KAHABA HUMWINDA MTU ILI AMNASE NAFSI YAKE ILIYO YA THAMANI.

 Na Peter M Mabula. Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.


 BWANA YESU atukuzwe.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Leo tunajifunza kuhusu kahaba na ukahaba.

Mithali 6:26b  ''Na kahaba humwinda mtu anase nafsi yake iliyo ya thamani ''.

Kahaba ni mtu anayefanya mambo ya uasherati.
Kahaba ni malaya.
Malaya ni mwanamke au mwanaume mwenye tabia ya uzinzi.
Kahaba humwinda mtu ili anase nafsi yake iliyo ya thamani, ndugu kataa dhambi hiyo.
Kahaba ni mwanamke anayejiuza   ili kupata pesa.
Makahaba ni viberenge na vibiriti ngoma, ni mbaya sana mwanadamu kuwa kahaba.

Ezekieli 16:15 ''5 Lakini uliutumainia uzuri wako, ukafanya mambo ya kikahaba kwa sababu ya sifa zako, ukamwaga mambo yako ya kikahaba juu ya kila mtu aliyepita; ulikuwa wake.''

Biblia inakataza ukahaba.
Ukahaba ni dhambi na ukahaba hautakiwi kuwa kwa watu wapendwao na MUNGU.
Maana nyingine ya kahaba ni kiruka njia.
Kiruka njia ni mwanamke au mwanaume asiyetulia katika ndoa yake.
Kahaba ni mzinifu.
Mzinifu maana yake ni mtu mwenye tabia ya kufanya ngono na mtu asiye na ndoa naye.
Ni dhambi kuwa kahaba na ni dhambi kujihusisha na ukahaba.
Kahaba humwinda mtu ili anase nafsi yake iliyo ya thamani, ndugu kataa dhambi hiyo.

1 Kor 6:15-16  '' Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya KRISTO? Basi nivitwae viungo vya KRISTO na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha! Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja. ''

Makahaba ni machangudoa yaani ni wanawake wanaojiuza ili kupata pesa.
Biblia hapo juu inasema ''Aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja na kahaba''
Je ni watu wangapi ambao ni mwili mmoja na kahaba?
Kwanini ndugu uamue kuwa kahaba?
Kuwa kahaba ni kumchagua shetani ili akutumie, ni hatari sana.
 Wewe mkristo kwa sababu ya wokovu na utakatifu umekuwa mwili mmoja na KRISTO hivyo haitakiwi wewe kuhusika kwenye dhambi ya ukahaba tena.
 Kahaba humwinda mtu ili anase nafsi yake iliyo ya thamani, ndugu kataa dhambi hiyo.

kahaba jina jingine anaitwa dadapoa.
Kwa nini uitwe dadapoa?
Umekubali kuwa kama mpira ambapo kila mchezaji huupiga tu atakavyo.
Umekubali kuwa kama njia ambayo kila mtu huikanyaga, kila ngome hupitia na kuinyea, nyoka huivuka na mvua huinyeshea na kuacha matope.
Haitakiwi kabisa wewe uliyeumba na MUNGU vizuri eti ukajihusisha na ukahaba.
Ndugu, ni vyema ukajitenga na ukahaba.
Ni vyema ukajitenga na makahaba wanaokutaka kimapenzi.
Usikubali kuisaliti ndoa yako.
Usikubali kufanya uzinzi wala uasherati. Kahaba humwinda mtu ili anase nafsi yake iliyo ya thamani, ndugu kataa dhambi hiyo.

Mithali 6:25 ''Usiutamani uzuri wake moyoni mwako; Wala usikubali akunase kwa kope za macho yake. ''

 Kahaba sio lazima awe barabarani tu, hata mtandaoni kuna makahaba wengi tu.
Hata kanisani anaweza kuwepo kahaba kama mtu huyo hufanya uzinzi na uasherati.
Hata kazini kwako anaweza kuwepo kahaba kama mfanyakazi mwenzako huyo anakutaka kimapenzi.
Huyo mzinzi usikubali akunase kwa kope zake.
Huyo anayevaa mavazi ya kikahaba usikubali akakunasa kwa kope zake.
Huyo anayevaa vimini mitaani  usikubali akakunasa kwa kope zake.
Huyo anayevaa nguo za kuacha matiti nje usikubali akakunase kwa kope zake.
 Kahaba humwinda mtu ili anase nafsi yake iliyo ya thamani, ndugu kataa dhambi hiyo.

 Mithali 6:32 '' Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.''

Usikubali kuisaliti ndoa yako iliyo ya thamani sana mbele za MUNGU.
Usikubali kuwafuata dadapoa, ni dhambi.
Kama wewe ni kahaba hakikisha unaacha ukahaba na okoka ili jina lako  libadilike kutoka kuitwa kahaba na uanze kuitwa mteule wa MUNGU.
Hakuna mzinzi  mwenda mbinguni  labda tu atubu  na kuacha uzinzi wake.
 Kahaba humwinda mtu ili anase nafsi yake iliyo ya thamani, ndugu kataa dhambi hiyo.
Mwandishi mmoja wa Biblia aliona kijana akilaghaiwa na mwanamke mke wa mtu.
Mwandishi huyo wa Biblia anasema;

''
Maana katika dirisha la nyumba yangu Nalichungulia katika shubaka yake; Nikaona katikati ya wajinga, Nikamtambua miongoni mwa vijana, Kijana mmoja asiyekuwa na akili, Akipita njiani karibu na pembe yake, Akiishika njia iendayo nyumbani kwake, Wakati wa magharibi, wakati wa jioni, Usiku wa manane, gizani. Na tazama, mwanamke akamkuta, Ana mavazi ya kikahaba, mwerevu wa moyo; Ana kelele, na ukaidi; Miguu yake haikai nyumbani mwake. Mara yu katika njia kuu, mara viwanjani, Naye huotea kwenye pembe za kila njia. Basi akamshika, akambusu, Akamwambia kwa uso usio na haya, Kwangu ziko sadaka za amani; Leo hivi nimeziondoa nadhiri zangu; Ndiyo maana nikatoka nikulaki, Nikutafute uso wako kwa bidii, nami nimekuona. Nimetandika kitanda changu, magodoro mazuri, Kwa matandiko ya Kimisri yenye mistari. Nimetia kitanda changu manukato, Manemane na udi na mdalasini. Haya, na tushibe upendo hata asubuhi, Tujifurahishe nafsi zetu kwa mahaba. Maana mume wangu hayumo nyumbani, Amekwenda safari ya mbali; Amechukua mfuko wa fedha mkononi; Atarudi wakati wa mwezi mpevu. Kwa maneno yake mengi na ulaini akamshawishi, Kwa ubembelezi wa midomo yake akamshinda. Huyo akafuatana naye mara hiyo, Kama vile ng'ombe aendavyo machinjoni; Au mpumbavu kuadhibiwa katika pingu; Hata mshale umchome maini; Kama ndege aendaye haraka mtegoni; Wala hajui ya kuwa ni hasara ya nafsi yake. -Mithali 7:6-23 ''

 Kwenda kufanya uzinzi ni kwenda machinjioni maana yake ukifa  katika uovu huo wewe ni wa jehanamu.
Kufanya ukahaba ni kuchungulia mlango wa jehanamu.
Kufanya uasherati ni kujiharibia maisha yako wewe mwenyewe.
Kahaba ni aina ya mtu ambaye '' .... amewaangusha wengi waliojeruhi, Naam, jumla ya waliouawa naye ni jeshi kubwa. Nyumba yake ni njia ya kwenda kuzimu, Hushuka mpaka vyumba vya mauti.-Mithali 7:26-27''

Ndugu, Acha ukahaba.
acha kusaliti ndoa yako.
Acha kufanya ngono wakati wa uchumba, ni dhambi na ni mbaya sana.
 Kahaba humwinda mtu ili anase nafsi yake iliyo ya thamani, ndugu kataa dhambi hiyo.
 ukahaba ni upumbavu.
Ili mtu asiwe mpumbavu anatakiwa aache upumbavu.
Mithali 9:13-18 '' Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu. Hukaa mlangoni pa nyumba yake, Juu ya kiti mahali pa mjini palipoinuka, Apate kuwaita wapitao njiani, Waendao moja kwa moja katika njia zao. Kila aliye mjinga na aingie humu. Tena amwambia mtu aliyepungukiwa na akili, Maji yaliyoibiwa ni matamu, Na mkate ulioliwa kwa siri hupendeza. Lakini huyo hajui ya kuwa wafu wamo humo; Ya kuwa wageni wake wamo chini kuzimuni. ''

 Kahaba humwinda mtu ili anase nafsi yake iliyo ya thamani, ndugu kataa dhambi hiyo.
Asante kama unanielewa ndugu yangu.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili.

Comments