Apostle Maboya Awashauri wahubiri nchini

Apostle Maboya
Ninawashauri wahubiri ukiona mambo yako hayajanyooka usihubiri mambo ya mafanikio, hubiri uaminifu ili watu wa-“Take serious”. Wanataka kuhubiri mafanikio tu wakati kuna mambo mengi ya kuhubiri. Msichukue meseji za watu na kuanza kuhubiri. Unaona mtu kanunua gari na wewe unasema, “Kwa mbinde zozote nitanunua gari”, nakuambia utapoteza muujiza wako. Mungu atakubariki kwa wakati wake. Ndio maana hata Isaka alimuuliza mwanae Yakobo, “Mbona umewahi umeleta mboga hii mapema?” Kwasababu alielewa uhitaji ni kazi ya kukesha. Lakini unaona mtu dakika kumi jambo alilotaka limekuja na ukimuuliza anasema, “Bwana ameniandalia”.
Unapoona mtu anahubiri usichukue tu mahubiri angalia na hali yake kama inafanana na acho hubiri. Watumishi wengine wana-“copy” mahubiri, na wengine wanachukua mahubiri ya akina Oyedepo kwasababu mahubiri yao ni “Wisdom” Anavyokuhubiria kuwa unakwenda kutajirika unaangalia na viatu vyake na anapokaa, Jamani hata macho huoni.
Watu wengi sana wanapata vitu kiulani na kuwadanganya watu kwasababu wanalegeza maandiko ya Mungu kupitia Biblia. Kwasababu Isaka alipokuwa akimshika Yakobo akasema, “Mwili huu ni wa Esau lakini sauti ya Yakobo”, alionyesha kushtuka. Halafu Yakobo akamchapa andiko, “Bwana ameniandalia na amenifanikisha”.
Ni lazima uwe muangalifu kwasababu kuna watu wanajificha kwa jina la Bwana, na ndio maana Mungu amekutaka wewe usikie sauti ya mchungaji. Hata kama mtu atasema nimeonyeshwa na Bwana na kuna mapigo yatatokea nyumbani kwako, toa sadaka hii usikubali kwani Mungu hawezi kuonyesha kwa Baba wa kambo wakati una baba mzazi.
Kila kanisani huwa na mpangilio wake, kila “jeans” lina mguu wake, sasa kwanini taarifa yako iende nyumba ya jirani na mama yako asijue, na wakati Mungu amempa nguvu ya kulivuta kundi? Basi unapopata meseji za watu wa namna hii ujue hizo meseji ni feki. Mungu hawezi kuleta meseji za kukuua wewe, ukiona hivyo ujue hiyo meseji feki. Kwasababu Mungu anafuata ile neema “inoder” jambo la aina yoyote lazima lifike, na likifika hata lingekuwa ni gumu kiasi gani, wazo la mchungaji atakalolitoa lazima limalize shida hiyo, kwasababu Mungu anamtumia mchungaji wako kama wakili wako wewe.


Sasa hizi nyota zinawafanya watu wengi waumie, lakini mimi nisema, “ Kuanzia sasa uangalie nyota ya asubuhi” Nabii yoyote akikuletea ujumbe wowote uwe wa kufa usipinge lakini uchukue na upeleke kwa mchungaji wako. Unajua watu wanakwenda na “seniority”. Kwamfano atakapotokea kijana yoyote akakutabiria kitu ovyo, na kikakuumiza moyo wako, na akataka ku-“comfirm” , na akatokea mchungaji wako akasema sio, basi amini sio. Mungu anaangalia “Senior between that person and your pastor”.
Kuna agano la Rehema ambalo linasemama juu yako, utakapo kuwa umefanya kosa kwa bahati mbaya, angano la rehema linakulinda. Utakapoingia katika misukosuko ya kukuletea hatari agano la rehema linakulinda. Mungu akakupe rehema ndani yako, ndoa yako, maisha yako, mipango yako. Kwa miezi hii sita Bwana akaangalie agano la rehema.
Katika amri za Mungu tunapenda ile amri ya kwanza naya pili. Mimi ndimi Mungu wako usiabudu miungu mingine, lakini kuna amri ya nane, tisa na kumi. Ninachotaka kusema ni kwamba Mungu atakupenda, atakukaribia na atakupongeza. Ninachotaka kukutia moyo ni kwamba lazima ufanye kazi na utajirikie ili ukifika mbinguni useme kweli duniani nilifaidika na mbinguni nafaidika, sio wewe uteseke duniani na mwisho wa siku mbinguni nako usikuone au ukuone. Ninachotaka kusema unaweza kuwa maskini duniani na mbingu ukafika kama alivyokuwa Lazaro.

Comments