Na Peter Mabula. Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU. |
BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU aliye hai.
Leo nazungumzia maombi.
Maombi ni mahitaji anayopeleka Mkristo mbele za MUNGU wake.
Kila mmoja ana hitaji lake au mahitaji yake.
MUNGU hujibu maombi na huwapenda wanamaombi maana hao huonyesha kumtegemea MUNGU na sio akili zao, ndio maana wanaomba kwake.
Katika maombi naomba tujue mambo yafuatayo.
=Ni Lazima Tumwombe MUNGU Katika Jina La YESU KRISTO.
Yohana 14:13-14 ''Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili BABA atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.''
= Tena Ni Muhimu Tuombe Katika ROHO MTAKATIFU.
Waefeso 6:18 '' kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika ROHO, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote; ''
-Kuomba katika ROHO MTAKATIFU kuna maana mbili;
1. Kunena kwa lugha.
2. Kuomba kwa kufuata maongozo ya ROHO MTAKATFU aliye ndani yako.
Mfano kuna kipindi nilifunga siku tatu. katika hizo siku tatu niliorodhesha maombi mengi ya kuombea lakini nilipoanza tu kufunga sikuombea ombi hata moja katika yale niliyokuwa nimeyaandika katika notebook yangu, maana wakati wa kuomba nilikuwa napata maelekezo mapya na watu wapya wa kuombea hadi siku 3 zikaisha bila kugusia hitaji langu. Lakini hiyo haina maana kwamba MUNGU hakunijibu bali alinijibu.
=Lakini Pia Ni Muhimu Kuomba Kwa Akili.
1 Kor 14:15 '' Imekuwaje, basi? Nitaomba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia; mtaimba kwa roho, tena nitaimba kwa akili pia.''
-Kuomba katika ROHO ni muhimu sana lakini nauhakika sio kila saa utakuwa katika ROHO hata uombe katika ROHO.
Wakati mwingine unaweza kuomba kwa akili kabisa lakini kama umeomba kwa MUNGU na katika mpango wake kwako hakika unapokea hitaji lako.
Hatutakiwi Tuombe Kwa Sababu Tunajua Kuomba Bali Tunaomba Ili Tujibiwe.
Maombi Ni Wajibu Kwa Kila Mkristo.
=Maombi Ni Njia Ya Kumkaribia MUNGU Ili Kumwabudu Na Kumsifu Kwa Rehema Zake.
Wafilipi 4:6 ''Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na MUNGU.''
Maombi Ndio Mkono Mrefu Zaidi Wa Kupokea Kutoka Kwa BWANA.
=Ni Muhimu Sana katika maombi yako kukumbuka na Kuwaombea Na Wengine pia
1 Samweli 12:23 '' Walakini mimi, hasha! Nisimtende BWANA dhambi kwa kuacha kuwaombea ninyi; lakini nitawaelimisha katika njia iliyo njema, na kunyoka Mcheni BWANA tu, mkamtumikie kwa kweli kwa mioyo yenu yote; maana, kumbukeni jinsi alivyowatendea mambo makuu. ''
Kila Mtu Anatakiwa Mwenyewe Awe Muombaji.
Kuombewa Ni Muhimu Lakini Wakati Mwingine Ni Kuchelewa Kupokea Maana Huyo Unayetaka Akuombee Na Yeye Anaweza Kuwa Ana Mambo Yake Binafsi Ya Kuombea. Sasa Wewe Kumtegemea Yeye Akuombee, Huku Wewe Hata Hujawahi Kujiombea Inavyotakiwi Itakuchelewesha Kupokea, Maana Ombi Lako Litakuwa Ni Ziada Tu Katika Maombi Yake.
Usipende Kuwaambia Watu Wafunge Kwa Ajili Yako Huku Wewe Unaendelea Na Mambo Yako.
Watafunga Kweli Lakini Watajiombea Wao Tu.
Ushindi Upo Katika YESU KRISTO, Mafanikio Yapo.
Hata Hivyo Tunamiliki Katika Mapambano Ya Kiroho.
Kumb 2:24 "Ondokeni, Mshike Safari Yenu, Mvuke Bonde La Arnoni; Nimemtia Sihoni Mwamori Mfalme Wa Heshboni Mkononi Mwako, Na Nchi Yake; Anzeni Kuimiliki, Mshindane Naye Katika Mapigano".
Ndugu Zangu, Tunatakiwa Tufanye Kitu Ili Kufikia Ushindi Wetu Ambao Uko Tayari Kwa Ajili Yetu.
Tuondoke Tulipo, Tushike Safari Ya Maombi, Tuvuke Mabonde Na Vikwazo Vya Kipepo Ambavyo Ni Vipingamizi Vya Kiroho, Tumtazame ROHO Wa MUNGU Anavyotuelekeza.
BWANA Anasema Amemtia Adui Mikononi Mwetu, Ufalme Wa Kipepo Uko Mikononi Mwetu Hivyo Sisi Ndio Tunapanga Tuwafanyeje.
Tukipenda Wabaki Watatutesa, Heri Kuwapiga.
Tuanze Kumiliki Na Kutawala Kwa Njia Ya Maombi Maana BWANA Ametupa Kumiliki.
Tunachotakiwa Ni Kushindana Na Adui Kwa Kufunga Na Kuomba. Kufunga Na Kuomba Ndio Mapigano Yetu.
Ushindi Wetu Ulipatikana Tangu Msalabani Golgotha.
Neno La MUNGU Ndio Ushindi Wetu.
Tuombe Ndugu Zangu, Adui Anajua Tutashinda Ila Anatuchelewesha Tu ndio maana hapo kwenye andiko tunaweza kujifunza kwamba waisraeli walipewa kumiliki ardhi ila walichotakiwa kufanya ni kuwafukuza tu wenyewe wa aneo hilo ambalo MUNGU amewabariki watu wake.
Ndugu, Mtegemee YESU KRISTO Kwa Maombi Maana Ana Ushindi Wako Na Baraka Yako.
''1 Yohana 3:22Na lo lote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake.''
MUNGU Ni MUNGU Tu.
Mawazo Yetu Sio Mawazo Ya MUNGU.
Tunaweza Kupanga Mipango Yetu Lakini Kumbe Ikawa Tofauti Na Mipango Ya MUNGU Kwa Ajili Yetu, Tutasumbuka Sana Ili Tufanikiwe Lakini Ni Lazima Tu Tufuate Mipango Ya MUNGU Juu Yetu.
Unaweza Kupanga Kutafuta Mchumba Na Kwamba Mwaka Huu Utafunga Ndoa, Wakati Unapanga Hiyo Mipango Ya MUNGU Anataka Uokoke Kwanza.
Mara Nyingi Tunapanga Mipango Mibaya Maana Hata Hatutaki Kuokoka Maana Kuokoka Ndio Mpango Namba Moja Wa MUNGU Kwako.
MUNGU Akisema Neno Hana Kurudi Nyuma Wala Kusita. watu wengi wanatembea katika mipango ya shetani.
MUNGU Anawaonya Watu Wake Kwamba Wasifanye Mapatano Na Waabudu Shetani Maana Watawateka.
Kutoka 34:12-17 '' Ujihadhari nafsi yako, usije ukafanya agano na wenyeji wa nchi ile unayoiendea, lisiwe mtego katikati yako. Bali utabomoa madhabahu zao, na kuvunja-vunja nguzo zao, na kuyakata-kata maashera yao. Maana hutamwabudu mungu mwingine, kwa kuwa BWANA, ambaye jina lake ni mwenye wivu, ni MUNGU mwenye wivu. Usije ukafanya agano na wenyeji wa nchi, watu wakaenda kufanya uzinzi na miungu yao, na kuitolea sadaka miungu yao; mtu mmoja akakuita, ukaila sadaka yake. Ukawaoza wana wako binti zao, nao binti zao wakaenda kufanya uzinzi na miungu yao, wakawavuta wana wenu wafanye uzinzi na miungu yao. Usijifanyizie miungu ya kuyeyusha. ''
Ndugu, Panga Mipango Yako Ukimshirikisha BWANA YESU. Ukipanga Mipango Kwa Kujitegemea Unaweza Ukafanya Mapatano Mabaya, Soma Kutoka 23:20-27 .
Naomba BWANA YESU Awe Yote, Tumtegemee Na Kuomba.
Tulitii Neno La MUNGU Na Kuenenda Kwa ROHO MTAKATIFU. Usijitenge Na Wokovu Wa YESU Maana Kujitenga Na YESU Ni Kujitenga Na Uzima Wa Mikele. BWANA Yuaja.
Ndugu jiokoe na kizazi hiki chenye ukaidi.
BWANA YESU anakungoja sasa ili uamue vyema leo.
Ubarikiwe sana.Nakuomba pia nisaidie kuwasambazia na wengine ujumbe huu.
Ni mimi ndugu yako Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
Mabula1986@gmail.com
+255714252292.
Comments