AINA MBILI ZA MAHUBIRI

Na Mtumishi Dr. Frank P. Seth

“12 Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima. 13Basi Mafarisayo wakamwambia, Wewe unajishuhudia mwenyewe; ushuhuda wako si kweli. 14Yesu akajibu, akawaambia, Mimi ningawa ninajishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu ndio kweli; kwa sababu najua nilikotoka na niendako; lakini ninyi hamjui nilikotoka wala niendako. 15Ninyi mwahukumu kwa kufuata mambo ya mwili; mimi simhukumu mtu. 16Nami nijapohukumu, hukumu yangu ni kweli; kwa kuwa mimi si peke yangu, bali ni mimi na yeye aliyenipeleka. 17Tena katika torati yenu imeandikwa kwamba, Ushuhuda wa watu wawili ni kweli. 18Mimi ndimi ninayejishuhudia mwenyewe, naye Baba aliyenipeleka ananishuhudia. 19Basi wakamwambia, Yuko wapi Baba yako? Yesu akajibu, Mimi hamnijui, wala Baba yangu hammjui; kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba yangu. 20Maneno hayo aliyasema alipokuwa akifundisha hekaluni, katika chumba cha hazina; wala hakuna mtu aliyemkamata, kwa sababu saa yake ilikuwa haijaja bado” (Yohana 8:12-20).
Neno “mahubiri”, yaani kazi ya “mhubiri” kwenye kichwa cha habari hapo juu, linaweza kutumika kwa “mwalimu”, “shahidi” au mtu yeyote asemaye NENO kwa watu wengine kwa namna fulani. Kitaalamu, maneno haya ni tofauti japo kwa muktadha wa dini mara nyingi neno “kuhubiri” limetumika kwa upana na mara nyingine limetumika badala ya “kufundisha” au “kushuhudia”.
Kulingana na KANUNI za wataalamu wa Kiyahudi wakati huo, watu wa dini kabisa, watu waliojua maandiko na kuyatumia, yaani Mafarisayo na wenzao, mahubiri/mafundisho/ushuhuda wa BWANA Yesu ulikuwa UMEPUNGUA kwa sababu za KIUFUNDI kwamba mtu hawezi kujishuhudia mwenyewe! Na akijishuhudia, ushuhuda wake ni wa UONGO (Yohana 8:13).
Ukitazama mistari hii utaona BWANA anawaambia, “hamnijui mimi wala hamumjui Baba (Mungu mnayedai mnamfuata, kumwabudu na kumtumikia)” (Yohana 8:19).
Sasa angalia jambo hili, tufauti kubwa ya Mafarisiyo na BWANA ni EXPERIENCE (hali ya kuhusika na jambo moja kwa moja kwa uhalisia) na sio KNOWLEDGE (kujua kinadharia). Hapa ndipo tunapata aina mbili za WAHUBIRI/WALIMU/MASHAHIDI.
Makundi haya ni:
1. Wanaohubiri/fundisha/shuhudia kwa sababu WAMEJIFUNZA au KUSIKIA habari za Mungu.
2. Wanaohubiri/fundisha/shuhudia kwa sababu ya MAISHA yao binafsi (personal experience) na Mungu.
Makundi haya mawili wanafanana juu ya jambo moja, KNOWLEDGE (ufahamu wa kimaarifa kwa nadharia) na wanatofautina kwa jambo moja EXPERIENCE (uhusiano wao binafsi na Mungu kwa namna ya vitendo na kwa uhalisia).
Ukiangalia vitabu vingi sana kwenye Biblia utagundua kilichoandikwa ni uzoefu binafsi na Mungu (personal experience with God) na sio “waleta habari za wengine” tu.
Angalia vitabu 5 vya Musa, utaona experience ya Musa na Mungu; utaona experience ya akina Yusufu na Mungu; Abraham na Mungu, Yakobo na Mungu, nk. Angalia kitabu cha Joshua, utaona experience ya Joshua na Mungu. Angalia vitabu vya Daniel, utaona experience ya Daniel na Mungu wake; Shadrack, Meshack na Abednego na Mungu wao, nk. Angalia vitabu vya Injili (Mathayo, Marko, Luka na Yohana), utaona experience ya hao mitume na BWANA, pia experience ya BWANA na Mungu na Roho Mtakatifu; Experiance ya BWANA na Shetani kule nyikani akijaribiwa, nk. Ukiangalia kitabu cha Ufunuo wa Yohana, utaona experience ya Yohana na Mungu na mambo yale yaliyoandikwa. Ndio maana Yohana anaeleza vitu kama “nikasikia sauti ya mtu akisema kama sauti ya tarumbeta” hii ni experience.
Wakati Mafarisayo wanadhani BWANA anajishuhudia mwenyewe, hawakujua kwamba BWANA anaongea habari ya experience yake na Mungu; UHUSIANO binafsi na Mungu na mambo anayofanya na Mungu wake. Ndio maana BWANA anasema “sifanyi jambo ambalo sikuliona kwa Baba”; kuona ni “personal experience”, hakusikia tu kwa mtu kwamba Baba alisema, amesikia yeye mwenyewe kwa Baba yake!
Kama kuna jambo gumu kuelewa ni kusema Mungu ni BABA yako wakati huna EXPERIENCE naye wala hukumbuki ni wapi mlikutana (personal encounter) ila vijikitu viwili au vitatu tu vya hapa na pale! Je! Umejiuliza UHUSIANO wako na baba yako mzazi uko hivyo? Kama mtu anaitwa baba yako mzazi basi utasema EXPERIENCE yako na yeye zaidi sana kuliko “ulichosikia” kwa watu juu ya baba yako mzazi. Hivi ndivyo watumishi wengi na “wapendwa” wengi wanafanya kwa baba yao ambaye wanadhani na Baba wa Mbinguni kumbe hawana experience naye! Je! Ni Baba kwao?
Frank P. Seth

Comments