TOFAUTI KATI YA HUDUMA /OFISI NA KARAMA/KIPAWA

Na Mtumishi Geofrey Mwanza.

Bwana Yesu asifiwe?
Huduma/ Zawadi ni ofisi maalum mtu fulani anayopewa na Mungu ili kuthibitisha utumishi wa kazi ya Mungu.
Karama/talanta/kipaji ni kipawa cha utenda kazi ili kuhakikisha kuwa huduma imesimama kikamilifu.
Kunao watu ambao wanachanganywa na maneno haya mawili yaani "Huduma" na " Karama"
Waefeso 4:11-12 "Ndiye aliyewapa watu zawadi,wengine aliwajalia wawe mitume,wengine manabii,wengine waeneza injili, wengine wachungaji na waalimu.
Alifanya hivyo apate kuwatayarisha watu wote wa Mungu kwa ajili ya kazi ya huduma ya Kristo ili kuujenga mwili wa Kristo".
1Wakorintho 12:4 -11 "Vipaji vya Roho ni vya namna nyingi bali Roho avitoaye ni mmoja.Kuna namna nyingi za kutumikia lakini Bwana anayetumikiwa ni mmoja.
Kuna namna mbalimbali za kufanya kazi ya huduma lakini Mungu ni mmoja anayewezesha kazi zote katika wote...."

Karama/kipawa/kipaji hupeanwa na Roho ili kufanikisha huduma.Haimaanishi kuwa kila mwenye kipawa ana huduma, unaweza kuwa na kipawa/karama na Mungu akakuweka chini ya mtu aliye na huduma ili kipawa chako cha uimbaji kitumike pale penye mwenye huduma ya kinabii/kimitume.
Kuna watu leo wakijua kuwa ni waimbaji/waombezi wanakimbia kufungua Kanisa bila kujua kuwa ile karama yao Mungu ameiweka ikae chini ya huduma ya mtu fulani.
Pia kuna wenye huduma wengi wanaowakanyagia/wanawazuia wenye karama fulani kisa na maana unaona kama huyu atahubiri kwa Kanisa langu upako wake utaonekana kuzidi upako wangu.
Ndugu mwenye huduma,husimkanyagie mwenye karama yake kumtumikia Mungu ndani ya huduma uliyopewa na Mungu maana Mungu amemweka pale si mshindane bali mwkamilishe huduma ya Kristo.
Nawe mwenye karama fulani sikiliza,husiwe na kiburi hata kama unaona upako wako wamshinda wa mwenye huduma.
Upako wako hauwezi kuzidi wa mwenye huduma vile vile tu mwanafunzi hawezi kumshinda mwalimu au mtoto kamzidi maarifa babaye.
Tumtumikieni Mungu na kutumia huduma hizi na karama zote kwa kuwavuta watu kwa Bwana Yesu bali si kwa kujisifu.
Upako hauna cha mimi ndio nilikufunza kuimba/kuhubiri.Hutegemea na neema Roho atakayomneemesha mtu.
Mungu anatupenda site na anataka tuhubiri injili ya kweli isiyo na mwegemeo wowote.
Kemea dhambi,fundisha ukweli,fungua wafungwa,toa unabii wa kweli kama umejaliwa na usimpige mwenzako vita vya kihuduma.
Kama umeusoma ujumbe huu na haujaokoka okoka leo.
Ubarikiwe sana naukae katika upendo wa kikristo maana Kristo mwenyewe ni upendo.
MUNGU wa mbinguni akubariki sana.
Ni mimi ndugu yako Mtumishi Geofrey Mwanza.
Huduma ya "The Global Evangelism Ministries".
(Kenya).
0724 656 653
Geoffreymwanza@yahoo.com

Comments