UNA HABARI GANI?-02

Na Mtumishi Nickson Mabena.


Bwana Yesu asifiwe sana,
Namshukutu Mungu kwa kunipa nafasi tana ya Kukuletea Ujumbe wa Neno la Bwana,

Sehemu ya kwanza na ya pili ya Somo hili, nimeelezea Jinsi habari Mbaya za Watu waliookoka, zinavyoweza kuwakatisha tamaa, au kuwazuia watu kuingia kwenye Wokovu!.
Kama hukuyasoma Masomo hayo, waweza kunitafuta fb kwa jina langu Nickson Mabena, au uitafute page yangu fb inayoitwa Utukufu Kwa MUNGU. Humo utayapata na Masomo mengine Mengi, tangu nianze kupost Miaka kama mitatu iliyopita!.
Kwenye Somo hili, Nazungumzia Upande wa Pili,
Jinsi Gani, habari Mbaya za mtu aliyeokoka, zinavyoweza Kuua huduma, au kuvunja vikundi mbalimbali Makanisani, Au Kuua kiroho cha Mtu, au Kumfanya Mtu ajione/aonekane hafai Kanisani n.k.
Tuanze kusoma andiko lifuatalo,
ISAYA 53:1
"Ni nani aliyesadiki habari tuliyoileta?
Na mkono wa BWANA amefunuliwa nani?"

👉Nilikwambia wakati tunaanza Somo, Kwamba, kwamba Habari mbaya ninazokwambia kwenye somo hili, Sio habari za Kawaida,
Ni Habari ambazo, Mtu akizisikia na akaziamini, Anakata tamaa, anazimia, anakufa kiroho, anajiskia kushindwa!.
Kwenye Isaya, Isaya anauliza Swali,
Ni nani aliyesadiki (aliyeziamini), habari tuliyoileta?, na Mkono wa BWANA YESU amefunuliwa nani!?,
Isaya alitaka tujue, Mtu anayesadiki habari Njema za Ufalme wa Mungu, Mkono wa Mungu unafunuliwa Kwake,
"Naye Yesu alikua akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina." MATHAYO 9:35
Yesu alijua,
Mtu akisadiki habari njema za Yesu, Mkono wa Wokovu ulioletwa na Yesu unafunuliwa kwake,

Ndio Maana Biblia inasema, "Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo". RUMI 10:17
Hii ina maana kwamba, Mtu anasikia kwanza Habari za Imani ya Kristo, ambazo huletwa na Neno lake linalohubiriwa na Watumishi wake, Akisadiki, akaweka kwenye matendo, basi Mkono wa Bwana Unafunuliwa kwake, na kunakuwa na Mabadiliko ndani ya Mtu huyo!.
Kama ni hivyo basi, Naweza nikasema Kinyume chake ni Kweli,
Kwamba Mtu akizisadiki Habari mbaya, Kuna Mkono wa Shetani unafunuliwa Kwake,
Na Mkono wa Shetani ukifunuliwa kwake, Kifo cha kiroho, au kukata tamaa, au hofu vinaingia ndani yake!.
Sikiliza Mtu wa Mungu nikwambie Jambo kwenye hili,
Unakuta Unaimba Kwaya, alafu unatoka Unafanya Kazi, ya Kusambaza Maneno (habari mbaya), na hujui kwamba kwa kufanya hivyo unaiua kwaya yenu!.
Kila atakayesikia habari mbaya kuhusu kwaya Yenu, haipendi tena kwaya yenu, hata kama hizo habari ni za Uongo!.
Ngoja nikuulize maswali kidogo,
Kuna Habari ngapi mbaya umezisadiki, hadi zikazaa kutomuamini au kutompenda Mtu mwingine?,
Je! Wewe huwa unatoa habari Gani?,
Najua, Kuna Mtumishi au Watumishi huwapendi, sio kwa sababu ni Wabaya, bali ni kwa sababu Ukisikia habari mbaya zinazowahusu,
Hupendi hata Mahubiri yao, kisa habari za kusikia..
Kazi ya Kusambaza habari mbaya, ni ya Mapepo,
Kama unafanya hivyo, ujue unamsaidia kazi Shetani, na wakati huu ni Mwaka wa Kumfilisi Shetani, Wewe Unamsaidia Kazi..
Maandiko yanasema, "Akatoka pepo, akasimama mbele ya BWANA, akasema, Mimi nitamdanganya". 1FALME 22:21
Liko Pepo, lenye kazi ya Kudanganya (Kusambaza habari mbaya),
Ili kudhoofisha Kazi ya Mungu,
Bila kujua, na wewe tangu uliposikia, habari mbaya za Mtumishi, bila kujali ni za kweli au uongo, Ukazisadiki,
Mkono wa pepo, ukafunuliwa kwako, ukamchukia huyo Mtumishi bila sababu,
Ukamuita Freemason na nabii wa Uongo,
Baada ya hapo, ukawapelekea habari na wengine, na wao wakasadiki, kisha wakamchukia bure.
Kibaya kwako, ni kwamba, Mwenzako hata hajui, na Mungu anazidi Kumpaka Mafuta, Huduma yake inazidi Kuchanua,
Lakini wewe, hali yako ya kiroho ni Mbaya,
Hali yako ya maombi ni mbaya, pengine ukiomba sana ni robo saa!!.
Swali langu lipo palepale,
WEWE UNA HABARI GANI?,
Je!, una habari mbaya zinazowatawanya Waliookoka, au zinazowarudisha tena!?.
Kwa leo naomba niishie hapo,
Somo litaendelea...
Mungu akubariki sana!.
By Mwalm Nick
0712265856
(WhatsApp#)

Comments