JILINDE ILI MOYO WAKO USIJE UKALEMEWA NA MAMBO YA DUNIA.

 Na Peter M Mabula. Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.


BWANA YESU atukuzwe.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Niseme Au Nisiseme?
Ngoja Niseme Najua Atapona Mtu Kupitia Ujumbe Huu.
BWANA YESU Anasema Katika Luka 21:34-36 Kwamba "Basi Jiangalieni, Mioyo Yenu Isije Ikalemewa Na Ulafi, Na Ulevi, Na Masumbufu Ya Maisha Haya; Siku Ile Ikawajia Ghafla, Kama Mtego Unasavyo. Kwa Kuwa Ndivyo Itakavyowajilia Watu Wote Wakaao Juu Ya Uso Wa Dunia Nzima. Basi, Kesheni Ninyi Kila Wakati, Mkiomba, Ili Mpate Kuokoka Katika Haya Yote Yatakayotokea, Na Kusimama Mbele Za Mwana Wa Adamu".
 
 Jiangalieni, Mioyo Yenu Isije Ikalemewa Na Ulafi, Na Ulevi, Na Masumbufu Ya Maisha Haya; Siku Ile Ikawajia Ghafla.
Siku ya mwisho itakuja ghafla maana hakuna mwanadamu atakuwa anajua siku hiyo ila atakayekuwa anajua ni  MUNGU tu.
Kuna mambo mengi ya kidunia yanaweza kumfanya mwanadamu kuwa mbali na MUNGU wake.
Mambo mengi ya kidunia yanaweza kumfanya mwanadamu akawa mbali na Mwokozi wake.

Watu Wengi Kwa Ulafi Wao Hukosa Muda Maombi Ya Kufunga Au Hata Maombi Ya Kawaida Na Hivyo Kubakia Watu Wa Mwilini. 
Na Siku zote Watu Wa Mwilini Huwa Viwanja Vya Kuchezea Mapepo, Majini Na Mizimu. 

Yohana 3:6 '' Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa ROHO ni roho.'' 

Mtu Asiye Na Maombi Siku Zote Huwa Hayuko Macho Kiroho, Huwa Mvivu Kiroho, Anatekwa Na Mihemko Ya Uzinifu. 
Ukiwa Mtu Wa Mwilini Akili Zako Hujaa Uchafu Na Mawazo Mabaya. 
Hata Mchungaji Au Askofu Kama Huwa Huombi Unaweza Kuwa Mateka Wa Dhambi. 

Warumi 8:7 Inasema "Kwa Kuwa Ile Nia Ya Mwili Ni Uadui Juu Ya MUNGU".

 Nia Ya Mwili Ni Uadui Kwa MUNGU Kwa Sababu Nia Ya Mwili Haikusudii Mema.
 Nia Ya Mwili Haimzuii Mtu Kufuata Utaratibu Wa Dini Na Ibada Kila Siku Asubuhi, Mchana Wala Jioni Lakini Nia Hiyo Ya Mwili Inaweza Kumzuia Mtu Huyo Kuokoka. 

Mathayo 26:41'' Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.''

Nia Ya Mwili Inamtaka Muombaji Kuomba Kidogo Tu Ili Mwili Usichoke.
 Ukiwa Mtu Wa Kuutii Mwili Utatenda Dhambi Tu Lazima. 
Mwili Unachotaka Ni Uzinzi, Kula Chakula Kizuri Na Kutunzwa Hivyo Inatakiwa Kila mtu Amtii MUNGU Badala Ya Kuitii Nia Ya Mwili. 
Kama Mwili Unakukosesha Hakikisha Unaokoka Na Hakikisha Unakuwa Na Muda Wa Kufunga Na Kuomba Pamoja Na Kuwa Na Muda Wa Kuomba Maombi Ya Kuutiisha Mwili Wako. 
Jitenge Na Marafiki Wabaya Na Kataa Mazoea Mabaya Na Watu Wa Jinsia Tofauti Na Yako, Acha Kusikiliza Wala Kuangalia Nyimbo Za Kidunia Na Usiangalie Picha Wala Video Za ngono. Mwite BWANA YESU Atakushindia.

 Hata kama umeokoka tayari naomba ujumbe kwamba maadui bado wapo. Maadui Zako Wakuu Ni Shetani Na Mwili Wako. Ndugu Yangu, Tiisha Mwili Wako Na Huyo Shetani Hatapata Nafanya Kwako. Jina La BWANA Ni Ngome Imara; Mwenye Haki Huikimbia Akawa Salama.

Mithali 18:10 '' Jina la BWANA ni ngome imara; Mwenye haki huikimbilia, akawa salama.''

Ukiona Mtu Matumaini Kwa MUNGU Yamepungua Ujue Kabisa Mtu Huyo Matumaini Kwa Wanadamu Yameongezeka. 
Huko ndiko kwenenda kimwili na sio kiroho.
Ni Hatari Mtu Kuondoa Tumaini Kwa MUNGU Aliyemuumba Na Kuhamishia Tumaini Lake Kwa Wanadamu.

Watu wa Mwilini hata kulipiza kisasi kwao ni kawaida.
Kumbuka kwamba Ubaya Huwa Unashindwa Kwa Wema Tu Na Si Vinginevyo. Huwezi Kuushinda Ubaya Kwa Kutenda Ubaya. Usilipe Ubaya Kwa Ubaya Bali Lipa Ubaya Kwa Wewe Kutenda Mema. 

Warumi 12:21 '' Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema. ''

Kuna watu pia husema kwamba ujana ni maji ya moto laki ukweli ni kwamba Ujana utaitwa maji ya moto kama tu mwanadamu atautumia ujana wake kwa shetani, huko ndiko kwenda kimwili. Hayo ndiyo matendo ya mwilini ambayo hayatakiwi kuwa kwa wanadamu.

Utafiti wangu ni huu.
Watenda dhambi wanaotambua kwamba wanatenda dhambi ni 98%
Watenda dhambi wanaotaka kutubu na kuacha dhambi ni 2%
Watenda dhambi wanaoutaka uzima Wa milele ni 100%
Watu wengi wanautaka uzima wa milele lakini hawataki kuufuata uliko ambako ni kwa YESU KRISTO tu.
Watu wengi wanajua kabisa kwamba wanatenda dhambi lakini hawataki kutubu, hiyo ni hatari, hiyo ni kuukataa uzima wa milele. 

1 Petro 1:15 '' bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;''


Leo injili inahubiriwa kila mahali ili watu wapone.
Leo Tunahubiri Injili ya BWANA YESU ili watu waokoke.
Leo Tunahubiri ili watu waujue ukweli pekee kwamba bila YESU hawawezi kusamehewa na tena bila YESU hawawezi kuingia Uzima Wa  milele.

 Mithali 14:8 ''Akili za mwenye busara ni kujua njia yake; Lakini upumbavu wa wapumbavu ni udanganyifu.'' 

 Ukweli Niliotaka Uujue Leo Ni Huo, Naamini Umeupokea Na Utachukua Hatua Njema. BWANA YESU Yu Karibu Kumlipa Kila Mwanadamu.

Asante kama unanielewa ndugu yangu.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili.

Comments