HUDUMA YA KINABII(1)

Na Mtumishi Generali Geoffrey Mwanza Wambua,
The Global Evangelism Ministries (Kenya)
Bwana Yesu asifiwe?
Nabii ni mtumishi aliye na ufahamu wa kindani wa kiroho; ana uwezo wa kusikia kutoka kwa MUNGU moja kwa moja na kupewa mambo yajayo.
Waefeso 2:20 "Mmejengwa juu ya misingi ya mitume na manabii naye Kristo ndiye jiwe kuu la msingi"
Hii ina maana kuwa wateule wa Kristo wote wamejengwa juu ya huduma ya kitume na kinabii ambazo chanzo chake ni Yesu Kristo.
Waefeso 4:11 "Ndiye aliyewapa watu zawadi; wengine mitume; wengine manabii;wengine wainjilisti; wengine wachungaji na kisha waalimu;Alifanya hivyo spate kuwatayarisha watu wote wa MUNGU kwa ajili ya kazi ya huduma ya Kristo; ili kuujenga mwili wa Kristo"
Si kila mtoa unabii Kanisani au popote ambaye ni nabii; kwani kuna tofauti kati ya unabii na nabii.
Unabii anaweza kutoa mtu yeyote kwa kutumiwa na ROHO MTAKATIFU wakati huo wa kutoa ujumbe.
Nabii tunayezungumzia ni mtu anayetumika upande huo kama ofisi yake (huduma yake).
Nabii ni lazima aambatane na karama zifuatazo:
-Neno la hekima
-Neno la ujuzi

Umuhimu wa unabii kama yasemavyo maandiko ni kuonya; kujenga; kutia moyo na kufariji.
1Korintho 14:3-4"Lakini mwenye kipaji cha kutabiri husema na watu kwa ajili ya kuwajenga; kuwafariji na kuwatia moyo"
Kunao manabii aina mbili; manabii wa kweli na manabii wa uongo.
Mathayo 7:15 " Jihadharini na manabii wa uongo wanaowajieni wakivaa nguo za kondoo na kumbe ndani yao ni mbwa mwitu"
Mathayo 24:24 "Watatokea manabii wa uongo; watafanya ishara kubwa na maajabu na kuwapotosha hata wateule"
Nabii wa uongo hutumia nguvu za giza (Kumbukumbu 13:1-4)
Yeremia 23:25-27 na 23:32.
Nabii wa uongo humpinga sana nabii wa kweli (1Wafalme 22:24) ambapo tunamwona nabii wa uongo Zedekia akimpiga kofi nabii wa MUNGU Mikaya.
Somo hili la "Huduma ya Kinabii" ni refu sana na lipitie mpaka mwisho utajifunza mengi.Nimetayarisha kutoka sehemu ya kwanza hadi ya tisa ili ukajifunze mpendwa.
Unabii sahihi lazima uwekwe chini ya misingi sahihi ya mafundisho sahihi yanayoambatana na Neno la Yesu Kristo la kuokoka na kuacha dhambi.
YESU KRISTO ndiye jiwe kuu la pembeni ambalo mitume na manabii wamejengwa juu ya mafundisho sahihi na imani sahihi na Kanisa (mwili wa Kristo).
Ili huduma ya kinabii ikamilike; lazima pawe na mafundisho ya kweli ya toba kwani unabii wa kweli unaandamana na Neno la injili ya Bwana YESU.
Anachokitabiri nabii wa MUNGU lazima kiendane na anachosema MUNGU katika maandiko (Biblia) kwani MUNGU hajipingi kwa Neno lake.


AINA ZA MANABII
Luna zaidi ya aina kumi na tano za manabii ambao nitafundisha hapa katika somo hili; manabii hawa ni pamoja na:
-Nabii wa ndoto
-Nabii wa maono
-Nabii wa mafunuo
-Nabii wa maono ya MUNGU Baba.
-Nabii wa baraza
-Nabii wa Neno
-Nabii wa Neno;maono na mafunuo ya MUNGU
-Nabii anayezungumza na MUNGU mdomo kwa mdomo.
-Nabii mwenye mamlaka ya kuliitia Jina la Bwana akaitikwa.
-Nabii wa mataifa
-Nabii katika idara ya mwonaji.

NABII WA NDOTO
Hii hutokea usiku anapolala usingizi mzito; Mara nyingi ndoto hutokea mtu anapolala usingizi mzito na hasa usiku wa manane.
Kuna watu hupinga ndoto sana; Mimi Geoffrey miaka saba nyuma hats nikiwa sijaokoka; MUNGU alikuwa akiongea nami katika ndoto akiniambia kuwa nitakuja kuhubiri injili na nilikuwa nikipuuza; lakini alichokuwa akinambia MUNGU ndicho hiki ninachokifanya leo!
Hesabu 12:6 "Kisha MUNGU akawaambia"sikilizeni maneno yangu kama kuna nabii miongoni mwenu Mimi MUNGU hujifahamisha kwake katika maono na kuongea naye katika ndoto"
Kumbuka Yusufu aliota ndoto pia zikaja kutimia baada ya muda mrefu; (Mwanzo 37:9
Yeremia 23:28 "Nabii aliye na ndoto aseme ndoto yake na yeye aliye na Neno langu aseme Neno language kwa uaminifu"
Nabii anayefunuliwa kupitia ndoto anapata maneno haya kama ifuatavyo:
MUNGU hupenda kutumia mfumo wa fikra ulio ndani ya mwanadamu ili kupitisha ujumbe wa picha na sauti kwa namna ya ndoto kumwarifu mtu tukio fulani.
Unspoamka usingizini na upate kuwa ulikuwa waota ndoto ya kupigana vita na mapepo unachotakiwa kufanya ni kuomba ukizuia vita hivo ulivyoviona ndotoni.
Watu wengi leo wanaoteshwa wakilishwa vyakula vya kichawi ndotoni; wakifukuzwa na mashetani; walk nyongwa; wakifanyiwa mapenzi na watu wasiowajua katika ndoto kisha wanadharau.
Wengine wanaoteshwa wakifunga harusi ndotoni; kumbe ni mapepo/mizimu inayowafunga ili wasiolewe; unakuja kushtukia ukiwa na miaka 37 na bado uko kwenu au uliolewa na ukaachwa.
Waweza pia kuoteshwa ukiwa ndani ya pango; ukiota nyoka;mazishini kwenu au visanga viovu; unatakiwa uombe na kukaa kwa utakatifu ndani ya wokovu wa YESU KRISTO.
Kuna matukio mengi sana ya ndoto katika Biblia (Mwanzo 15:12-16,28:21-17,37:5,40:5-8, Danieli 2:1-4, Hesabu 22:20, Mathayo 2:13-15 nk


2.NABII WA MAONO
Nabii huyu hupewa jicho la kiroho la kuona umbali wa wastani kwa mfano miezi kadhaa iliyopita au ijayo.
2Samweli 12:1-7-9 "Ndipo Bwana akamtuma Nathani kwa Daudi.Nathani akamwendea Saudi akamwambia" Kulikuwa na wanaume wawili katika mji mmoja; mmoja alikuwa tajiri na mwingine maskini...."
Kuna aina nyingi sana za manabii wa maono na ambazo tunazipata ndani ya huduma hii.
Aina za Manabii wa maono:
-Nabii wa maono anayefunuliwa mashauri ya wafalme.
-Nabii wa maono anayetumika na adhabu ya MUNGU
-Nabii wa maono anayetumika na sauti ya baragumu.
-Nabii wa maono ya mbinguni anayetumika na radi kuu.
-Nabii wa maono anayetumika na baragumu saba.
-Nabii wa maono anayefunuliwa kupitia kioo.
-Nabii wa maono mwenye karama na matendo makuu ya miujiza ya MUNGU .

Nabii wa maono anayefunuliwa siri za wafalme(2Samweli 12:1-10)
Huyu anafunuliwa siri na mashauri ya watawala au wakuu wa kidunia.Mara nyingi MUNGU anamwonyesha mashauri ya wafalme na kumtuma kwenda kuwaonya.
Nabii huyu anakuwa mkali sana anapoonya katika asili yake.Baada ya kuokoka anapokea kipawa hiki na kutumika namna hii.
Nabii huyu hutumika na adhabu kwani anaweza kutamka vitu vya kuadhibu na zitatokea.
Baadhi ya adhabu ni kama:
-Mapigo ya njaa katika uso wa nchi yanayosababisha vifo.
-Fimbo ya magonjwa makubwa kama tauni;yanayopelekea watu kufa.
-Fimbo ya vita katika nchi inayosababisha maafa mfano kama lililotokea Yugoslavia; Bosnia;Afghanistan; Iraq; Iran nk.

Nabii wa aina hii akipatikana Kanisani lazima viongozi na waumini wakae katika tahadhari na kwa utakatifu lasivyo kifo kinawamaliza; kwa sababu kinywa chake ni hatari sana kwa wanaomwasi MUNGU.
Nabii wa maono anayetumika na sauti ya baragumu
Huyu anapokea unabii katika hali na namna ya utukufu na utisho wa pekee unaoambatana na sauti yenye vitisho kutoka mbinguni inayoambatana na sauti yenye utisho kutoka mbinguni kwa MUNGU.
Ufunuo 1:10-13 "Nilikuwa katika Roho siku ya Bwana; mikado a sauti kuu nyuma yangu kama sauti ya baragumu......"


Nabii wa maono ya mbinguni anayetumika na radi kuu:
Huyu hutumika na uchungu na hasira kali sana ya MUNGU na nguvu nyingi za MUNGU.Hubeba unabii wenye maonyo kutoka mbinguni maana amepewa jukumu la kufuatilia utekelezaji wa sheria ya Mungu ndani ya Kanisa la Yesu mahali atakapoelekezwa na MUNGU.
Ezekieli 3:12-17 "Ndipo roho ikanichukua nami nikasikia nyuma yangu sauti kama mshindo wa radi kuu...."
Maadili ya kiroho yanapovunjwa nabii huyu huwa mkali sana wakati wa kuonya akiwa katika mafuriko ya RohoMtakatifu kwa wingi na hasira kali wakati wa maombi au ibada ndipo utisho wa hali ya juu unatawala mahali alipo.Pia anatumika na Roho ya utakatifu akiwa katika hali hii

Warumi 1:4 "Na kudhihirishwa kwa uweza kuwa mwana wa MUNGU kwa jinsi ya Roho ya utakatifu kwa ufufuo wa wafu; Yesu Kristo Bwana wetu".
Nabii wa maono anayetumika na ngurumo saba
Hupokea ujumbe kutoka mbinguni kwa namna ya utisho sana unaoambatana na ngurumo saba; ndani ya kila ngurumo inayomjia inaambatana na sauti na picha au atakavyopenda MUNGU mwenyewe.
Ufunuo 10:1-3 "Kisha nikaona malaika mwingine mwenye nguvu akitoka mbinguni amevikwa wingu na upinde wa mvua juu ya kichwa na uso wake...."
Nabii wa aina hii ana uwezo wa kufundisha madhabahuni kwa sura ya mwalimu.
Nabii huyu ni muhimu sana kwa Kanisa maana anapewa ufunuo wa Neno na wakati anafundisha anaweza kuangalia ulimwengu wa kiroho na kupata mafunuo yanayowahusu anaowafundisha wakati akiwa madhabahuni.
Huyu ndiye mwalimu wa kipekee anayehitajika Kanisani ili kusaidia wengi wenye mahitaji.

Nabii wa mafunuo anayefunuliwa kupitia kioo
Nabii huyu ansfunuliwa kupitia kioo maalum kutoka mbinguni.Kioo hiki kina picha ambayo Roho anataka nabii huyu some na kuileta kwa macho yake ya rohoni.

1Korintho 13:12 "Maana wakati wa sasa tunaona kwa kioo; kwa jinsi ya fumbo wakati ule tutaona uso kwa uso ....."
Maneno yaliyofichika sana kutoka ulimwengu wa roho; yeye anapewa neema ya ziada inayomwekea kioo ili aone kwa ufasaha.

Nabii wa maono mwenye karama na matendo makuu ya miujiza ya MUNGU
Nabii huyu anatumika sana na maajabu ya MUNGU pua anatumika na nguvu ya uumbaji wa ki-Mungu na nguvu za zamani zijazo
 
 
Nabii wa maono mwenye karama na matendo makuu ya miujiza ya MUNGU.
Nabii huyu anatumika sana na maajabu ya MUNGU; Pia anatumika na nguvu za uumbaji wa ki-Mungu na nguvu za zamani zijazo kutoka mbinguni kwa hali ya juu sana inayopita uweza wa kufikiri kwa mwanadamu.

Waebrania 6:4 "Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru na kukionja kipawa cha mbinguni na kufanywa washirika wa RohoMtskatifu"
Mfano wa zamani wa nguvu zijazo:
Marko 6:47-51 Yesu akitembea juu ya maji.
Kutoka 7:19. Musa anageuza maji kuwa damu.
Kutoka 8:17 Musa anageuza vumbi kuwa chawa.
Kutoka 14:15-18 Musa agawanya bahari na njia kupatikana.
Kutoka 17:6-7 Musa apiga jabali na kutoa maji.
Nabii wa aina hii anaweza kuita kitu chochote na kikatokea katika hali ya kushangaza sana.Akitamka neno hats kama ni la kwake linatokea wakati huo huo.

Yoshua 10:22 "Ndipo Yoshua akasema "Wewe jua simama; nalo jua likasimama....."
Hatari iliopo kwa nabii wa aina hii ni kuwa ukimdharau; ukimwonyesha ujeuri unakufa.

Sasa tumemaliza manabii wa maono; tulikuwa tumewaona manabii wa ndoto; Tuwaangalie sasa manabii wa mafunuo;
3.NABII WA MAFUNUO
Huyu hupewa jicho la kuona mbali sana kama miaka mingi ijayo au iliyopita.
Ufunuo 21:10 "Akanichukua kwa Roho mpaka mlima mkubwa mrefu akanionyesha ule mji mtakatifu....."
Faida za nabii wa mafunuo kiuchumi:
Kuna wale ambao wana neema ya kuonyeshwa mambo ya elimu na aina mbali mbali za ufundi; sayansi na tekinolojia kwa ajili ya maendeleo na ustaarabu.
Manabii wa aina hii wameisaidia sana Ulaya; Marekani kuendelea kisayansi na tekinolojia hata kiuchumi.

Kutoka 31:1-4 "MUNGU akamwambia Musa angalia nimemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Huri naye nimemjaza Roho ya MUNGU katika hekima; maarifa na ujuzi...."
4.NABII WA MAONO YA MUNGU BABA
Ezekieli 8:1-3 "Naye akanyosha mfano wa mkono akashika kwa kishungi kimoja cha nywele za kichwa changu;nayo Roho ikaniinua kati ya dunia na mbingu...."
Nabii wa aina hii amepewa neema ya kuvishwa mwili wa malaika kiasi cha kushangaza.Anaweza kutoweka na baadaye kurejea kama malaika.
Huyu anapewa neema ya kuona na kusikia siri za wanadamu na za MUNGU ; huwa anapelekwa mahali na kuonyeshwa maneno.
Hawaendi kwa mapenzi yao bali ya MUNGU ; Nabii huyu analetwa na Roho ndani ya nyumba fulani na kuonyeshwa siri za ndani sana za wanadamu.


Itaendeleaaaaaaaaaaaa ......................


 Kwa mawasiliano ya maombi ya siri ya kutubu dhambi hii; nipigie: Generali Geoffrey Mwanza Wambua,
The Global Evangelism Ministries (Kenya)
+254 724 656 653
geoffreymwanza@yahoo.com

Comments