TAFUTA INJILI ISIYOGHOSHIWA

Na Mtumishi Peter Mabula.
BWANA YESU atukuzwe,
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Neno la MUNGU ni upanga wa ROHO MTAKATIFU.
Ukimkataa ROHO MTAKATIFU wewe umeikataa Biblia.
Kumkataa ROHO wa MUNGU ni kuikataa mbingu.


Waefeso 6:17 '' Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa ROHO ambao ni neno la MUNGU;''

Neno la MUNGU ni upanga wa ROHO wa MUNGU.
Katika maisha yako mtake sana ROHO MTAKATIFU na nguvu zake.

Injili iliyo sahihi ni injili inayowataka watu kuukimbilia Wokovu wa BWANA YESU.
 
Waebrania 4:12 ''Maana Neno la MUNGU li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.''
Kujua Kwamba Unahitaji Dhambi Zako Zisamehewe Ni Hatua Ya Kwanza Ya Kuutaka Uzima Wa Milele. Dhambi Ni Deni Kubwa Ambalo Ni Lazima Lilipwe. Dhambi Ni Mzigo Mzito Sana Unaotakiwa Uondolewe Kwenye Kichwa Cha Mtu Na Utupwe Chini Huo Mzigo.

Mathayo 11:28 '' Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. ''
 
Jambo muhimu ni kumfuata YESU na kuishi maisha mataktifu.
Kuna baadhi ya watu waliojikinai hupotosha watu wa MUNGU.
Sio makanisa yote hutumia Biblia kama ndio kanuni yao ya imani.
Sio wote wanaoitwa wakristo wanaye KRISTO ndani yao.
Sio kila anayesema BWANA YESU asifiwe yuko safari ya mbinguni.

 2 Petro 3:3 '' Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika siku za mwisho watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe,''

Kuokoka ni kujikana sio kufuata dini ya wazazi ambayo dini hiyo haijawahi kuwasaidia wazazi wako maana dhambi bado zimewakamata hata kama wana zaidi ya miaka 40 tangu waanze kuhudhuria kwenye dini.
Aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja na kahaba.
Jiulize swali hili;
Kama kuna watu wanasujudia sanamu wakati Biblia inakataza, Hata kama wanaitwa wakristo je wanajitambua na wanamtambua BWANA YESU?
biblia inasema;

 " Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba
ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale
wawili watakuwa mwili mmoja. ” 1 Wakorintho
6:16.

 
Kama kuna watu ni mwili mmoja na kahaba Je unadhani walio mwili mmoja na sanamu watakosekana?
Kama watu ni mwili mmoja na kahaba je walio mwili mmoja na shetani watakosekana?
Unaloga na kanisani unaenda wewe ni mwili mmoja na shetani.
Unaiba na kanisani unaenda wewe ni mwili mmoja na shetani.
Sio wote waitao BWANA BWANA watakaoingia paradiso Bali watakatifu tu.

wewe ambaye bado umeng'ang'ania katika uovu huku unaenda kanisani ni kwa sababu tu hitaki injili iliyo hai, ya wokovu na uzima.

Matendo 3:19 ''Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake BWANA;'' 

 Anayedhani anajua huku akiendelea na dhambi Huyo hajui na anatakiwa kujua kwamba hakuna mbingu ya watenda dhambi.

Utu uzima ni dawa lakini utu uzima wa kiroho ni dawa kuu na baraka kuu.
Maana mtu mzima kiroho hakosi kuzijua hila za shetani na kuziepuka.


Miungu kama haina manabii huwa haina nguvu.
shetani kama hana mawakala wake hawezi kuvuma wala kuonekana ndio maana shetani huwateka baadhi ya watu wanaomkataa KRISTO na kuwafanya manabii zake.
Ndio maana leo manabii wengi wa uongo wamejaa kila kona.
Manabii hawa wa uongo wengi wao hata hawaitwi majina kwamba ''Nabii' bali wanaitwa majina mengine mazuri tu ili kuwapoteza watu wa MUNGU.



Mathayo 24:23-27 ''Wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule msisadiki. Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule. Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele. Basi wakiwaambia, Yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani, msisadiki. Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. '' 

Ukweli ni kwamba sio kila dini inatokana na MUNGU wa mbinguni.
Ukweli ni kwamba sio kila dhehebu hata kama lina miaka 1500 eti linatokana na MUNGU wa mbinguni.
Sio kila jengo la Ibada lina waabudio halisi.
Ndugu zangu hizi ni nyakati za kuwa makini sana.

Wokovu wa KRISTO upo na unamhitaji kila mmoja.
Mwenye sikio la kusikia anaweza kuisikia leo.

Waefeso 4:22-24 ''mvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu wa zamani, unaoharibika kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya; na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu; mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya MUNGU katika haki na utakatifu wa kweli.''

 ishi maisha matakatifu, ongeza maombi na jifunze Kwa walioshinda
Epuka kujilinganisha na wasio kwenye majaribu wakati huu.
Ita damu ya YESU na jina la YESU.
Kesho yako haitakuwa kama leo yako.
Tunza siri zako na shirikisha mchungaji wako. Epuka dhambi na Baraka yako I karibu yako sana.
Usijiue maana kujiua ni kujipeleka jehanamu.
Kujiua ni kuongeza tatizo na sio kupunguza tatizo.
Mtii KRISTO na Neno lake utaishi.


 1 Kor 6:9-11 ''Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa MUNGU? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa MUNGU, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi. Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la BWANA YESU KRISTO, na katika ROHO wa MUNGU wetu.''
 Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichaka chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili.


Comments