KAZI ZA ROHO MTAKATIFU

Na Mtumishi Nickson Mabena
Kazi za Roho Mtakatifu zipo nyingi sana,
Mimi nataka nizungumzie baadhi ya kazi hizo, ambapo kwa namna nyingine naweza nikaziita FAIDA ZA ROHO MTAKATU..
Kanisa lolote linalotaka kufanikiwa, lanalotaka kushinda, linalotaka kumuona Mungu akitenda kazi, lazima litambue uwepo wa Roho Mtakatifu,
Ukimkataa Roho Mtakatifu, umekataa kazi zake, na hutakuja kuona faida ya kuwa na Mungu kwenye maisha yako,
Naposema Kanisa namaanisha, Mtu aliyeokoka, lakini Pia namaanisha Watu wanaomwabudu Mungu pamoja,
KAZI/FAIDA ZA KUWA NA ROHO MTAKATIFU.
1.ROHO MTAKATIFU HULETA NGUVU.
Nguvu ya Mungu, inapatikana kwa Roho Mtakatifu,
Yesu alisema, "Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyitakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi." MDO 1:8
Ni wazi kwamba, Roho Mtakatifu, anazo nguvu, lakini yeye sio nguvu,
Ukisema Roho Mtakatifu ni nguvu, utakua unakosea, kwa sababu, Roho Mtakatifu ni nafsi hai, ni Mungu, sio 'kitu',
Ni Mungu mwenye Nguvu,
Yesu amesema, akiisha kutujilia Roho Mtakatifu, tutapokea Nguvu,
Kanisa linalotaka kushinda, lazima liwe na nguvu za Mungu,
Mkristo anayetaka kusonga mbele lazima awe na Nguvu za Roho Mtakatifu,
Mungu alishatuambia, tusimuhitaji yeye peke yake, bali tumuhitaji yeye na Nguvu zake!.
"Mtakeni BWANA na nguvu zake, Utafuteni uso wake sikuzote" ZAB 105:4,
Nguvu zake zipo kwa Roho Mtakatifu,
Ujue, zipo faida pia nyingi tu za kuwa na hizi nguvu za Roho Mtakatifu,
Ngoja nikutajie baadhi, zingine utazitafuta,
👉Nguvu za Roho Mtakatifu ni ulinzi.
"Mtu *mwenye nguvu* aliyejifunga silaha zake, alindapo nyumba yake, vitu vyake vi salama;" LUKA 11:21
Umeona?,
Ukiwa na NGUVU za Roho Mtakatifu, vitu vyako ni salama,
Lakini kinyume chake, ni Kweli,
Angalia Mstari unaofuata wa sura hiyo,
Unasema, "lakini mtu mwenye nguvu kuliko yeye atakapomuendea na kumshinda, amnyang'anya silaha zake zote alizokua akizitegemea, na kuyagawanya mateka yake" LUKA 11:22
Ujue ipo hivi,
Shetani anazo nguvu, Mtu anazo nguvu, Mungu anazo nguvu,
Shetani anazo nguvu kuliko Mtu, lakini Mungu ana nguvu kuliko Shetani, na ana nguvu kuliko Mtu,
Kwa hiyo, Mtu hawezi kumshinda Shetani kwa nguvu zake mwenyewe,
Kama akihitaji kumshimda Shetani, anazihitaji Nguvu za Mungu.
Ndio maana Yesu alisema, LAKINI MTU MWENYE NGUVU KULIKO YEYE, AKIMWENDEA NA KUMSHINDA.....
Ni wazi Shetani akikufuata, akakushinda, Ujue ananguvu kuliko wewe,
Kwa sababu hiyo, unazihitaji nguvu za Roho Mtakatifu za kutosha,

Ukiwa na nguvu za Roho Mtakatifu za Kutosha, ULINDAPO NYUMBA YAKO, VITU VYAKO NI SALAMA!!!!.
👉Nguvu za Roho Mtakatifu huzaa/huzalisha.
Nguvu hizi, zinauwezo wa kuzaa kitu kipya, zima uwezo wa kuzalisha,
Mariamu wakati anapewa ujumbe wa kupata Mtoto, alimuuliza swali Malaika, "Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijui mume?" LUKA 1:34
Mariamu, alikua anajua kwamba kwa kawaida, ili azaliwe mtoto, lazima ajue mume,
Nalipenda sana Jibu la Malaika, "Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na *nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli*; kwa sababu hiyo kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu" LUKA 1:35,
Bila Shaka kuna picha umuiona hapo ndani,
Nguvu zake aliye juu, ni Nguvu za Roho Mtakatifu,
Zilipomfunika Mariamu, kikazaliwa kitakatifu, kilichotengwa kwa kusudi maalumu, kinachofaa,
Hata kwako, Nguvu za Roho Mtakatifu zikikufunika, kitu kipya kitazaliwa!!!.
Zikikufunika, tabia njema, vitu vya ki-Mungu vitazaliwa!!!.
👉Nguvu za Roho Mtakatifu zinaweza kuponya.
Mwanamke aliyetokwa na damu, alipogusa vazi la Yesu, alipokea uponyaji,
Wengi hawakuelewa kwenye ule Mkutano kwamba kuna Mtu amepona, kwa kumgusa Yesu,
Yesu alielewa, ndio maana akauliza, "Ni nani aliyenigusa?" (LUKA 8:45)
Wao walidhani anaulizia kuguswa kwa kawaida,
Lakini Yesu akasema, "Mtu alinigusa, maana naona ya kuwa *nguvu zimenitoka*" LUKA 8:46
Nguvu za Roho Mtakatifu, zilimtoka Yesu, na kwenda Kumponya yule Mwanamke aliyetokwa na damu!!.
Nguvu hizi, zinaweza kuponya pia udhaifu wako!!!.
Hizi ni baadhi tu, ya faida za nguvu za Mungu,
Faida zungine, nitazielezea kwenye Kazi zingine za Roho Mtakatifu,
Hadi hapo naamini kwamba Umeona kwamba, una sababu ya Kuzitafuta Nguvu za Roho Mtakatufu,
Unaona sababu za Kanisa kuwa na Nguvu za Roho Mtakatifu!.
Tukikosa nguvu hizi, tunakua na kanisa LILILOPOAAA!!.
Ukiona nguvu zimepungua, zitafute, ziongezeke!!
.......Naomba, niishie hapo,
Nitaendelea, na Kazi zingine za Roho Mtakatifu!!.
Naitwa Mwalm Nick,
0712265856
(WhatsApp#)

Comments