SHEREHE YA MAPINDUZI

Na Mchungaji  MACHUMU MAXMILIAN, Ufufuo na uzima.



Esta 9: 24 kwa sababu Hamani bin Hamedatha, Mwagagi, adui ya Wayahudi wote, alikuwa amefanya shauri juu ya Wayahudi ili kuwaangamiza, akapiga Puri, yaani kura, ili kuwakomesha na kuwaangamiza pia; bali mfalme alipoarifiwa, aliamuru kwa barua ya kwamba hilo shauri baya alilolifanya juu ya Wayahudi limrudie kichwani pake mwenyewe; na ya kwamba yeye na wanawe watundikwe juu ya mti. Hivyo wakaziita siku hizo Purimu, kwa jina la Puri. Basi, kwa ajili ya maneno yote ya barua hiyo, na kwa yale waliyoyaona wenyewe juu ya jambo hilo, na mambo yenyewe yaliyowajia, Wayahudi wakaagiza na kutadariki juu yao wenyewe, na juu ya wazao wao, na juu ya wote watakaojiunga nao, isikome, ya kwamba watazishika siku hizo mbili sawasawa na andiko lile, na kwa majira yake kila mwaka; siku hizo zikumbukwe na kushikwa kwa vizazi vyote na kila jamaa, katika kila jimbo na kila mji; wala siku hizo za Purimu zisikome katikati ya Wayahudi, wala kumbukumbu lake lisiishe kwa wazao wao. Ndipo malkia Esta, binti Abihaili, pamoja na Mordekai Myahudi, alipoandika kwa mamlaka yote kuithibitisha barua hii ya pili ya Purimu. Amri yake Esta ikayathibitisha mambo hayo ya Purimu; ikaandikwa katika kitabu.”
Esta 2:17 “Mfalme akampenda Esta kuliko wanawake wote, naye akapata neema na kibali machoni pake kuliko mabikira wote; basi akamtia taji ya kifalme kichwani pake, akamfanya awe malkia badala ya Vashti.”
Esta 6:6 “ 1 Usiku ule mfalme hakupata usingizi; akaamuru aletewe kitabu cha maandiko ya taarifa, nayo yakasomwa mbele ya mfalme.
2 Ikaonekana kuwa imeandikwa ya kwamba Mordekai aliwachongea Bigthana na Tereshi, wasimamizi wawili wa mfalme, katika hao waliolinda mlango, waliotaka kumtia mikono mfalme Ahasuero.
3 Mfalme akasema, Je! Ni heshima gani au jaha gani Mordekai aliyofanyiziwa kwa ajili ya hayo? Watumwa wa mfalme waliomhudumu wakamwambia, Hakuna alilofanyiziwa.
4 Mfalme akasema, Yupo nani behewani? Ikawa Hamani alikuwa ameingia katika ua wa nje wa nyumba ya mfalme, aseme na mfalme, ili kumtundika Mordekai juu ya mti ule aliomwekea tayari

Basi watumwa wa mfalme wakamwambia, Tazama, Hamani yupo, amesimama behewani. Mfalme akasema, Na aingie.Basi Hamani akaingia. Mfalme akamwambia, Afanyiziwe nini yule ambaye mfalme apenda kumheshimu? Hamani akasema moyoni mwake, Ni nani ambaye mfalme apenda kumheshimu kuliko mimi? Basi Hamani akamwambia mfalme, Yule ambaye mfalme apenda kumheshimu, na aletewe mavazi ya kifalme ambayo mfalme amezoea kuyavaa, na farasi ambaye mfalme humpanda mwenyewe, ambaye ametiwa taji ya kifalme kichwani; na yale mavazi na yule farasi akabidhiwe mkononi mmojawapo wa maakida wa mfalme aliye mstahiki; ili makusudi amvike yule ambaye mfalme apenda kumheshimu, na kumrakibisha juu ya farasi kuipitia njia kuu ya mjini, na kupiga mbiu mbele yake, kusema, Hivyo ndivyo atakavyofanyiziwa mtu yule ambaye mfalme apenda kumheshimu. Basi mfalme akamwambia Hamani, Hima! Twaa mavazi na farasi kama ulivyosema, ukamfanyizie vivyo hivyo Mordekai, Myahudi, aketiye mlangoni pa mfalme; lisipungue neno lo lote katika yote uliyoyasema.Ndipo Hamani alipoyatwaa mavazi na farasi, akamvika Mordekai yale mavazi, akamrakibisha juu ya farasi kuipitia njia kuu ya mjini, akapiga mbiu mbele yake, Hivyo ndivyo atakavyofanyiziwa mtu yule ambaye mfalme apenda kumheshimu.Kisha Mordekai akarudi kwenye mlango wa mfalme. Bali Hamani akaenda mbio nyumbani kwake, mwenye msiba, na kichwa chake kimefunikwa.”
Mungu alifanya mapinduzi wakati haman alipokuwa akienda kwa Mfalme ili akamtundike Modekai kwenye msalaba, Mungu alifanya mapinduzi ambayo yalisababisha vile vitu ambavyo Modekai
alistahli kufanyiwa vitokee vilevile kabla ya haman hajavipata.

Kwenye maisha yetu kuna baadhi ya mambo ambayo unatakiwa uyapate lakini kuna mtu ambaye amekuingilia ili ayamiliki na inawezekana mtu huyo ni Bosi wako kazini anatumia nyota yako ya kupendwa, ndugu yako amekufunika ili usionekane au rafiki yako amemiliki kile ambacho Mungu amekupa.
Modekai alivipata vitu ambavyo alistahili kuvipata na yule mbaya wake Hamani ambaye alivitaka vitu hivyo alikuwa akimpigia mbiu kila kona. Mfalme ameagiza Haman apewe anachostahili. Kwenye maisha haya kuna watu wanapitia mwanzo mgumu kwenye maisha yao lakini Mungu anafanya mapinduzi ya jambo ambalo kila mtu akisikia lazima astaajabu na haya ndio mapinduzi ambayo yanastahili kusheherekewa. Ni Mungu asiye na upendeleo kwa aliyepata au ambaye hajapata.
Esta hakupenda maisha yale aliyokua akiishi lakini Mungu alikuwa anamuona na alimfanyia mapinduzi ambayo yalileta sherehe kubwa. Wanawake wazuri wa mji ule waliachwa, wenye sifa njema na wenye elimu waliachwa, walioonekana wazuri machoni pa watu na kufaa waliachwa na Mungu akafanya mapinduzi la ajabu kwa Esta ambaye alikuwa sio mtu wa taifa hilo.
Mapinduzi ni mabadiliko ya muda mfupi ambayo hutokea na kufanya vibadilike kwa muda mfupi. Mapinduzi haya sio ya kisiasa au nchi, ni mapinduzi ya kwenye ulimwengu wa Roho.Matendo ya Mitume 17:6 “na walipowakosa, wakamkokota Yasoni na baadhi ya ndugu mbele ya wakubwa wa mji, wakipiga kelele, wakisema, Watu hawa walioupindua ulimwengu wamefika huku nako.”
Ezekieli 21: 27 “Nitakipindua, nitakipindua, nitakipindua; hiki nacho hakitakuwa tena, hata atakapokuja yeye ambaye ni haki yake; nami nitampa.”
Mungu ameahidi mapinduzi na mapinduzi hayo yanaendelea mpaka leo hii. Esta na Mordekai walimwamini Mungu pamoja na mazingira waliokuwa wanayapitia kuwa magumu sana.
Kwenye bustani ya Eden shetani aliingia akafanya mapinduzi lakini Yesu alikuja na kufanya mapinduzi ambayo yametupa kusheherekea. Uko uwezo wa Mungu kwenye ulimwengu wa Rohoni ambao unafanya mapinduzi ya uhakika kwenye maisha yetu ya kila siku.
Mordekai alikuwa akimpendeza Mungu sana kiasi cha kutokubali kumuinamia mtu yeyote isipokuwa Yehova. Modekai hakuacha kumwabudu Bwana na hakuona aibu kumkiri mbele za watu.
Haman alitangaza si kwa Modekai peke yake bali ni kwa wayahudi wote. Haman aliamua kupanga siku moja ili wayahudi wote wauawe lakini Mungu alifanya mapinduzi ambayo yaliwastaajabisha watu wote.
Esta pamoja na wayahudi waliamua kufunga na kuomba ili Mungu awaokoe. Walifunga siku tatu kuomba kwanza yale mambo yasiyowezekana yawezekane, na cha pili Mfalme abatilishe mabaya waliyoyapanga adui zao. Pia aliomba hekima ya kuongea na Mfalme ndipo aliapoamua kwenda kwa Mfalme kinyume na sheria. Mfalme alipomwona Esta alimnyoosheta fimbo ya dhahabu na kumruhusu aingie ndani japo ilikuwa kinyume na sheria.
Hekima ya mwanamke Esta ilimsaidia baada ya kumwandalia chakula kizuri. Hekima nzuri kwenye ndoa kama mwanamke unataka kumwomba kitu mume wako lazima umpe chakula kizuri ale, ashibe ndipo umweleze shida yako kama Esta alivyofanya kwa Mfalme kwa hekima yake aliyopewa na Mungu
Mfalme alipokula kile chakula alimuuliza Esta nini kilichomleta kwake na ndipo Esta akamwelezea yeye na ndugu zake wanataka kuuwawa na Haman na ameandaa mti ili amtundike modekai. Mfalme aliposikia hayo aliamuru maakida wakamtundike Haman kwenye mti uleule aliouandaa kwa Modekai na ule waraka haukutekelezwa juu ya wayahudi
Leo Mungu bado anafanya mapinduzi kwako na utasheherekea jinsi Bwana atakavyofanya mapinduzi ya shida zako na utakuwa huru na kusheherekea kwa jina la Yesu.

Comments