UKIWASHWA SANA MEZA MAJI YALIO HAI

Na Mtumishi Geofrey Mwanza.
Bwana Yesu asifiwe?

Yohana 4:13-14 "Yesu akamjibu akamwambia kila atakayekunywa maji haya ataona kiu tena.Lakini atakayekunywa maji nitakayompa hataona kiu tena"
Leo nimevaa mavazi ya uinjilisti upende usipende lazima uondoke hapo umekwamia kwa kutomtii Mungu.
Mungu ni mtakatifu na anatutaka tuishi kama yeye.Ujumbe huu ni wangu na wewe si wako peke yako wala wangu peke yangu.
Kwanini bado shingoni zetu tumevaa shanga za uovu na huku tunasema sisi ni wana wa Mungu!?
Watoto wa Mungu tunapaswa kufanana na Baba yetu.
1Yohana 3:9-10 "Kila aliye mtoto wa Mungu hatendi dhambi,maana anayo hali ya kimungu ndani yake, hawezi kutenda dhambi kwa sababu yeye ni mtoto wa Mungu...."
Ni lazima wahubiri tuihubiri injili ya kuwasongeza watu wa Mungu kwa Mungu wao bali sio kuzidi kuwapoteza.
Mimi nitakwambia ukweli leo utake usitake.Mungu hawezi kukuondolea hicho kinachokutatiza kama hutakubali kuokoka.
Hata kama ulikutana na nani na ukapanda mbegu ya sadaka ujue ulidanganywa hautafanikiwa ng'o!
Nani akupe gari huku wewe ni mwizi mkubwa?
Nani akupe ndoa na huku unawaliza dada wenzako kwa kuwapokonya waume zao?
Acha ukahaba kwanza na uokoke ndio uolewe!
Ondoa masengenyo kinywani mwako ndio Ubarikiwe!
Umefanya urafiki na wachungaji heti ni ndugu na dada na unataka kutwaa upako! Uko juu ya laana na utakufa hata ukikataa.
Waficha dhambi Mchungaji heti kila mtu ataubeba mzigo wake! huku ukikosa kuikemea dhambi Kanisa lisivunjike!
Acha pombe mzee wa Kanisa na uokoke.
Acha kiburi mtumishi na uokoke.
Acha ufisadi ndugu yangu na uokoke.
Acha Tabia ya kutoa mimba na uokoke.
Acha uasherati na uokoke.
Acha kuiinamia sanamu na umwinamie Bwana Yesu atakuokoa.
Acha kufitinisha familia za watu huku zikivunjika unafurahia.Okoka sasa na umwendee Yesu.
Wacha kusengenya wachungaji na uokoke leo.
Achana na kutumia nguvu za giza Kanisani mtumishi na uokoke Bwana Yesu atakusamehea.
Wacha kumchukua mke/mume wa watu na kumfanya mkeo/mumeo.

MUNGU wa mbinguni akubariki sana.
Ni mimi ndugu yako Mtumishi Geofrey Mwanza.
Huduma ya "The Global Evangelism Ministries".
(Kenya).
0724 656 653
Geoffreymwanza@yahoo.com

Comments