ASKOFU GWAJIMA AMESHARUDI NCHINI NA JANA ALIHUBIRI KANISANI KWAKE IKO VIDEO HAPO CHINI WAKATI ASKOFU AKIHUBIRI.

Askofu Wa Kanisa la Ufufuo na uzima Dr Josephat Gwajima akihubiri jana kanisani kwake baada ya kurejea kutoka nje ya nchi.
Askofu Dr Josephat Gwajima amewasili leo kutoka Barani Asia ambapo alifanya mikutano zaidi ya kumi ya injili miji tofauti tofauti. Baada ya kurudi amehubiri jioni hii kanisani Ufufuo na Uzima, Ubungo Dar es Salaam ambapo ameongea kwa habari ya Ramani ya Vita.
Katika somo Hilo Askofu, ametumia kitabu cha Esta akionyesha jinsi ambavyo Modekai na Wana wa Israel walitengenezewa mchoro wa vita ili kuwaangamiza lakini Mungu aliwaweka adui zao kwenye mchoro badala ya waisrael. Pamoja na somo Hilo, Askofu Dr Gwajima amewaombea watu waliokuwa na matatizo mbalimbali na kuponya wagonjwa.
Mungu amekuwa mwaminifu kwetu.
Imetolewa na David Mgongolwa
Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano
Ufufuo na Uzima. Makao Makuu.


Katika Ukurasa wake wa Facebook, Askofu Gwajima alisema baada ya mahubiri kwamba 
''Jana 11/07/2016, nilipata nafasi ya Kuhubiri kanisani Ufufuo na Uzima, Ubungo, Dar es Salaam. Mungu amekuwa mwaminifu tena.   ''

Hapa chini ni video ikionyesha sehemu ya mahubiri hayo ja jana jioni.

Comments