KAZI YA KUPINDUA ULIMWENGU

Na Frank P. Seth .

"1 Wakiisha kupita kati ya Amfipoli na Apolonia wakafika Thesalonike, ambapo palikuwa na sinagogi la Wayahudi.
2 Na Paulo, kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimo, akahojiana nao kwa maneno ya maandiko sabato tatu,
3 akiyafunua na kuwaeleza ya kwamba ilimpasa Kristo kuteswa, na kufufuka katika wafu; na ya kwamba, Yesu huyu ninayewapasha ninyi habari zake ndiye Kristo.
4 Wengine miongoni mwao wakaamini, wakashikamana na Paulo na Sila; na Wayunani waliomcha Mungu, wengi sana, na wanawake wenye cheo si wachache.
5 Na Wayahudi wakaona wivu, wakajitwalia watu kadha wa kadha katika watu ovyo wasio na sifa njema, nao wakakutanisha mkutano, wakafanya ghasia mjini, wakawaendea watu wa nyumba ya Yasoni, wakataka kuwapeleka mbele ya watu wa mji;
6 na walipowakosa, wakamkokota Yasoni na baadhi ya ndugu mbele ya wakubwa wa mji, wakipiga kelele, wakisema, Watu hawa walioupindua ulimwengu wamefika huku nako,
7 na Yasoni amewakaribisha; na hawa wote wanatenda mambo yaliyo kinyume cha amri za Kaisari, wakisema na kwamba yupo mfalme mwingine, aitwaye Yesu.
8 Wakafadhaisha ule mkutano na wakubwa wa mji walipoyasikia hayo.
9 Nao walipokwisha kumtoza dhamana Yasoni na wenziwe wakawaacha waende zao. "
(Matendo ya Mitume 17:1-9)

Tangu enzi na enzi, KAZI ya KUPINDUA ulimwengu imefanywa na watu wasiotarajiwa tena wasiokubalika kwa VIGEZO vya hao waliojipangia taratibu, kanuni na mizania za vipimo.
Siongelei habari ya KAZI ya huduma tu ila kila kilichoitwa maarifa, elimu na ujuzi.
Nitaanza na KAZI ya huduma.
Ukingalia mageuzi makubwa ya kiimani tangu nyakati za mitume na manabii , utagundua sio wengi sana wasomi waliobobea katika eneo fulani wameleta mageuzi katika eneo hilo. Wapo watu ambao wanaitwa "wapindua ulimwengu". They think outside the box japo wamo kwenye box!

Pale majira ya alasiri, Petro na wenzake wanaingia hekaluni kupitia mlango mzuri, kiwete anaamka. Moja Wapo ya mambo yaliyoibuka ni "elimu" ya Petro. Hajasoma. Ni mvuvi tu!
Akina Marko nao ni mitume lakini kitaaluma ni daktari (tabibu)! Paulo naye anakuja na mambo tufauti kabisa na mitaala ya shule za akina Gamalieli. Wakuu wa mafarisayo! Utasemaje Yesu ni Kristo kwa wayahudi?
Sasa narudi kwenye fani zingine.
Mageuzi makubwa ya computer (wapindua ulimwengu) sio computer scientists! Hata degree moja hawana licha ya PhD! Angalia akina Bill Gates, Steve Jobs, na wenzake. Vinara katika maswala ya computer ..hao elimu yao ilikuwa ya sekondari tu wakati wanapindua ulimwengu!

Nina mifano mingi hadi siwezi kuandika.
USHAURI
1.Ukisubiri mpaka ukasome degree ya kilimo SUA ili uje kulima na kusindika bidhaa za kilimo...ukirudi mtaani utagundua waliopindua ulimwengu kwenye mashamba na usindikaji kuna Mohamed Enterprise, Azam Bakresa na wengine. ..wote hawajasomea kilimo.
2. Ukisubiri upate degree ya kufuga kuku ndio uanze. Kweli utaanza ila kupindua ulimwengu huhitaji sana hiyo degree. Mimi ni mtu wa taaluma na nimeenda shule lakini naheshimu wapindua ulimwengu ambao hawajasoma kuliko maprofesa wangu. Nina listi ya majina ya wapindua ulimwengu hapa Tanzania waliovuka mpaka ya taaluma zao na wanakulisha kuku na mayai hujajua tu.
3. Walioandika vitabu vingi sana sio wataalamu wa lugha kwa kusomea. Na Waliyoandika mengi yao hawana cheti kwamba wamesomea hayo mambo. Hao nao wamepindua ulimwengu!
4. Ninafahamu washauri wa mambo ya biashara, ujasiriamali, mahusiano, ndoa, nk. Waulize vyeti vyao kwenye hayo mambo wanayofundisha watu kwa maelf elf. Wengi wao hawana. Je! Watu hawafanikiwi kwa kuwasikiliza? Je! Hao nao hawakupindua ulimwengu?
ANGALIZO
1. Ukianza shughuli ya kupindua ulimwengu, utakatishwa tamaa na wale wa "taaluma". Wakija na kanuni zao na vipimo vya kukuonesha umepungua. Songa mbele. Usiwasikilize kwa maana wivu unawaka ndani yao kama moto.
2. Usipuuzie ushauri wa kitaalamu kama ukihitajika. Soma vitabu na majarida kujiongezea maarifa.
3. Mtaji sio kikwazo. Wewe ndio kikwazo cha kwanza.
Frank P. Seth .

Comments