FAIDA ZA NGUVU ZILIZOMFUFUA YESU KRISTO NDANI YAKO (2)

Na Mwl. Christopher Mwakasege
Bwana Yesu asifiwe milele!

Je umeokoka? Ikiwa umeokoka, ujue basi ya kuwa, nguvu za Mungu zilizomfufua Kristo toka kwa wafu, zimo ndani yako! Nguvu hizi zimebebwa na Roho Mtakatifu aliye ndani yako! Hii ni kwa sababu imeandikwa hivi “lakini ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu” (Warumi 8:11).
Je, unajua faida kwa ajili yako – sasa wakati huu – yaani katika ulimwengu huu, kwa nguvu za Mungu zilizomfufua Kristo kukaa ndani yako? Na kama unazijua – je; unazitumia na kufaidika kwa kiwango kipi katika maisha yako? Hebu tafakari faida chache zifuatazo:


Inaendelea..........
Je umeokoka? Ikiwa umeokoka, ujue basi ya kuwa, nguvu za Mungu zilizomfufua Kristo toka kwa wafu, zimo ndani yako! Nguvu hizi zimebebwa na Roho Mtakatifu aliye ndani yako! Hii ni kwa sababu imeandikwa hivi “lakini ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu” (Warumi 8:11). Je, unajua faida kwa ajili yako – sasa wakati huu – yaani katika ulimwengu huu, kwa nguvu za Mungu zilizomfufua Kristo kukaa ndani yako? Na kama unazijua – je; unazitumia na kufaidika kwa kiwango kipi katika maisha yako? Hebu tafakari faida chache zifuatazo:

Make Money Online : http://ow.ly/KNICZ
Faida ya 4 unayotakiwa kunufaika nayo unapokuwa unazo ndani yako, nguvu zilizomfufua Yesu ni hii: “Imani uliyonayo kwa Mungu, katika Yesu Kristo, na katika neno lake – inapata uhai na inakuwa na uwezo wa kuzaa”!
Hii ni kwa sababu biblia inasema “tena kama Kristo hakufufuka, basi, kuhubiri kwetu ni bure na Imani yenu ni bure” (1 Wakorintho 15:14). Hebu oanisha maneno ya mstari huu na maneno ya mistari hii: “Imani isipokuwa na matendo, imekufa nafsini mwake” (Yakobo 2:17).
“Lakini wataka kujua, wewe mwanadamu usiye kitu, kwamba imani pasipo matendo haizai?” (Yakobo 2:20). “Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa” (Yakobo 2:26).
Imani uliyonayo kwa Mungu katika Kristo, na katika neno lake inatakiwa iwe hai! Imani yako hiyo isipokuwa hai ndani yako ni bure…yaani inakuwa haina faida kwako, wala msaada wowote kwako! Ina maana ni imani usiyoweza kuitumia! …kwa kuwa imekufa na haina uhai nafsini mwake!
Kwa mfano: Kufuatana na Warumi 10:9, 10 ukiamini au ukiwa na imani moyoni mwako, unatakiwa uokoke. Wokovu unazaliwa kama tunda mojawapo la imani iliyo ndani yako! Pia tunajua ya kuwa; “mashetani nao waamini na kutetemeka” (Yakobo 2:19), lakini hakuna shetani aliyewahi – kuokoka kwa Imani hiyo? Na pia, tuna wanadamu wanaoamini ya kuwa Mungu yuko, lakini hawakubali kuokoka! Hii ina maana ya kuwa unaweza ukawa na imani na isikusaidie.
Kwa nini? Kwa sababu; 1. Imani pasipo matendo imekufa; na 2: Imani pasipo matendo haizai! Je, Imani uliyonayo iko hai au imekufa? Je, Imani uliyo nayo ni tasa au inauwezo wa kuzaa kilichomo ndani yake? Kumbuka – hata ikiwa imani yako uliyonayo katika Kristo Yesu na katika neno lake inapigwa vita (1 Timotheo 6:12) au inajaribiwa (Yakobo 1:3) – bado imani hiyo inatakiwa ikuzalie matunda mazuri!
Ndiyo maana imeandikwa hivi: “Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi (uvumilivu). Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno” (Yakobo 1:2-4).
Ni maombi yetu kwa ajili yako wiki hii ya kwamba: Nguvu zilizomfufua Yesu zilizomo ndani yako, zitaihuisha imani yako, ili iwe hai – kama imekufa! Na kama iko hai – basi, iendelee kuwa hai na izae matunda ya kile kilichobebwa na imani hiyo! …Katika jina la Yesu – Amen!


 Faida ya 5 unayotakiwa kunufaika nayo nguvu zilizomfufua Yesu zinapokuwa ndani yako ni hii: “Imani uliyonayo moyoni mwako inatakiwa iunganishwe na maneno ya kinywa chako kwa msaada wa nguvu za ufufuo zilizo ndani ya moyo wako!”
Kufuatana na Mathayo 12:34 kinywa huwa kinanena yale yaliyojaa moyoni! Lakini, pia, kuna wakati kinywa hicho hicho, kinauwezo wa kusema ambacho hakitoki moyoni mwa msemaji huyo!
Hii ni kwa sababu biblia inasema hivi: “Watu hawa huniheshimu kwa midomo, ila mioyo yao iko mbali nami” (Marko 7:6). Na kwa ajili hiyo kufuatana na Marko 7:7, hawapati faida yo yote kumheshimu na kumwabudu Mungu katika hali ya namna hiyo.
Imani ya mtu inayoonekana au kusikiwa kwa njia ya maneno ya mtu, inakuwa na nguvu, ikiwa imeunganishwa na imetokana na msukumo wa imani iliyomo moyoni mwa msemaji.
Hebu soma na kutafakari mstari huu wa biblia pamoja nasi: “Lakini kwa kuwa tuna roho ile ile ya imani; kama ilivyoandikwa, naliamini, na kwa sababu hiyo nalinena; sisi nasi tunaamini, na kwa sababu hiyo twanena” (2 Kor 4:13).
Ingawa mtu asiye na nguvu hiyo iliyomfufua Kristo ndani ya moyo wake, anaweza akawa na imani ya namna hii (Soma Luka 7:2 – 10); lakini Roho aliyemfufua Yesu anapokuwa ndani yako, anakurahisishia kuunganisha imani iliyo moyoni mwako – na maneno ya kinywa chako!
Kumbuka msingi huu: unaposema unachoamini kilichoko moyoni mwako, unapokea hicho ulichosema! Msingi huu unafanya kazi kote kote – kwa kitu kizuri na kwa kitu kibaya. Soma 2 Kor 4:13 na Mathayo 15:18 – 20 na Yakobo 3:8 – 12.
Ni maombi yetu kwa ajili yako wiki hii, ya kwamba Mungu akujalie neema ya kujaza imani moyoni mwako. Na nguvu za ufufuo zilizo ndani yako, ziwezeshe kinywa chako kusema maneno yaliyojaa imani hiyo!
Na Mungu anapojibu maombi yetu hayo tuombayo kwa ajili yako – neno lake hili la 2 Samweli 23:2 litimie maishani mwako – nalo linasema hivi: “Roho ya Bwana ilinena ndani yangu, na neno lake likawa ulimini mwangu”.


 Faida ya 6 unayohitaji kunufaika nayo kwa msaada wa nguvu zilizomfufua Yesu zilizomo ndani yako ni hii: “Nguvu hizo zinampa Yesu uhalali wa kuwa mdhamini wako katika maisha yako ya hapa duniani”!
Unapookoka unaingia kwenye uhusiano kiagano na Mungu. Yesu amefanyika “mdhamini wa agano lililo bora zaidi” (Waebrania 7:22). Agano linalosemwa hapa tunalijua zaidi kama “agano jipya” (Luka 22:20).
Kila aliyeokoka ni sehemu halali ya agano hili, na kwa ajili hiyo Yesu anakuwa mdhamini wake! Ikiwa wewe umeokoka, basi ujue Yesu ni mdhamini wako halali kisheria!
Biblia inaendelea kusema juu ya faida ya udhamini huu ya kwamba: “Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai siku zote ili awaombee (Waebrania 7:25). Neno hili “awaombee” pia lilivyotumika katika mstari huu lina maana ya “awatetee”. Huu utetezi unaofanyika ni kama ule unaofanywa na wakili mahakamani, au mahali popote utetezi wa kisheria unapotakiwa!
Kwa mfano unapoomba kazi mahali – mara nyingi huwa unatakiwa uweke majina angalau mawili ya “marefarii”! Hawa “marefarii” huwa kama wadhamini wako katika kile ulichoandika juu yako na juu ya ujuzi ulio nao. Usisahau ya kuwa Yesu ni mdhamini wako. Pamoja na kwamba hujamwandika – lakini unaweza ukaweka mkono wako juu ya barua hiyo, na kuikabidhi kwa Yesu kwa njia ya maombi ili naye afanye kazi ya kukudhamini na ya kukutetea.
Roho aliyemfufua Kristo aliye ndani yako ataingia kazini rasmi kufanya kazi hiyo ya kukudhamini na kukutetea kwa niaba ya Yesu Kristo!
Tunapata uthibitisho wa jambo hili kufanyika kwa kuwa tumetiwa “muhuri” na Roho Mtakatifu mioyoni mwetu, ili iwe ishara ya “udhamini” wake juu ya maisha yetu.
Biblia inasema hivi juu ya hili: “Basi yeye atufanyaye imara pamoja nanyi katika Kristo, na kututia mafuta, ni Mungu, naye ndiye aliyetutia muhuri akatupa arabuni ya Roho mioyoni mwetu” (2 Wakorintho 1:21,22). Unaweza kulipata wazo hili tena ukisoma Waefeso 1:13,14. Neno “arabuni” lina maana ya “udhamini” juu ya hicho kilichotiwa muhuri na Roho Mtakatifu.
Kujua hili kukupe kunufaika na udhamini huu kwenye maeneo mbalimbali ya maisha yako – kama vile masomoni (Danieli 1:17); katika biashara (Isaya 48:17); katika hali ya afya ya mwili wako (Warumi 8:11); katika maongozi ya maamuzi yako ya kila siku (Zaburi 32:8); katika kazi (Daniel 6:4-16); nakadhalika!
Mungu akubariki katika neno hili kwenye maisha yako!

Comments