USHUHUDA WA AJALI MBAYA YA GARI ALIYONUSURIKA KUFA MTUMISHI WILBERT CHUNYULI.

Wilbert Chinyuli.

Ajali ilikuwa mbaya kuliko maelezo, asingekuwa Mungu kututetea kwa kweli mngenizika.
Tar 17 Jpili nilisari ibada ya asubuhi kanisani kwangu Mvumi Dodoma. Nikaondoka saa nne kwenda Dodoma mjini kwa ajili ya kutafuta usafiri kuekekea Dar kununua bidhaa za dukani. Nilifika Dar salama. Na ratiba yangu ilikuwa nirudi Jumanne ya tarehe 19. Jumatatu kwenda bank ni-draw pesa nikaambiwa akaunt ina shida mpaka washughulikie. 

Ushughulikiaji ukakamilika Jumatano ya tarehe 20.
Tarehe hiyo nikaenda Kaliakoo kufanya manunuzi na kukamilisha tarehe 21 ya Alhamisi. Mizigo nikapakia kwenye lori usiku wa Alhamisi na ikafika Dodoma Ijumaa alfajiri. Mimi nikaondoka Ijumaa alfajiri Dar na basi na kufika Dodoma saa kumi.

Baada ya kufika Dodoma nikakodi pickup nikapakia mizigo yangu tayari kwa safari ya kwenda kijijini Mvumi.

Kutoka nje kidogo ya mji wa Dodoma kuna mlima panaitwa Dowico tulinusurika kugongana uso kwa uso na pickup double kibin. Tukaendelea na safari huku tukimshukuru Mungu kwa kutunusuru.
Kufika eneo moja karibu na Mvumi Makulu kwa mtemi Mazengo kuna kona kali, dereva akiwa speed sana akakunja kona kulia na gari ikakataa na kutuvuta huko kulia ikarudi kushoto ikarudi tena kulia, iliporudi tena kushoto ikiwa mwendo mkali ikaanguka kwa kujibamiza kwa nguvu upande wa kushoto niliko kuwa nimekaa mimi. Baada ya kujibamiza upande huo ikaruka juu na kuja kujibamiza kimgongomgongo, maana yake miguu juu, yaani sasa ikapinduka kabisa.

Mimi nilipohisi tu ajali nilifumba macho na kumwambia Mungu kuwa kwa hali hii usalama wetu uko kwake peke yake. Sikufumbua macho mpaka nilipoona kweli tumeanguka ndipo nikafumbua macho na kuona mwanga kidogo dirishani na forcefully kupenyea hapo haraka. 

Mara rafiki yake na dereva aliyekuwa kakaa kati ya dereva na mimi nae akatoka haraka. Wawili tukiwa nje hakuna aliyekumbuka kuwa dereva bado yuko humo mpaka mwenyewe alipopiga kelele kuomba msaada ndipo mimi na rafiki yake tukaanza kubomoa kioo na kumtoa. Tulikuwa watatu: -
Mimi niliyekodi gari
-dereva na-rafiki yake. Nilipotoka sikuamini kama niko hai, sikuamini kama niko hai, sikuamini kama nina viungo vyote salama.
Lakini ashukuriwe sana Mungu nwokozi wa ajabu!


NAMNA ALIVYOTUOKOA MUNGU

Barabara ni ya vumbi lakini imechongwa vizuri na pembeni kuna mfereji kwa ajili ya kutiririsha maji na pembeni ya mfereji kuna ngema kubwa ambayo ndiyo ukingo wa barabara.
Sasa gari kama nilivyosema ilianza kwa kujibamiza upande wangu na kisha kuruka juu na kupinduka upsidedown.
Iliporuka na kupinduka kibini ikalala barabarani, bodi ikalala kwenye ngema. Mahali wanapokaa watu na hapo tulipokuwa tumekaa sisi paka-hang kwenye mfereji na ndo ikawa salama yetu maana hatukubamizwa na kukandamizwa na kitu chichote zaidi ya kugongana sisi kwa sisi na kujigonga kwenye gari lenyewe kwa ndani.


MADHARA

Wote hatukuumia sana, bali michubuko kidogo na maumivu.
Kwa kweli nina mshukuru sana Mungu na nina mtukuza mno kwa jinsi anavyonipenda na namna hasa alivyoniokoa katika ajali ile mbaya sana ambayo sikustahili kupona kabisa.


Mimi katika maisha yangu nimepitia na ninapitia changamoto nyingi sana ambazo naamini ni hila za shetani na mawakala wake ili kunifirisi kiroho na kimwili. Shetani kwa kuwa ni roho anaona vilivyo kusudi la Mungu la kutaka kunibariki kiroho na kimwili ndiyo maana haishi kunifuatilia ini aniangamize. Lakini nina mshukuru sana Mungu kwa kuwa ananipenda na ana mpango nami ndo maana anaendelea kuniokoa na kunitunza mpaka kusudi lake litimie. Nami kwa jina la Yesu nasema sitakufa bali nitaishi mpaka kusudi la Mungu litimie! Amina!!

 Mungu wetu yu hai milele na anaweza. Naahidi kumuishia na kumtumikia maisha yangu yote. Jumapili tutamshukuru Mungu kanisani kwa ajili ya hilo na mengine mengi yasiyo na idadi anayotutendea katika maisha yetu; karibuni tumtukuze Mungu pamoja.

Ajali nilipata Ijumaa, Jumamosi niliendelea na shughuli zangu kama kawaida na jana nimeingia Dar kibiashara na leo nitageuka Dom.
Mungu awabariki saaaana na niombe mniombee!! 

Waweza share pengine popote ili watu wamtukuze na kumwamini Mungu mwokozi wa ajabu

Comments