KANISA LA UFUFUO NA UZIMA LAKEMEA UZUSHI WA KUFUTIWA USAJILI.

 
Askofu Mkuu wa Ufufuo na Uzima, Dr Josephat Gwajima.



TAARIFA SAHIHI KUHUSU KANISA LA GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH maarufu kama UFUFUO NA UZIMA.
 
Kumekuwa na taarifa zinazozunguka katika mitandao ya kijamii kuhusu kufutiwa usajili wa kanisa la Glory of Christ Tanzania maarufu kama Ufufuo na Uzima. Taarifa hizo SI ZA KWELI, zenye lengo la Kupotosha na zipuuzwe na watu wote. 

Kanisa kama taasisi hatujapokea barua yoyote ya kuhusu kufutiwa usajili. Ni kosa kisheria kwa mtu kusambaza taarifa zisizo sahihi hivyo, tunawaomba watu wote kuzipuuza taarifa hizo zisizo na tija kwa Ustawi wa Taifa Letu. 

Pia, toa taarifa kwa vyombo vya sheria iwapo mtu atakutumia uzushi na uongo huo.
Imetolewa na David Mgongolwa
Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano,
GCTC, Makao Makuu.
12 Julai 2016.


Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano wa kanisa la Ufufuo na uzima, Mchungaji David Mgongolwa

Comments