KANISA LA KRISTO HUONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU.

Na Mtumishi Peter Mabula

BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno hai la MUNGU aliye hai.

 ''Bali wote waliompokea(YESU) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa MUNGU.-Yohana 1:12-13'' 

Kanisa ni watu waliompokea YESU KRISTO kama BWANA na Mwokozi wao. Mwokozi wa kanisa ni YESU KRISTO.
Wajibu wa kanisa ni kuishi maisha matakatifu na kushuhudia walio nje kuhusu injili ya KRISTO inayookoa.
Msimamizi wa kanisa ni ROHO MTAKATIFU.
Kanisa hasa sio jengo bali ni mtu binafsi aliyeamua kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wake.
Kanisa lolote likijitenga na YESU KRISTO hilo linahama kutoka kuwa kanisa la MUNGU na kuwa kanisa la shetani.
Kanisa lolote litakalomkataa ROHO MTAKATIFU hilo linakuwa kanisa la kidini na sio kanisa hai la MUNGU. 

Warumi 8:14 ''Kwa kuwa wote wanaoongozwa na ROHO wa MUNGU, hao ndio wana wa MUNGU.''

Huwezi Kuwatenganisha YESU KRISTO Na ROHO MTAKATIFU Hata Siku Moja. Kuna Madhehebu Wanaamini Katika YESU KRISTO Lakini Hawamwamini Wala Kumhitaji ROHO MTAKATIFU. Huo Ni Uchanga Wa Kiroho Wa Level Ya Mwisho Kabisa. Haiwezekani Mtu Kumpokea Na Kumtii YESU KRISTO Harafu Mtu Huyo huyo Asikubali Kumpokea ROHO MTAKATIFU.
 Kama Mtu Atamkataa ROHO MTAKATIFU Atabaki Pia Akiwa Hamjui Kwa Usahihi YESU KRISTO. 
 Biblia Iko Wazi Sana Ikisema Kwamba "Haiwezekani Mtu Kusema Kwamba YESU Ni BWANA Isipokuwa Katika ROHO MTAKATIFU- 1 Kor 12:3".

 Wakristo Au Wasio Wakristo Wanaomkataa ROHO MTAKATIFU Ndio Wale Ambao Husema Kwamba "Yesu Ni Mtu Tu, Yesu Ni Nabii Tu, Yesu Ni Malaika Mikaeli Tu, Yesu Ni Mtoto Wa Maria Hadi Leo, Yesu Ni Mtume Tu, Yesu Ni Mtoto Wa Seremala Tu N.k". 
Hawa Hawajamjua Bado BWANA YESU Ni Nani Kwa Sababu Hawana ROHO MTAKATIFU. Ubarikiwe wewe ambaye unapata Ufahamu Huu Muda Huu  niliopewa Nikujulishe.

 Mkristo Ni Yule Anayeongozwa Na ROHO MTAKATIFU. 
Asiye Na ROHO MTAKATIFU Huyo Sio Mkristo Ndivyo Biblia Inavyosema Katika Warumi Sura Ya 8:9

 ''Lakini ikiwa ROHO wa MUNGU anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na ROHO wa KRISTO, huyo si wake-Warumi 8:9".

Kama huna ROHO wa KRISTO ambaye ndiye ROHO MTAKATIFU wewe sio wake KRISTO.
ROHO wa KRISTO huingia ndani ya mtu pale mtu huyo anapoamua kuokoka. Kama mtu huyo akiuacha wokovu wa KRISTO na kurudia mambo ya dhambi, ROHO wa KRISTO huondoka kwa mtu huyo.
Wenye ROHO MTAKATIFU Tu Ndio Watoto Wa MUNGU Ndivyo Biblia Inavyosema Katika Warumi Sura Ya Nane ule mstari wa tisa. 
 Je Wewe Una ROHO MTAKATIFU?
Kuna tofauti ya kuwa na ROHO MTAKATIFU na kufurika ROHO MTAKATIFU.
 Lakini pia Kuna Viwango 3 Vya Ujazo Wa ROHO MTAKATIFU Ndani Ya Wateule. 
=Kuna Kubatizwa Kwa ROHO MTAKATIFU.
1 Kor 12:13 '' Kwa maana katika ROHO mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa ROHO mmoja.''
= Kuna Kujazwa Endelevu 
Waefeso 5:18 ''Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe ROHO;''
= Kuna Kutiwa Mafuta Na ROHO MTAKATIFU. 
 1 Samweli 16:13  “Ndipo samweli akaitwaa pembe yenye mafuta, akamtia  mafuta kati ya ndugu zake; na ROHO ya BWANA akamshukia Daudi kwa nguvu tangu siku ile
 
Hivyo Kuna Wakristo Wamebatizwa Kwa ROHO Ila Hawajafikia Viwango Vingine. 
Ninachotaka Ni Nini?. 
Ndugu Mtake Sana ROHO MTAKATIFU Na Nguvu Zake, Na Karama Zake Na Matunda Yake. 
Kama Kanisani Kwenu Wanamkataa ROHO MTAKATIFU Ni Heri Kuhama Huko na  Kuhamia Kanisa La Kiroho Linaloamini Katika ROHO MTAKATIFU. 
Je Utashindaje Ya Dunia Kama Huna ROHO MTAKATIFU? 
Ndio Maana Nakuletea ujumbe huu leo  Usome Utaelewa Kwamba Bila ROHO MTAKATIFU Ni Hasara Kuu.

 Kanisa La KRISTO Huongozwa Na ROHO MTAKATIFU Lakini Kanisa La Kibinadamu Huongozwa Na Tamaa Za Viongozi Wa Kanisa, Huo ndio utofauti katika makanisa.

ROHO MTAKATIFU hufunua siri zote hivyo ukiwa naye wewe uko sehemu salama labda tu usimtii ROHO.
Ufunuo wowote uliotolewa na mizimu ni machukizo mbele za MUNGU haijalishi kama ni ufunuo mzuri au mbaya.
Hayo yanawatesa wengi kwa sababu tu hawana ROHO MTAKATIFU.
Sio kila mtumishi ameitwa, wengine wamejiita ndio maana anaweza hata akatumia mizimu katika utumishi wake. Lakini akiwapo ROHO wa MUNGU ya shetani yatajulikana tu.

 ROHO MTAKATIFU Ndiye Mtawala Wa Kanisa Halisi La KRISTO. 
Kanisa Lolote Lisilo Na ROHO MTAKATIFU Ni Vigumu Kufanya Yaliyo Ya MUNGU. 
Wakristo Wote Wanatakiwa Wawe Na ROHO MTAKATIFU, Wakristo Halisi Ni Nyumba Ya Kukaa ROHO MTAKATIFU Ndivyo Biblia Inavyofundisha.
  ''Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la ROHO MTAKATIFU aliye ndani yenu, mliyepewa na MUNGU? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni MUNGU katika miili yenu.-1 Kor 6:19-20''

 ROHO MTAKATIFU hutoa karama zake kwa wateule wa KRISTO lakini nataka niseme jambo juu ya karama ya kunena kwa lugha ambayo kuna watu huenda tofauti.
 Kunena Kwa Lugha Sio Ishara Ya Mtu Kukua Kiroho Kuliko Wengine Wala Kunena Kwa Lugha Sio Ishara Ya Mtu Kwamba Yuko Juu Kiroho Kuliko Alivyokuwa Kabla.
 Kunena Kwa Lugha Ni Jambo Muhimu Sana Kwa Mteule Wa KRISTO Lakini Tukio Hilo Takatifu Sana Listafasiriwe Vibaya. Kunena Kwa Lugha Wakati Mwingine Ni Karama Ya ROHO MTAKATIFU Lakini Pia Kunena Kwa Lugha Ni Ahadi Ya MUNGU Kwa Waamini Wa Kweli. Tamani Kunena Kwa Lugha Ila Ukifanikiwa Kunena Usijipandishe Kiroho Kuliko Mchungaji Wako Au Waumini Wenzako. Binafsi Mimi Hunena  Lakini Hiyo Hainifanyi Kuwadharau Wengine.

Yohana 14:15-17  '' Mkinipenda, mtazishika amri zangu. Nami nitamwomba BABA, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; ndiye ROHO wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.''

ROHO MTAKATIFU ni muhimu sana katika kanisa.
Tukimtii ROHO MTAKATIFU  tutakuwa tunatimiza kusudi la MUNGU.
Ukiona Viongozi Wa Kanisa Wamekosana Na Kuwa Makundi  mawili tofauti Tambua Tu Kwamba Hapo Kuna Nuru Na Giza. Nuru Na Giza Havichangamani Na Vimepingana 

 Wagalatia 5:16-17 ''Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.''.

 Waambieni Waliogeuka Giza Waache Ugiza Wao Na Waungane Na Nuru Ili Wamtumikia MUNGU Aliye Hai Kwa Pamoja.

 Mkitaka Kuchagua Viongozi Kanisani Kwenu Chagueni Wenye ROHO MTAKATIFU, Wenye Hekima Na Wema Ndivyo Matendo 6:3 Inavyofundisha. '' Basi ndugu, chagueni watu saba miongoni mwenu, walioshuhudiwa kuwa wema, wenye kujawa na ROHO, na hekima, ili tuwaweke juu ya jambo hili;''

 Jambo jingine ni kwamba Karama Ya Uponyaji Hupatikana Katika Kanisa Ambalo Ni Mwili Wa KRISTO. Karama Ya Uponyaji Haikufungiwa Kwenye Droo Za Kabati La Dhehebu Fulani Tu Hata Walio Nje Na Dhehebu Hilo Wasiweze Kuombea Watu Wakapona. Ni Kweli Kabisa Kwamba Watumishi Huzidiana Imani Lakini Maombi Kwa Kina Na Utakatifu Hufanya Karama Za ROHO MTAKATIFU Kufanyika Kwa Usahihi. Ndugu Zangu Katika KRISTO, Naomba Tujue Kwamba Maombi, Imani Na Utakatifu Ndivyo Vichocheo Vya Karama Ya Uponyaji Na Nyingine Kufanya Kazi.
 Kama ulikua hujui naomba ujue kwamba KANISA LA KRISTO HUONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU.
 Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichaka chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili.

Comments