KANISA BILA KUWA PAMOJA KWA UMOJA HALIWEZI KUSONGA MBELE.


 
Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU

BWANA YESU atukuzwe mtu wa MUNGU.
Karibu tujifunze Neno hai la MUNGU.

Zaburi 133:1 '' Tazama, jinsi ilivyo vema, na kupendeza, Ndugu wakae pamoja, kwa umoja.''

Wana kanisa ni ndugu katika KRISTO na ili kuifanya kazi ya MUNGU vyema wanatakiwa wawe pamoja tena kwa umoja.
Ni vizuri kukaa pamoja kwa umoja.
Tunaweza kukaa pamoja lakini tusiwe pamoja.
Tunaweza tukaimba pamoja lakini tusiwe na umoja.
Tunaweza tukahubiri pamoja lakini tusiwe na umoja.
Kanisa kuwa pamoja tu haitoshi kama umoja hautakuwepo.
Tunaweza tukapanga mipango pamoja lakini kama hatuna umoja mipango yetu haitafanikiwa.
Kukaa pamoja kwa umoja maana yake ni kupanga mipango pamoja na  kuitekeleza mipango hiyo pamoja.
Kukaa pamoja kwa umoja  ni kuwa pamoja, kupanga pamoja, kuwa na nia moja au kunia mamoja katika mipango hiyo.
Mfano kanisa linaweza likapanga kwamba kabla mwaka haujaisha liwe limemaliza ujenzi. Kama hakuna umoja katika kanisa hilo ujenzi ule utabaki midomoni tu lakini sio katika matendo, maana hakuna pamoja kwa umoja kwa watu hao.
Jambo la kujua ni kwamba Bila umoja hakuna jambo linaloweza kufanikiwa.

Mwanzo 13:8 ''Abramu akamwambia Lutu, Basi, usiwepo ugomvi, nakusihi, kati ya mimi na wewe, wala kati ya wachungaji wangu na wachungaji wako; maana sisi tu ndugu.'' 

Ibrahimu la Lutu walikuwa ni wateule wa MUNGU waliobarikiwa na MUNGU.
Ibrahimu kwa kutambua faida za umoja na madhara ya kutokuwa na umoja alimua kutengeneza na ndugu yake ili umoja wao uendelee kudumu.
Ibrahimu anasema kusiwepo na ugomvi maana yake kuwepo na umoja.
Ukiona kwenye kikundi au idara au kwenye viongozi kuna ugomvi maana yake hakuna pamoja kwa umoja.
Kama ndugu katika KRISTO ni lazima muwe na umoja ndipo kazi ya MUNGU itaendelea mbele zaidi.

1 Kor 1:10 ''Basi ndugu, nawasihi, kwa jina la BWANA wetu YESU KRISTO, kwamba nyote mnene mamoja; wala pasiwe kwenu faraka, bali mhitimu katika nia moja na shauri moja.'' 

Moja ya mafundisho muhimu kwa kanisa ni kuwa pamoja kwa umoja katika KRISTO.
Biblia hapo kwenye andiko inawataka kanisa la MUNGU kunena mamoja katika utakatifu maana yake haitakiwi roho ya uasi katika kanisa, haitakiwi usengenyaji katika wana kanisa.
Biblia inalitaka kanisa kuwa na shauri moja katika utakatifu na kuwa na nia moja katika kazi ya MUNGU, kwa kufanya hivyo faraka au niseme mafarakano hayatakuwepo kanisani.
Leo kuna baadhi ya makanisa waumini hadi wamefikia hatua ya kugawanyika.
Unakuta ndani ya kanisa hilo moja kuna kundi la mchungaji, kuna kundi la mama mchungaji, kuna kundi la katibu wa kanisa na kuna kundi la mzee wa kanisa. Kama kundi moja likipanga mipango ya maendeleo kwa kanisa ni rahisi sana kundi jingine kupinga na kuanza kampeni za kuhakikisha jambo husika halifanyiki katika kanisa.
Ndugu zangu, ni muhimu sana kujua kwamba kanisa la KRISTO ni moja na linatakiwa kumfuata KRISTO na sio mambo ya kidunia.
Biblia inakataza jambo moja tu kwamba kanisa halitakiwi kuwa na umoja na dhambi tu basi.
Hivyo kama kuna mtu ni mpingaji wa mambo ya dhambi huyo anafanya vyema lakini yule anayepinga hata mipango ya kiMUNGU kabisa na ambayo hata Biblia inaagiza huyo hafai.
Ni vizuri sana ndugu waliookoka wakae pamoja kwa umoja.
Ni muhimu sana wateule wa KRISTO wakae pamoja kwa umoja.

Yakobo 4:6 ''Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, MUNGU huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu.''

MUNGU huwapinga wajikuzao.
Wajikuzao ni wale wenye viburi, ni wale ambao maoni yao tu ndio hutaka yatekelezwe na si vinginevyo.
Kanisa linatakiwa liwe pamoja kwa umoja.

Madhara ya kutokuwa pamoja kwa umoja ni pamoja na;

1.  Kutokufanikisha mipango mzuri mliyojiwekea kama kanisa.
-Bila umoja hakuna utekelezaji katika mipango hiyo.

2.  Huduma ya kazi ya MUNGU haitasonga mbele.
-Maana kutokuwa na umoja ni kizuizi cha huduma kusonga mbele.
 
3.  Nguvu na uwepo wa MUNGU kutokuwepo kanisani.
-Kanisa kutokuwa na umoja wa kiMUNGU kutazalisha mambo mengine yasiyompendeza MUNGU, na hayo ndivyo yatakayokuwa yananyosha nguvu za MUNGU kanisani na kuondoa uwepo wa MUNGU kanisani.
 
4.  Dhambi itatawala.
-Kwa sababu pasipo umoja kutakuwa na chuki, masimango na uzushi usio na maana N.k na hivyo vyote ni dhambi.

5.  Makwazo yatatawala.
-Kama hakuna umoja kanisani ni rashisi tu viongozi kupendelea na hivyo kuwakwaza wengine N.k
 
6.  Kutakuwa na ubaguzi ndani ya kanisa.
-Umoja ukiondoka kwa vyovyote vile dhambi ya ubaguzi itachukua nafasi.
 
7.  Kutakuwa na kudharauliana.
-Kama umoja ukiondoka lazima pia dharau ichukue nafsi.

Ni Vizuri sana kanisa la MUNGU likwa pamoja kwa umoja.

Yohana 13:34-35 ''Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo. Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi.'' 

Penye umoja wa kiMUNGU hapo ndipo penye upendo sahihi.
Kama kanisa likiwa na upendo hakika na umoja utakuwa rahisi sana kuwepo.
Mwenye kanisa ambaye ni BWANA YESU anatutaka tuwe na umoja na upendo.
Ndugu kuwa pamoja kwa umoja ni kwa sababu ya upendo wa KRISTO ndani yao.
Ni vyema sana kanisa la MUNGU likawa pamoja kwa umoja.
Ni muhimu sana idara ya wamama ikawa pamoja kwa umoja.
Ni muhimu sana idara ya vijana ikawa pamoja kwa umoja.
Ni Muhimu sana wachungaji wakawa pamoja kwa umoja.
Ni Muhimu sana mashemasi na wazee wa kanisa wakawa pamoja kwa umoja.
Ni muhimu sana walimu wa Neno la  MUNGU wakawa pamoja kwa umoja.

Wefeso 4:1-6 ''Kwa hiyo nawasihi, mimi niliye mfungwa katika BWANA, mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa; kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendo;  na kujitahidi kuuhifadhi UMOJA wa ROHO katika kifungo cha amani.  Mwili mmoja, na ROHO mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu.  BWANA mmoja, imani moja, ubatizo mmoja.  MUNGU mmoja, naye ni BABA wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote.''

Asante kama unanielewa ndugu yangu.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili.

Comments