.
Shetani anaweza kutumia keki unayokata kukufunga.
Shetani anaweza kutumia ajenti wake akakuiba mbegu za uzazi wakati wa arusi ikawa hata mkioana hamtapata watoto.
Shetani anaweza kutumia chochote kinachohusiana na maandalizi ya harusi yako kukufunga.
Mungu anaweza kunitumia mimi Geoffrey Mwanza ili yeye (Mungu) akufungue kupitia kukuhubiria Yesu Kristo ambaye atakuokoa.

Hii ndiyo maana wakazi wa kijiji cha Kana ya Galilaya walimwalika Yesu kwa harusi iliyokuwa pale kwani walijua kuwa wakimwalika Bwana Yesu harusini hiyo mambo yatakuwa shwari.
Yohana 2:1 kuendelea.
Kwanini tumwalike Bwana Yesu harusini zetu na kwa mioyo yetu?
1Yohana 3:8b "Kwa maana mwana wa Mungu alidhihirishwa kuzivunja kazi za ibilisi".
Anza kuiombea ndoa yako leo na itafunguka.
Kama hujaokoka tubu na uokoke leo Mungu anakupenda sana.


MUNGU wa mbinguni akubariki sana.
Ni mimi ndugu yako Mtumishi Geofrey Mwanza.
Huduma ya "The Global Evangelism Ministries".
(Kenya).
0724 656 653
Geoffreymwanza@yahoo.com

Comments