UNA HABARI GANI?-01

Na Mwl Nickson Mabena.

"Wakawaletea wana wa Israeli habari mbaya ya ile nchi waliyoipeleleza, wakasema, Ile nchi tuliyoipita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi inayowala watu wanaoikaa; na watu wote tuliowaona ndani yake na watu warefu mno". HESABU 13:32
Bwana Yesu asifiwe Mtu wa Mungu, popote pale ulipo,
Ninamshukuru Mungu kwa ajili yako unayeusoma Ujumbe huu,
Pia namshukuru sana Mungu kwa kunipa nafasi ya kuliandika somo hili.

Mwaka 2014, kwa mara ya kwanza nilifiks Mkoa wa Singida kwa ajili ya Huduma,
Tulikua na Semina pamoja na Mkutano wa Injili, kwenye Huduma ile Mimi nilikua Miongoni mwa Walimu wa Semina,
Siku moja kabla ya Vipindi Vya Semina Kwa siku hiyo kuanza, tulipita Mtaani kushuhudia Habari za Yesu anayeokoa,
Tuliingia kwenye kilabu kimoja cha pombe, ili kumtangaza Yesu kwa Wauzaji na Watumiaji Wa Pombe,
Wakati tunaendelea Kuyasema Maneno ya Mungu, Kuna Mtu aliongea Maneno, ambayo ukiyasikia, yanaweza kukukatisha tamaa ya kuendelea kushuhudia,
Naweza nisikumbuke yote kwa kunukuu, lakini ujumbe nikawa naukumbuka,
Alisema, "Nyinyi mnatuambia TUOKOKE, Mbona flani, anaabudu hapo Kanisani, yupo hivi!?, (akawa anataja shuhuda mbaya za watu waliookoka)."
Wakati anaendelea, Roho Mtakatifu, akaniwekea Ujumbe ndani yangu, niliuhubiri kwenye Semina ile,
Ujumbe wenyewe ulinipa kutoka kwenye Hesabu 13,
Kule Singida niliupa Kichwa kinasema, "UNA HABARI?, HABARI GANI"
Mungu alinifundisha Vingi, vichache ndio nakushirikisha Kwenye Somo hili!.
👉WOKOVU NI NCHI YA AHADI, ULIYEOKOKA NI KAMA MPELELEZI.
Kabla ya Wana wa Israel hawajaingia kwenye Nchi ya Ahadi, Mungu akamwambia Musa awatume watu ili Watu Wakaipeleleze nchi,
Mungu alisema "Tuma watu, ili waende wakaipeleleze nchi ya Kanaani, niwapayo wana wa Israeli;........". HESABU 13:2
Watu hao waliotumwa, Walitakiwa Warudishe Habari (ripoti), ya Walichokiona Kwenye Nchi Walioingia kuipeleleza.
Sasa, tutafakari Pamoja,
Kati ya Wale watu kuna wengine walikua hawajawahi, kuikanyaga ile nchi, Isipokuwa, Wale Walioenda,

Naweza nikasema, Uliyeokoka, umeingia kwenye 'nchi ya ahadi', Kuna Watu hawajaokoka, Wanasubiri 'habari', kutoka kwako uliyeingia!.
👉KUINGIA, AU KUTOKUINGIA KULITEGEMEA HABARI YA WAPELELEZI.
Tuendelee kutafakari, kuingia au kutokuingia kwa Mkutano Wa Wana wa Israeli, kulitegemea na Aina ya Habari watakazoletewa na WATU Walioenda Kuipeleleza Ile Nchi!.
Kwa hiyo naweza nikasema Kuna Watu hawajaokoka, Lakini Kuokoka kwao kunategemea Habari watakazopewa na Waliookoka!.
Ni, pagumu kidogo lakini Utanielewa tu!.
Kwenye andiko letu la somo hili, Tunaambiwa, WALE WAPELELEZI, WAKAWALETEA WANA WA ISRAELI, HABARI MBAYA YA ILE NCHI!.
Habari hizi, hazikua Mbaya za Kawaida, Zilikua Habari mbaya zinazokatisha tamaa, zinazovunja moyo, zinazorudisha nyuma, zinazoonyesha kwamba nchi ya ahadi, ni nchi MBAYA SANA!.
Ndio Maana Walipozisikia zile habari, "Mkutano wote wakapaza sauti zao; watu wakatoka machozi usiku ule". HESABU 14:1
Kwa hiyo, naweza kusema kwamba, Kuna Watu hawana Mpango wa Kuokoka kwa sababu ya Habari Mbaya unazowapa kuhusu Wokovu!.
Wao wanakuangalia wewe uliyeokoka.
Angalia huo mfano mdogo tu, niliokupa Hapo juu,
Watu wamethaminisha Maisha ya Waliookoka, Wanaona Kama ni hivyo, hakuna Haja ya Kuokoka (Ingawa hawapo sawa),
Kwa Maneno, kwa Matendo, unawapa habari watu muhusu Wokovu!.
Wewe una habari Gani!?,
Mwenyewe fikiria, nawezaje Kumwambia Mtu aokoke, wakati Jana yake tu, ametoka KUZINI na Mtu aliyeokoka!?,
Je! Unadhani atakubali tu, bila kujiuliza kwamba anaachaje Uzinzi wakati Aliyezini naye anaimba Kwaya Kanisani!?.
Wewe Binafsi, Watu Wanaokuzunguka, Wanapata Habari gani!?,
Je! Wakikutathimini, Wanatamani Wokovu ulionao, au wanakata tamaa ya Kuja Kwenye Wokovu!?..
Mkutano Mzima, Walikata tamaa ya kwenda kwenye nchi ya Ahadi, kwa sababu ya Habari Mbaya toka kwa WALIOFIKA KWENYE NCHI YA AHADI!.
Mimi leo nina Swali Moja Kwako,
UNA HABARI GANI!?.

"Wakawaletea wana wa Israeli habari mbaya ya ile nchi waliyoipeleleza, wakasema, Ile nchi tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi inayowala watu wanaoikaa; na watu wote tuliwaona ndani yake ni warefu mno." HESABU 13:32

Kwenye Somo hili tunakwenda na tafakari kwamba, Mtu uliyeokoka ni kama wale Wapelelezi, Upo kwenye Nchi ya Ahadi (Wokovu), lakini wapo watu ambao Hawajafika ndani ya Wokovu, wanasubiri HABARI Kutoka kwako, ili na wao Waje kwenye Wokovu,
Nikasema, Wapelelezi wale 12, 10 Kati yao (yaani zaidi ya robo tatu), Walileta habari Mbaya,
Habari za kukatisha tamaa, habari za kuonyesha wokovu haufai, habari ambazo waliozisikia ziliwafanya wasitamani kuokoka.
Nika kuuliza Swali, Wewe una habari gani!?.
Kupitia Maneno, Matendo, na Mwenendo wako, Watu ambao hawajamjua Mungu, wanaweza wakatamani kuokoka, au wasitake kabisa kuokoka!.
Kuna Vitu nilitaka nieleze kwenye sehemu hii ya pili, lakini Roho wa Mungu ananihimiza kuendelea na kipengele hikihiki, ila niweke msisitizo flani.
Tuyaangalie wote Maandiko yafuatayo.
MATHAYO 5
14 Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima.
15 Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani.
16 Vivyo hivyo nuru yenu iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.
👉Ukisoma vizuri Hayo Maandiko, utaona Mambo mengi ndani yake,
Yesu anasema, Mtu uliyeokoka, wewe ni nuru ya Ulimwengu,
Maana yake, kuna watu ili waone, wanakuhitaji wewe, kuna watu ili wapige hatua, wanaihitaji nuru yako,
Sasa mwenyewe tafakari, hayo Mavazi unayoyavaa, yanatupa HABARI GANI?,
yanaonyesha wewe ni Nuru au ni Giza!?,
Unasema Bwana anaangalia Moyo, haangalii mavazi, mbona umesahau kusema Wanadamu wanaangalia Mavazi!?,
Biblia imesema, ".....BWANA haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali BWANA huutazama moyo." 1SAM 16:7,

Umeona!?, Kumbe Sisi watu TUNAPATA HABARI KUPITIA SURA YAKO YA NJE, YAKIWEMO NA MAVAZI YAKO!.
Kwenye Mafundisho ya Yesu, ule mstari wa 16 kwenye hiyo Mathayo 5, anasema "Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni."
👉Wale ambao hawajaokoka, wanatazama Matendo yako na Maneno yako, ambayo huwapelekea habari, itakayowafanya wamtukuze Mungu wako, au Wamtukana!.
Habari zatakauowafanya, Waseme, Kama Kuokoka ni Kama Dada flani, basi na mimi naokoka, au Waseme, kama kuokoka ndio hivi, Basi Hakuna haja ya Kuokoka!.
👉Wapendwa, Tumemtukanisha Mungu wetu kwa Mienendo mibovu inapeleka habari mbayo kwa wasiomjua Mungu.
Sasa hivi, kuona tofauti ya watu ambao hawajaokoka na waliookoka ni ngumu kidogo,
Kwa sababu wanavaa sawa, wanaongea sawa, wananyoa sawa, tabia sawa, n.k!.
Swali langu kwako unayesoma Ujumbe huu, UNA HABARI GANI!?,
Je! Watu wanamtukuza Mungu, au Wanamdhihaki kwa Ajili yako!?.
Tusome maandiko ya Mwisho, alafu nimalize kwa sehemu hii ya Pili!.
1PETRO 2
11 Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho.
12 Mwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa.
👉Umewafungia wengi sana wasije kwenye Wakovu, kwa sababu ya Habari mbaya unazozitoa kupitia Matendo yako ya Giza!.
NATAMANI UBADILIKE, ILI YESU ATUKUZWE.....
Naomba niishie hapa, nitaendelea na somo hili, Nitaeleza mengine, Upande mwingine!.
Mungu akubariki sana!.
Somo litaendelea.....
By Mwalm Nick
0712265856
(WhatsApp#)

Comments