FAIDA KUMI(10) ZA MAOMBI YA KUFUNGA.

Na Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.

BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze kuhusu maombi ya kufunga.
Kufunga Ni Utii Wa Kujitoa Kwa Ajili Ya BWANA MUNGU, Ili Kwamba,  MUNGU Aweze Kutenda Kupitia Wewe Yale Ambayo Asingeweza Kutenda Kama Usingefunga. 
Maombi Ni Mawasiliano Ili BWANA YESU Atende Kwako Yale Ambayo Yasingetendeka Kama Usingeomba. 
Kutoa Matoleo Ni Utii Unaosafisha Mfereji Ili BWANA Apate Kutenda Makuu Kwako. 
Maombi ya kufunga ni muhimu sana katika maisha ya wakristo.
Wakristo hawafungi mara moja kwa mwaka, bali inawezekana kabisa mkristo anaweza kufunga hata mara 100 kwa mwaka, na ndio wengi walioshinda wanavyofanya.
 Mathayo 6:16-22 ''Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso; ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi. Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba; bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi; kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako. Taa ya mwili ni jicho; basi jicho lako likiwa safi, mwili wako wote utakuwa na nuru. ''

Maombi ya kufunga ni muhimu sana kwako ila hakikisha hufungi ili kuwaridhisha watu fulani.
Usifunge ili uonekane wa kiroho bali funga ili ujibiwe mahitaji yako.
Usifunge ili kuwaonyeshea watu.
Maombi mazuri pia ni lazima yaambatane na utakatifu.
Maombi mazuri pia ni muhimu yakaambatana na utoaji.


Watu Wengi Hutaka MUNGU Awabariki Kiuchumi Huku Utakatifu Kwao Ni 0.001% Yaani Wana Utakatifu Wa Ndani Ya Ibada Tu, Wakitoka Ibadani Wanaendelea Kuwa Watoto Wa Shetani. 
Ndugu, Hata Kama Ukivipata Vyote Uvitakavyo Lakini Kama Utakufa Dhambini Ni Hasara Kwako.
Hivyo jambo muhimu zaidi ni utakatifu kisha maombi.

 1 Petro 1:15 '' bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;''


 Kufunga ni jambo la muhimu sana maana lina faida kuu kwa anayefunga.
Wakristo wote wanatakiwa kuwa watu wa maombi yakiwemo maombi ya kufunga.
Kufunga Sio Karama Hata Useme Huwezi Kufunga kwa kisingizio kwamba kufunga Sio Karama Yako. 
Kufunga Hakumo Ndani Ya Karama Za MUNGU Kwetu bali ni agizo jema kwetu.
 Maombi Ya Kufunga Ni Kufungua Pale Pasipoweza Kufunguliwa Kwa Njia Ya Kawaida. 
Ndugu, Usiache Kufunga Kwa Madai Kwamba Huna Karama Ya Kufunga.

1 Thesalonike 5:17 ''ombeni bila kukoma;''

Kuna faida kuu katika maombi ya kufunga.
Ni Kweli  wakati huu kwako Unaweza Kuwa Ni Wakati Wa Ukame, Lakini Mvua Ya Baraka Itanyesha Hivi Punde baada ya kuomba kwa imani maombi ya kufunga.
Hata Kama Kulikuwa Na Ukame Kiuchumi Kwa Muda Mrefu Lakini Kwa Kumwita BWANA YESU Hakika Mvua Ya Baraka Inaenda Kunyesha. 
Maombi Ni Maisha. 
Maombi ya kufunga Ni Mkono Mrefu zaidi Wa Kupokea kutoka kwa MUNGU. 
Biblia Inasema Kama Huombi Wewe Huna Hitaji. Kwa YESU Tunaomba Na Kupokea.

''Matofali Yameanguka, Lakini Sisi tutajenga Kwa Mawe Yaliyochongwa; Mikuyu Imekatwa Lakini Sisi Tutaweka Mierezi Badala Yake.-Isaya 9:10.
 Nampenda YESU Maana Anatengeneza Vitu Imara Zaidi Kuliko Nilivyowaza. Nampenda YESU Maana Yeye Ataleta Baraka Ambayo Ni Imara Na Ya Kudumu, lakini kama tu tukidumu katika utakatifu pamoja na kudumu katika maombi yakiwemo na maombi ya kufunga.


 ''Utafichwa Na Mapigo Ya Ulimi; Wala Usiogope Maangamizo Yatakapokuja-Ayubu 5:21''. 
 Ndugu, Kuna Mapigo Ya Ulimi Yanaelekezwa Kwako wakati mwingine, Mapigo Hayo Ni Maneno Mabaya Unayonenewa Na Watu Wabaya. Wanakunenea Magonjwa, Wengine Kwa Vinywa Vyao Wanataka Usipokee Baraka Yako. 
Mpendwa, Ulimi Una Mapigo Na Unapiga Ndio Biblia Inavyosema Hapo Juu. Nakuomba Uombe Leo Juu Ya Hili, Yapeleke Golgotha Maneno Mabaya Uliyonenewa Na Kupangiwa Na Watu Wabaya, Urudi Ukiwa Huru. 
Fanya maombi yako kwa imani na kwa kufunga na kuomba.



FAIDA 10 ZA MAOMBI YA KUFUNGA KULINGANA NA MATHAYO 17:21.

1. Kufunga kunasaidia kukua kiroho.

Mathayo 17:21 ''Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.''

Inawezekana kabisa umekuwa ni mtu wa kudumaa tu kiroho, umejitahidi kwa nguvu zako na akili zako ili ukue kiroho lakini umeshindwa. Neno la MUNGU linasema kwamba mengine huwa yanawezekana tu pale ambapo wewe utakuwa unafunga na kuomba. Tatizo la uchanga wa kiroho linaweza likatoka tu kwako pale ambapo utakuwa unafunga na kuomba na utakatifu.

2. Kufunga kunakufanya uwe msikivu zaidi wa kuisikia sauti ya MUNGU.


Mathayo 17:21 ''Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.''

Kuna watu ni ngumu kwao kuisikiliza sauti ya MUNGU.
Kuna watu makali yao ya rohoni hayajanolewa hata waweze kuwa wanaona mambo makubwa ya ki-MUNGU.
Tatizo kama hilo wakati mwingine litaondoka baada ya wewe kuwa unafunga na kuomba.
Tatizo halitaondoka kwako wakati mwingine mpaka kwa kufunga na kuomba.
 

3. Kufunga kunakusaidia kuutiisha mwili wako.

Mathayo 17:21 ''Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.''

Japokuwa maombi yana nguvu sana lakini naomba ujue kwamba maombi ya kufunga yana nguvu mara saba zaidi.
Kuna watu miili yao  inawatumikisha katika dhambi.
Kuna wanaume akiona tu sura ya mwanamke basi hawezi kujizuia kumtongoza, ni pepo hilo lakini kwa maombi ya kufunga na utakatifu hakika pepo hilo litaondoka.
Kama mwili wako unakusumbua katika dhambi mbali mbali kama uzinzi, uongo, tamaa mbaya n.k nakuomba anza kuwa mtu wa kufunga na kuomba maana mwili wako sasa utaenda kuitii roho yako. Mwili ni dhaifu sana lakini maombi ya kufunga yanaweza kuutiisha mwili wako hata usiweze kukuwashawasha tena pindi uonapo mtu wa jinsia tofauti na yako.
 
5. Kufunga husababisha ushindi kwako dhidi ya ngome za shetani.


Mathayo 17:21 ''Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.''

Kuna ngome zingine za adui kuzibomoa kunahitajika nguvu kubwa sana ya MUNGU.
Inawezekana unashindana na wachawi.
Inawezekana unashindana na mwanamke alikuendea kwa waganga ili tu akunyang'anye mume wako wa ndoa.
Inawezekana kuna mtu anakuroga ili ufukuzwe kazi.
Inawezekana kuna mganga amekufunga ufahamu wako hata hujielewi.
Inawezekana kabisa unapambana na mizimu au majini.
Ndugu yangu, yote hayo au moja katika hayo na mengine mengi unayoyajua mwenyewe, ili kuyashinda kunahitajika nguvu kubwa zaidi. Mengine hayawezi yakatoka hadi baada ya wewe kufunga na kuomba, ndivyo Biblia inavyosema hapo juu kwamba mengine hutoka tu hadi pale utakapofunga na kuomba.

6. Kufunga kunakuongezea mamlaka ya kiroho.

Mathayo 17:21 ''Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.''

Wenye nguvu nyingi za rohoni ni wale waliokaaa katika kusudi la MUNGU.
Wenye nguvu nyingi za rohoni ni wale waombaji, wanaoomba kwa imani na kufunga pamoja na utakatifu.
Kama unataka kuongeza mamlaka yako kiroho katika BWANA YESU hakika pia unatakiwa kuongeza maombi ya kufunga pamoja na utakatifu sana na kujifunza Neno la MUNGU na kulishika.

7. Kufunga kunakupa nguvu mpya ya kiroho.

Mathayo 17:21 ''Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.''

Nilipojua siri hii nilifanikiwa sana kiroho.
Kuna wachungaji wengi leo hata huwatumihumu wachungaji wenzao kwa sababu wanaombea watu wanapona lakini wao hawawezi, kumbe tatizo  ni kupungukiwa na maombi ya kufunga na utakatifu.
Nguvu mpya rohoni zinaweza kuja kwako baada ya maombi ya kufunga na kuomba na utakatifu.

8. Kimwili:Kufunga kunasababisha uponyaji wa wa mwili 

Mathayo 17:21 ''Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.''

 - Hata katika maombi ya kimwili, kufunga kuna faida sana. Kufunga kunaweza kukuasaidia kupunguza mafuta mwilini yasiyohitajika, yanayoweza kukuletea magonjwa n.k
-Kufunga kunaweza kukusaidia kuondoa uchafu katika mwili wako.

9. Kimwili: Kufunga kunaweza kukusaidia kuepuka kifungo cha ulafi.

Mathayo 17:21 ''Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.''

-Ulafi sio jambo zuri hata kidogo.
-Biblia inaataza wakristo kuwa walafi.
-Njia mojawapo ya kuusaidia mwili wako kuepukana na ulafi ni kufunga.
 Baada ya maombi ya kufunga  tumbo hupungua na chakula unaweza kuwa unakula kidogo tu na kushiba, hiyo ni faida nzuri ya maombi katika mwili wako.
 

10. Kufunga kutakupa faida ya kiroho, kimwili na kiakili(Nafsi)

Mathayo 17:21 ''Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.''

-Faida kubwa kabisa ya maombi ya kufunga ni kupokea hitaji lako. Baada ya kupokea hitaji lako hakika utakuwa safi kiroho na kiakili maana tatizo limeondoka.
-Faida ya kiroho inajumuisha mambo mengi sana ambayo yote ni muhimu sana kwa muombaji.

Naomba BWANA YESU Awe Yote, Tumtegemee Na Kuomba.
Tulitii Neno La MUNGU Na Kuenenda Kwa ROHO MTAKATIFU. Usijitenge Na Wokovu Wa YESU Maana Kujitenga Na YESU Ni Kujitenga Na Uzima Wa Mikele. BWANA Yuaja.
Ndugu jiokoe na kizazi hiki chenye ukaidi.
BWANA YESU anakungoja sasa ili uamue vyema leo.
Ubarikiwe sana.Nakuomba pia nisaidie kuwasambazia na wengine ujumbe huu.
Ni mimi ndugu yako Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
Mabula1986@gmail.com
+255714252292.

Comments